JE SALA YA ROZARI TAKATIFU NI YA KIMAANDIKO?

by Admin | 22 February 2020 08:46 am02

Historia fupi ya Rozari kama inavyosomwa na kanisa katoliki.(kulingana na wakatoliki inajulikana kama Rozari takatifu)

Rozari asili yake ni neno la kiingereza “rosary” lenye maana ya “bustani ya maua ya waridi”…Maua ya Rose kwa kiingereza ndio yanaitwa “waridi”..Kwahiyo bustani yake ndio inayoitwa rosary.

Katika sehemu za Ulaya kuna utaratibu wa kupelekeana maua hayo ya waridi ni kama ishara ya kuonyeshana upendo (Ingawa upendo halisi hauwakilishwi kwa maua)…

Hivyo yapo maua hayo ya waridi yaliyo ya rangi ya nyekundu na Nyeupe. Hivyo wakatoliki wanaamini kuwa Maria ni mama mtakatifu kwao, hivyo anastahili kupelekewa mfano wa ua hilo la waridi..na Hivyo sala ya rozari ndio kama ishara ya kumpelekea mama huyo ua hilo jeupe la Waridi kama ishara ya upendo wao kwake.

Sasa Historia ya hiyo sala ya rozari takatifu kwa wakatoliki ilianzia wapi?

Ilianzia karne ya 3 ambapo kulikuwa na watu wanaojulikana kama wahermiti kulingana na Wakatoliki. Watu hawa waliamua kuwa wanasoma kitabu cha Zaburi kila siku SURA ZOTE 150. Lakini baadaye wakazipunguza na kukusudia kusoma sura zote 150 kwa muda wa wiki moja.

Kwa kuwa walikuwa ni watu wasio na elimu, walitumia mbegu ndogo za mimea kuwakilisha kila zaburi moja wanayoisoma..Hivyo wakawa na mbegu 150, kwa idadi ya zaburi zote 150, hivyo kila walipokuwa wanamaliza kusoma zaburi moja waliweka mbegu moja katika kapu ili iweze kuwasaidia kujua wapo zaburi ya ngapi..n.k

Baadaye kulingana na kanisa katoliki, wanasema watu hao majirani zao walivutiwa na sala hiyo ya zaburi, na wao pia wakaanza sala kama hiyo lakini wakawa wanasali sala ya “Baba yetu uliye mbinguni” mara 150, badala hiyo ya Zaburi.

Baadaye tena wakabadilika na kuanza kutumia shanga 150 zilizopitishwa kwenye kamba badala ya vimbegu vidogo  vya mimea walivyokuwa wanavitumia hapo kabla.

Ilipofika karne ya 11 kadinali wa kikatoliki Mt. Peter Damiani, aliibadilisha sala hiyo kutoka katika kusali “Baba yetu uliye mbinguni” mara 150…Na kuwa “salamu Maria” mara 150.

Baadaye tena akatokea kiongozi mwingine wa kikatoliki akazigawanya hizo sala katika makundi 15..na kila baada ya salamu Maria 10 aliiweka Baba yetu uliye mbinguni…ikiwa vile vile kamba yenye vishanga 150.

Baada ya kipindi fulani tena wakavipunguza vile vishanga na kubakia vishanga 50 tu. Hivyo ndio mpaka leo wanasali rozari yenye vishanga hivyo 50.

Lakini Je jambo hilo ni  la kimaandiko?

Jibu ni la! Si la kimaandiko kwasababu hakuna sehemu yoyote katika maandiko tumeagizwa tusali sala ya “Salamu Maria”. Kwasababu Maria si mtu anayetuombea..yeye alishakufa, wafu wote hawana habari na mambo ya maisha yetu haya…..Anayetuombea ni mmoja tu biblia imemtaja ambaye ni ROHO MTAKATIFU.

Warumi 8:26 “Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa”.

Umeona? ni Roho Mtakatifu na si Bikira Maria. Na Roho Mtakatifu hatumuombi atuombee na kusema “Salamu Roho Mtakatifu tunaomba utuombee”..hapana Roho Mtakatifu anatuombea pale na sisi tunapoomba..aidha kwa kunena kwa lugha au kwa maneno dhahiri..Yeye ni kama Mkalimani wetu mbele za Mungu. Mkalimani hawezi kuzungumza kama wewe huzungumzi.n.k

Hivyo sala yoyote inayohusisha kumwomba Mtakatifu fulani aliyekufa atuombee ni sala ya upotofu..inayowafumba watu macho na kuwafanya wawe wavivu wa kuomba wenyewe na kutamani  kila wakati kuombewa tu! Na mtu anayesali sala hiyo anamwabudu shetani bila yeye kujijua.

Hali kadhalika sala halisi inatoka ndani ya Moyo, na si desturi au utaratibu fulani au fomula fulani ya kufuata. Unapotumia mfumo fulani wa kuhesabu shanga na kutimiza idadi fulani ya maneno..hapo utakuwa husali chochote zaidi ya kutimiza wajibu tu..Na hatuendi kumwomba Mungu ili kutimiza wajibu..Mungu anataka ibada halisi inayotoka ndani ya moyo wa mtu hata kama itamchukua mtu maneno machache lakini maadamu imetoka katika moyo uliomiminika mbele zake..hiyo inathamani kubwa sana mbele za Mungu kuliko maneno elfu yasiyo na maana.

Ukitumia mfumo fulani bila kuomba kwa Roho ni sawa na umemwekea Mungu baba, nyimbo zilizorekodiwa katika kaseti azisikilize afurahi..Umeona? ukifanya hivyo ni kumdharau Mungu..anachotaka kutoka kwetu ni nyimbo zinazotoka ndani ya vinywa vyetu zinazotoka moyoni..na sio nyimbo zilizorekodiwa…Kadhalika na sala anataka zinazotoka mioyoni mwetu na si zinazojirudia rudia kama kaseti.

Hivyo kwa hitimisho..sala ya Rozari  si sala ya kimaandiko..Imebuniwa na Shetani, na lengo lake ni kuwaharibu watu kiroho. Hivyo kama upo huko ndugu..toka haraka sana!..Anza kumwabudu Mungu leo katika Roho na Kweli..Tupa hiyo rozari usiisali tena…umeshaujua ukweli, na pia washirikishe wengine wasiojua ukweli huu..

Hizi ni nyakati za mwisho shetani anatumia kila namna  kuwazuia watu wasiijue kweli. Na anawatumia watumishi wake ambao kwa nje wanaonekana ni watakatifu, wanaonekana ni watumishi wa Mungu kumbe ndani ni Mmbwa mwitu wakali.

Bwana akubariki sana.

Ikiwa bado hujaokoka na unatamani kuokoka basi hujachelewa..kumbuka kuokoka sio dini mpya..bali ni kitendo cha kumpokea Yesu maishani mwako na kufanyika kiumbe kipya..kumkiri kwamba yeye pekee ndiye njia ya kweli na mpatanishiwa wa Mungu na wanadamu. Ukimkiri namna hiyo na kudhamiria kuacha dhambi kwa vitendo na kujikana nafsi yako na kumfuata yeye…ataingia moyoni mwako na kukubadilisha na kukufanya kuwa kiumbe kipya. Hivyo tubu na baada ya kutubu nenda katafute ubatizo sahihi wa kimaandiko wa kuzamishwa katika maji tele (Yohana 3:23) na kwa Jina la Yesu Kristo.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

UPAKO NI NINI?

SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?

LITANIA YA BIKIRA MARIA JE! NI SALA YA KIMAANDIKO?

Je! Bikira Maria ni MALKIA WA MBINGUNI?

JE BIKIRA MARIAMU ALIZAA WATOTO WENGINE?

Ni sahihi kumuita Mariamu mama wa Mungu?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/22/je-sala-ya-rozari-takatifu-ni-ya-kimaandiko/