Ufisadi una maanisha nini katika biblia?

by Admin | 17 February 2020 08:46 pm02

Ufisadi una maanisha nini katika biblia? (Ufisadi ni nini? Ni uwizi wa fedha nyingi au?)


JIBU: Neno ufisadi tofauti na linavyotafsiriwa siku hizi kwamba ni mtu anahujumu uchumi wa Taifa Fulani au shirika Fulani. Lakini katika biblia tafsiri yake ni tofauti.

Katika biblia neno fisadi limetumika kumtambulisha mtu mwenye tabia ya uzinzi na uasherati uliopindukia ambao hata haujali jinsia, umri wala maadili (unahusisha chochote kile ilimradi tu ni zinaa inafanyika)..Kwa lugha nyingine (ni ukahaba/umalaya mchafu). Hivyo popote pale katika biblia linapoonekana neno hili fahamu kuwa linamaanisha “ukahaba/ umalaya wa namna hiyo”.. Kwamfano tunaweza kusoma baadhi ya mistari michache inayozungumzia tendo hilo…

Waefeso 4:19 “ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani”…..

Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”…

Maana yake ni kuwa ulevi na ukahaba/Umalaya ni pacha, vinakwenda sambamba…

Mstari mwingine ni kama huu..

Tito 1:6“ ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni WAFISADI wala wasiotii.

7 Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu”.

Maana yake ni kwamba Watoto wa Maaskofu pia hawapaswi kuwa Malaya wala makahaba wala kujihusisha na vitendo vyovyote vya zinaa. Wanapaswa wawe watakatifu katika mwenendo wao ili wawe kielelezo kwa kanisa la Mungu. Mtu yoyote anayetaka kazi ya uaskofu kama Watoto wake ni wachafu kwa viwango hivyo biblia inasema hastahili kuwa Askofu..anapaswa awageuze kwanza Watoto wake ndipo aweze kulichunga kundi la Mungu.

Pia Wagalatia 5:19 inasema… “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, UFISADI.”.. Na 2Wakorintho 12:21 pia inasema…“Nami nitakapokuja tena, Mungu wangu asije akanidhili kwenu, nami nikawasikitikia wengi waliokosa tangu hapo, wasiutubie uchafu, na uasherati, na ufisadi walioufanya”…

1Petro 4:3 “ Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika UFISADI ule ule usio na kiasi, wakiwatukana”

Mistari mingine pia ni katika kitabu cha Petro…

2 Petro 2:6 “ tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;

7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa UFISADI WA HAO wahalifu”. Kama tunavyojua miji ya Sodoma na Gomora kiwango cha uasherati walichofikia..hata kuwatamani Malaika.

Na mistari mingine mingi inazungumzia tendo hilo…Unaweza kupitia binafsi mistari ifuatayo..(Marko 7:22, Warumi 13:13, 2Petro 2:18, na Yuda 1:4).

Je! Swali linakuja….Mafisadi watakwenda mbinguni?..Jibu ni la! Kama biblia ilivyosema hapo juu…

Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, UFISADI,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,

21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.

Unaona biblia imetuonya mapema kabisa kwamba watu wafanyayo hayo hawataurithi uzima wa milele?..Je ulevi ni suluhisho la kupunguza uzinzi na uasherati?..Jibu ni la! Kinyume chake Ndio kichochoe kikubwa cha ukahaba na umalaya huo(Ufisadi). Lakini Roho Mtakatifu ndiye jawabu la kuondoa tamaa ya uasherati na uzinzi.. kama Waefeso 5:18 inavyosema.. “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”…

Je umempokea Roho Mtakatifu?..ambaye ndiye msaada wetu wa kushinda dhambi? Kama bado unangoja nini?

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU.

39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.

40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.

41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu”.

Njia ya kumpokea huyo Roho Mtakatifu ndiyo hiyo hapo juu..Kutubu kwa kudhamiria kuacha dhambi na kwenda kubatizwa….Na wewe Tubu leo, ukabatizwe katika Jina la YESU na utapokea kipawa hicho cha Roho Mtakatifu, kwasababu Mungu sio mwongo, Naye atakupwa uwezo huo wa kuzishinda hizo tamaa mbaya.

Bwana akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

KWA VILE ALIVYOKUWA MTU WA HAKI.

JUMA LA 70 LA DANIELI

JE WAKRISTO TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA VALENTINE’S DAY?

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.

NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.

TUMAINI NI NINI?

TENZI ZA ROHONI

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/17/ufisadi-una-maanisha-nini-katika-biblia/