HUDUMA YA WALE MASHAHIDI WAWILI.

by Admin | 31 August 2020 08:46 pm08

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, libarikiwe. Nakukaribisha katika kuyatafakari maandiko.

Tunajua kuja kwa Yesu mara ya kwanza, kulibeba siri nyingi za kuja kwake mara ya pili, kwa mfano wakati ule kabla ya Herode, kutaka kumuua Yesu pindi alipozaliwa, kulitangulia kwanza sensa kubwa kwa watu wote wa ulimwengu, ambayo ilimlazimu kila mmoja aende kwenye mji wake aliozaliwa ili ahesabiwe huko..Na ndivyo itakavyokuja kuwa kipindi kifupi kabla ya Yesu kurudi mara ya pili duniani, mpinga-Kristo ataleta utaratibu mpya wa watu wote kuhakikiwa, mfumo huu mpya ndio ile  inayojulikana kama chapa ya Mnyama ambao utamlazimu kila mmoja awe nayo, kama mtu hana basi hataweza kuuza au kununua au kufanya biashara, au kuajiriwa mahali popote..kwa urefu wa somo hilo tutumie ujumbe inbox tukutumie ..

Lakini pia kulikuwa na jambo lingine, ambalo lilichochea kwa haraka sana dhiki kutokea pale Yerusalemu pindi tu Yesu alipozaliwa. Na jambo lenyewe, lilikuwa kwa wale Mamajusi kutoka Mashariki.

Sasa ukiangalia pale, utagundua habari ya kuzaliwa kwa Yesu ilikuwa imeshajulikana hata kabla ya baadha ya watu pale Israeli kujua, utaona kulikuwa na wale wachungaji kule makondeni waliotokewa na malaika na kuambiwa wamfuate mtoto..Ni kweli walienda na kushuhudia waliyoambiwa, na pengine baaada ya pale walisambaza taarifa za kuzaliwa kwa watu wengi vijijini na mijini, lakini habari zao hazikuwa na nguvu sana, wala hazikuleta mabadiliko yoyote kwa Israeli au kwa Herode, Vivyo hivyo, walikuwepo wakina Simoni na Hana, ambao Mungu aliwashuhudia kuwa huyu ndiye mwokozi na mfalme, pengine nao walitangaza, lakini taarifa zao pia hazikufika mbali  sana.

Walikuwepo wakina Zekaria kuhani na mke wake Elisabeti, ambao walitangaza habari za Yesu na Yohana, ambazo kwa habari ya Yohana biblia inasema zilijulikana katika mji wote ule lakini bado hazikuwa na mashiko sana..Lakini tunaona kulikuwa na kundi lingine la watu, toka mbali sana, lililoleta habari,..Hilo halikuwa la watu  wa pale Israeli, bali lilitoka mbali sana, ndio wale mamajusi wa Mashariki, walioina nyota yake na kufunga safari mpaka Israeli, na walipofika moja kwa moja wakamuuliza  mfalme Herode, yupo wapi mfalme wa Wayahudi aliyezaliwa..Sasa kwa taarifa hizo Biblia inatuambia sio tu Herode zilimfadhaisha, bali na Israeli nzima. Hapo ndipo pakawa mwanzo wa sura nyingine kwa taifa la Israeli.

Mathayo 2:1 “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,

2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.

4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi”?

Sasa kama tunavyoijua habari kilichofuata pale ni Herode kwenda kuwaua watoto wote waliokuwa Bethlehemu wakati ule (kukawa na kilio kikuu Bethlehemu).

Mathayo 2:18 “Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako”.

 Lakini kabla ya kuwaua, Mama na mtoto walihamishwa, na kupelekwa Misri kuikwepa dhiki.

Sasa, katika siku za mwisho, mambo kama hayo hayo yataenda kujirudia,. Baada ya Unyakuo kupita, dunia itakuwa imebakiwa na miaka 7 tu mpaka iishe kabisa, katika kipindi hicho, Mungu atawanyanyua watu watu wawili ambao watawatenga kwa lengo moja tu, la kwenda kuwatolea Unabii Israeli, juu ya kurudi kwa Kristo ulimwenguni kutawala kama mfalme wa wafalme…ndio mfano wa wale mamajusi wa Mashariki. (Na Huo ndio utakuwa wakati wa neema kuhamia Israeli)

Watu hawa ndio wale mashahidi wawili tunaowasoma katika Ufunuo 11, Watahubiri pale Israeli, kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu kama biblia inavyotuambia,..Na wakati huo mpinga-Kristo, atawasikia, na hiyo ndio itakuwa kama alert yake, kuwa mwisho umefika.Atakachofanya ni kufanya vita na hawa watu, na kuleta dhiki Israeli, na duniani kote, hiyo ndio ile dhiki kuu,

Ufunuo 11:3 “Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, hali wamevikwa magunia.

4 Hao ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili visimamavyo mbele za Bwana wa nchi.

5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.

6 Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo.

7 Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua”.

Lakini kabla hajafanikiwa, lipo kundi dogo ambalo litasikia injili ya wale mashahidi wawili, na kuondoshwa na kwenda kufichwa, ndio wale wayahudi 144,000, hao watafichwa na dhiki kuu haitawapata (Ufunuo 7&11).

Ufunuo 12:13 “Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.

14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.

15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule.

16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake.

17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari”.

Unaona, Lakini wayahudi wengine wote, waliosalia duniani, pamoja na wale watu ambao hawakuipokea chapa ya mnyama, Watapitia dhiki kubwa isiyokuwa na mfano tangu dunia kuumbwa.

Injili inayohubiriwa sasa hivi haiwezi kutikisa au kuleta matatizo duniani, ila kipindi cha injili za hawa manabii wawili watakaposimama, na kutoa unabii pale Israeli, na kwa yale mapigo yaliyoorodheshwa pale ndipo ulimwengu utakapojua rangi halisi ya mpinga-Kristo.

Hawa watu pengine tayari wapo duniani, kwasababu dalili zote zinaonyesha.. Lakini mpaka hayo yote yatokee sisi tuliookoka ambao tumejiweka tayari, tutakuwa siku nyingi tumeshakwenda utukufuni (kanisa halitashuhudia mambo hayo ya manabii wawili). Jiulize na wewe ndugu ikiwa unyakuo utapita leo, wewe utakuwa wapi? Utajisikiaje kuona wenzako wapo mbinguni, wanaona vitu ambavyo jicho halijawahi kuona, na wewe bado upo hapa duniani, kwenye dhiki za mpinga-Kristo, ukizingatia ulihubiriwa injili mara nyingi na hukutaka kusikia?..

Je! bado unadanganywa na manabii wa uongo? Je bado, unapumbazwa na ulimwengu huu unaopita, Je! bado unasita sita kwenye mawazo mawili. Tubu kama bado hujafanya hivyo, ukabatizwe, dunia hii ipo ukingoni. Hatuna muda mrefu sana.?.

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Neno I.N.R.I kwenye msalaba wa Yesu maana yake ni nini?

VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI

https://wingulamashahidi.org/ushirikina-na-madhara-yake/

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Biblia inamaana gani kusema;aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/08/31/huduma-ya-wale-mashahidi-wawili/