Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)

by Admin | 23 November 2020 08:46 am11

Santuri ni nini?


Santuri ni chombo cha muziki, ambacho kiliundwa kwa nyuzi nyingi, na kilipigwa kwa vijiti viwili ambavyo viligongwa gongwa juu ya nyuzi hizo ili kutoa midundo tofauti tofauti.

Tazama video hii, uone jinsi upigwaji wake ulivyokuwa na sauti zake zilivyo.

Asili ya chombo hichi ni kutoka katika nchi za mashariki ya kati, maeneo ya Iran na kando kando ya nchi ya Iraq, (ambayo Zamani iliitwa Babeli). Lakini baadaye zikaja kuwa maarufu na kutumika mpaka katika nchi nyingine nyingi za Asia na Ulaya kama vile India na Ugiriki.

Katika biblia tunaweza kuona Santuri zikitajwa, wakati ule wana wa Israeli walipochukuliwa utumwani Babeli (Iraq ya sasa).Kipindi ambacho mfalme Nebukadreza aliposimamisha sanamu yake ya dhahabu ili watu wote waiabudu, Na siku alipoisimamisha aliamuru miziki tofauti tofauti ipigwe kutoka katika vifaa mbalimbali vya muziki, ambapo kimojawapo kilikuwa ni Santuri.

Danieli 3:4 “Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi,

5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, NA SANTURI, na zomari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha”.

Soma pia Danieli 3:10,15

Je! Na sisi tunaweza kutumia masturi katika kumwimbia Mungu?

Santuri au ala zozote zile za muziki, haijalishi chanzo chake ni wapi, vinafaa katika kumwimbia na kumsifu Mungu. Isipokuwa tu hatupaswi kuziimbwa kwa staili za kiulimwengu. Bali katika uzuri na utakatifu, Lakini vifaa kama vifaa hakina shida.

Zaburi 150:1 “Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”.

Bwana akubariki.

Tazama Ala nyingine za muziki zilizotumika katika enzi za biblia chini.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)

Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)

Matoazi na Matari ni nini? (Kutoka 15:20)

MASERAFI NI NANI?

Sanduku la Agano lilikuwa linawakilisha nini katika Agano jipya?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/11/23/santuri-ni-nini-danieli-3510/