Ikiwa sisi tuliumbwa na Mungu,Je! Mungu aliumbwa na nani?

by Admin | 7 February 2020 08:46 am02

JIBU: Tukiweza kulijibu na swali hili “Ikiwa sisi tunakula ili tuishi, Je! Mungu naye anakula nini ili aishi?”…Basi tutaweza pia kulijibu hilo linaloulizwa kirahisi.

Awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa wazo lolote ambalo linakuja katika vichwa vyetu fahamu kuwa lilishawahi kuumbwa hapo kabla, Hivyo  wakati ulipofika na kuwekwa katika kichwa chako au changu, ndipo tukaliwaza, vinginevyo tusingekaa tuwe na wazo kama hilo vichwani mwetu kama hili la “Mungu aliumbwa na nani” kama halikuwahi kubuniwa na aliyetuumba.. hakuna wazo linalozuka lenyewe tu hewani, labda wewe ndio uwe wa kwanza kuligundua, ni kama kumputa tulizonazo kila kitu kilichomo ndani yake, kiliwekwa na mtu kwanza (installed)

Hivyo mpaka hapo ulipofikia kuwaza tu Mungu aliumbwa na nani, fahamu kuwa ni yeye mwenyewe alilibuni hilo wazo kisha akaliweka kwa makusudi katika ufahamu wako,..Hivyo usifikiri kuwa umegundua wazo la kumnasa Mungu, kama hilo la Mungu aliumbwa na nani,..nataka kwanza uondoe hilo akilini. Na aliamua kufanya hivyo ili wakati wake wa kufikirika ukifika ujiulize weee!!, uumize kichwa weee! kisha ukose majibu! … Wazo hilo alipenda tu ukose majibu yake, kama vile yale mengine alivyopenda upate majibu yake.

Jibu rahisi ni kuwa Mungu hatuwezi kumpima katika “wazo la kuumba au kuumbwa”..kwasababu hayo mawazo ya kuumba au kuumba aliyabuni yeye, hivyo hayawezi kuwa sehemu ya maisha yake..yeye, ni zaidi ya upeo wa fikra zetu.

Jaribu kuwazia mfano huu, unaohusiana na vitu tulivyoviumba sisi wanadamu ambavyo ni vya  elektroniki…Sasa kisa tu tumeviundia mfumo wa kutegemea umeme katika kujiendesha pale vinapoishiwa nguvu tunavichaji betri zako katika umeme.. Na kwamba visipochajiwa ni lazima tu vizime au vife kabisa, Simu zetu zinasema hivyo hivyo,  saa zetu hivyo hivyo , komputa zetu, na tochi zetu zinasema hivyo hivyo n.k..Halafu siku moja sasa eti  na vyenyewe vinaungana na kutuuliza  sisi tulioviumba maswali, vinasema Je! betri zenu ziko wapi, na mnachajiwa wapi? kwasababu hakuna maisha nje ya umeme?

Unaona lakini sisi je tunaishi kwa betri au umeme?…jibu ni la, maisha yetu yanaendeshwa na kitu kingine tofauti na wanachokifikiria, bali mambo hayo ya umeme  tumeviumbia vifaa vyetu vya elektroniki ili viishi kwayo..zaidi ya hapo haviwezi kujua jambo lingine linalotuhusu sisi..

Vivyo hivyo na sisi kwa kuwa tumezungukwa na mazingira ya  “kuumba na kuumbwa”,kila kitu tunaona ni lazima kiwe na chanzo chake ….Basi na sisi tunahitimisha na kusema Je Mungu naye kaumbwa na nani?..

Jibu  linalojitosheleza ndio hilo..Mungu hayupo katika viwango vya kibinadamu ni zaidi ya upeo wa fahamu zetu..hatuwezi kumpima katika mambo ya uumbaji.. ni sawa na leo uulize mwanga una ladha gani, au rangi ina harufu gani..na ndio maana tunapotoa jibu la mkato kuwa Mungu hajaumbwa basi ujue ni kwasababu hizo tunazozisema hapo juu….Mungu ni Zaidi ya upeo wa fikra na kwamba hatuwezi kumweka katika hilo kundi la uumbaji.

Ubarikiwe.

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?

Je! Mungu anasababisha ajali, kwamfano ajali ya kivuko cha MV Nyerere kuzama?

Kwanini Bwana Yesu, aliruhusu yale mapepo yawaingie nguruwe?

Nifanye nini ili niondokane na Hofu maishani mwangu?

Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

SI KILA KIPENDEZACHO KINATOKA KWA BWANA.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/07/ikiwa-sisi-tuliumbwa-na-munguje-mungu-aliumbwa-na-nani/