IPELEKE SADAKA YAKO MAHALI SAHIHI,ILI UBARIKIWE.

by Admin | 9 August 2020 08:46 pm08

Karibu tujikumbushe mambo machache, ambayo yanaonekana ni madogo lakini ni ya umuhimu sana, katika mapambano ya Imani.

Kuna tofauti ya sadaka na msaada. Unapomsaidia maskini huo ni msaada, na una thawabu zake mbele za Mungu..lakini sadaka ina matokeo makubwa zaidi kuliko msaada.

Sadaka ni nini?

Sadaka ni matoleo yoyote yanayohusisha madhababu!.. Katika agano la kale, sadaka iliyokuwa inakubalika kwa Mungu ni ile iliyokuwa inapelekwa mbele ya madhabahu ya Mungu katika nyumba ya Mungu…iwe ni kafara ya kondoo, au sadaka ya mazao au chochote kile. Vigezo ni lazima ipelekwe katika hema ya kukutania au katika nyumba ya Mungu.

Usipeleke sadaka yako kwa maskini, ukifanya hivyo utakuwa hujatoa sadaka bali umetoa msaada, utabarikiwa kwa ulichotoa lakini si kama ungeitoa kama sadaka. Sadaka ni lazima ihusishe madhabahu ya ki-Mungu.

Hata watu wanaokwenda kwa waganga huwa wanapewa masharti ya kupeleka sadaka..Na ile sadaka wanapewa maagizo ya kuiacha pale kwenye madhabahu zao, ili ilete matokeo wanayoyataka, kama ni kuku ataambiwa ampeleke hapo wamchinjia hapo hapo na kumwacha pale pale…Huwezi kusikia wanapewa maagizo na waganga na kuambiwa wakachinje jogoo mweusi nyumbani halafu wakawape maskini, au wakaipeleke kwa mganga mwingine,! Huwezi kusikia hicho kitu!.watakuambia leta hapa (kwenye hii madhabahu) hiki au kile kama sadaka yako, kwasababu ili kitu kiwe sadaka ni lazima kihusishwe na madhabahu.

Kwahiyo hakuna sadaka pasipo madhabahu.

Bwana Yesu alisema maneno haya katika

Mathayo 23:18 “Tena, Mtu atakayeapa kwa madhabahu, si kitu; bali mtu atakayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amejifunga”.

Maneno hayo yanaelezea uhusiano uliopo kati ya sadaka na madhababu.

Kwahiyo kama wewe ni mkristo, sadaka yako peleka kanisani na mahali unapokuzwa kiroho (kwamfano kwenye mikutano ya injili, semina n.k), ndipo utakapobarikiwa Zaidi… Bila kusahau kusaidia maskini na wenye uhitaji ambako pia kuna thawabu kubwa kutoka kwa Mungu. Lakini sadaka ina nguvu mara nyingi Zaidi ya hiyo, endapo utaelewa ufunuo wake!.. Ongeza bidii sana katika kutoa sadaka kuliko kupeleka michango yako sehemu nyingine.

Kuna fikra mbaya sana ambayo shetani kaisambaza kwenye akili za watu wengi, ambayo imewasababishia watu wengi kukosa baraka zao. Na hicho ni saikolojia ya kwamba ukiipeleka sadaka kanisani basi ni kuwatajirisha wale wachungaji na watumishi!, na hivyo ni afadhali kuipeleka kwa maskini, Hiyo ni saikolojia ya Adui, usikubali ikutawale.

Bwana Yesu alisema pia maneno haya..

Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,

24  iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.

Mambo haya yanaonekana ni madogo machoni pa wengi, lakini yana umuhimu mkubwa sana. Hivyo ni muhimu sana kuyafahamu na kuyazingatia. Zaka yako ipeleke nyumbani kwa Bwana, Sadaka zako za shukrani vilevile ipeleke nyumbani kwa Bwana.

Mungu akubariki sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 693036618/ 0789001312

Mada Nyinginezo:

TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Ubatizo wa moto ni upi?

MASOMO MBALIMBALI YA NENO LA MUNGU.

UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.

JE KUVAA PETE NI DHAMBI?

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/08/09/ipeleke-sadaka-yako-mahali-sahihiili-ubarikiwe/