Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?

by Admin | 1 September 2020 08:46 pm09

Je! Adamu alikuwa na mwanamke mwingine anayeitwa Lilith?


JIBU: Biblia imetupa majibu kama ifuatavyo..

Mwanzo 1:27 “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa MUNGU ALIMWUMBA, MWANAMUME NA MWANAMKE ALIWAUMBA.  

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”.

Huo ni mstari wa kwanza kabisa unaozungumzia uumbaji wa mwanadamu katika biblia, hakuna mstari mwingine kabla ya huu.. Na unasema Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. (maneno hayo mawili yapo katika umoja.). Na haijasema Mungu alimwumba Mwanaume na wanawake.. wala haijasema Mungu alimuumba mwanamke na wanaume. 

Kwahiyo hakukuwa na mwanaume Zaidi ya Adamu, na wala hakukuwa na mwanamke mwingine Zaidi ya Hawa katika uumbaji.

Jambo linalowachanganya wengi ambalo ndilo limezua swali hili, ni kuhusu mke wa Kaini, kwamba Kaini alitolea wapi mke?

Kwanza kabisa Ni muhimu kufahamu kuwa Adamu na Hawa, walizaa Watoto wengine wengi wakike na wa kiume baada ya Habili na Kaini. Watoto wa Adamu hawakuwa wawili tu, bali wengi.

Mwanzo 5:4 “Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake. Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa”.

Kwahiyo miongoni mwa hao Watoto wa kike aliowazaa Adamu, mmojawao ndio alikuwa mke wa Kaini, na Kaini na mkewe walizaa Watoto, na watoto wao walizaa Watoto, na wajukuu zao pia walizaa..Na wakati huo watu walikuwa na uwezo wa kuishi mamia ya miaka.

Kwahiyo ni uongo kusema kuwa Adamu alikuwa na mke mwingine tofauti na Hawa.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

BUSTANI YA NEEMA.

 

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/09/01/je-adamu-alikuwa-na-mwanamke-mwingine-anayeitwa-lilith/