Kikoto ni nini?(Yohana 2:15)

by Admin | 11 November 2020 08:46 pm11

Kikoto ni nini?


Kikoto ni aina ya kiboko mfano wa mjeledi. Tazama picha juu.

Tunaweza kuona wakati ule Yesu alipokwenda Hekaluni na kukuta watu wameigeuza nyumba yake kuwa pango la wanyang’anyi, tendo alilolifanya ni kuunda aina hii ya mjeledi, kwa kuusokota kwa kamba mbeleni. Ili awaadhibu vizuri wale watu waliokuwa wanasitiri maovu yao kule, waliokuwa wanafanya biashara zao mule ndani , pamoja na mifugo yao.

Yohana 2:13 “Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara”.

Ili kujua Bwana Yesu alimaanisha nini kusema msiigeuze nyumba ya Baba yangu kuwa pango la wanyang’anyi fungua hapa>> USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.

Hiyo ni kutuonyesha kuwa wivu wa Mungu sikuzote unaleta adhabu.

Na adhabu hii ipo kwenye makundi mawili;

Kundi la kwanza: Ni kwa wale watu wanaolinajisi hekalu lake leo hii (yaani Kanisa), kwa kufanya mambo ambayo hayana misingi ya kiimani. Mfano kuigeuza kazi ya Mungu kama biashara, kuabudu masanamu, kwenda nusu uchi kanisani, n.k.

Na kundi la pili: Ni lile la watu wanaolinajisi hekalu lake (yaani Miili yao) kwa kufanya mambo ambayo hayampendezi. Kama vile uzinzi, uuaji, ulevi, n.k. Kwani biblia inasema;

1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

19 Au hamjui ya kuwa MWILI WENU NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Na inasema tena;

1Wakorintho 3:16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Unaona? Na kikoto hichi tayari kipo mkononi mwa Bwana. Hivyo tujichunguze na sisi tumelitunzaje hekalu lake?  Kama tumekuwa tukiliharibu, ni heri tumgeukie kwa Bwana sasa, kabla ya wakati wa kuharibiwa haujafika. Kwasababu ukishafika na tukakutwa katika hali kama hizo, tujue kuwa hakuna neema tena.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya uvuvio?.

Nini maana ya kuabudu?

MOJA YA HIZI SIKU TUTAONA MABADILIKO MAKUBWA SANA.

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

MADHARA YA KUPUUZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

Mataifa ni nini katika Biblia?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/11/11/kikoto-ni-niniyohana-215/