KUSUDI LA MUNGU NYUMA YA SAFARI.

KUSUDI LA MUNGU NYUMA YA SAFARI.

Jina la Bwana YESU libarikiwe.

Tusomapo habari ya safari ya Wana wa Israeli kutoka Misri kuelekea Kanaani, tunajifunza mengi sana, lakini leo nataka tuangalie funzo moja la msingi sana.

Katika safari ile tunaona Mungu aliipiga Misri kwa mapigo kumi (10), ambayo ni mainzi, vyura, chawa, maji kuwa damu, mvua ya mawe, nzige, majipu, tauni, giza siku tatu na kufa kwa wazaliwa wa kwanza.

Kwa mapigo hayo, Misri iliharibika sana, iligeuka kuwa jangwa lisilo na mmea hata mmoja, nan chi ya magonjwa pamoja na misiba..mpaka waMisri wakakiri kabisa kuwa wamekwisha wote..

Kutoka 10:7 “Ndipo watumishi wa Farao wakamwambia, Mtu huyu atakuwa tanzi kwetu sisi hata lini? Wape hawa watu ruhusa waende zao, wamtumikie Bwana, Mungu wao; HUJATAMBUA BADO YA KUWA MISRI IMEKWISHA HARIBIKA?”

Kutoka 10:13 “Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Bwana akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.

14 Na hao nzige wakakwea juu ya nchi yote ya Misri, wakatua ndani ya mipaka yote ya Misri, WALIKUWA WABAYA MNO; HAWAJAKUWAPO NZIGE KAMA HAO MAJIRA YO YOTE, WALA BAADA YAO HAWATAKUWA WENGINE JINSI HIYO.

 15 Kwa kuwa waliufunika uso wote wa nchi, hata nchi iliingia giza; wakala mimea yote ya nchi, na matunda yote ya miti yaliyosazwa na ile mvua ya mawe; HAPAKUSALIA HATA JANI MOJA, MTI WALA MMEA WA MASHAMBA, KATIKA NCHI YOTE YA MISRI”.

Kutoka 12:33 “Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana walisema, TUMEKWISHA KUFA SOTE”.

Sasa mbali na kwamba MUNGU alifanya vile kuonesha uweza wake kwa Farao na kwa wana wa Israeli, lakini pia kusudi lingine la kuiharibu nchi ya MISRI, ni kuzuia au kuondoa HAMU ya wana wa Israeli kurejea MISRI.

Naamini kabisa kuwa endapo MISRI ingeachwa katika hali yake ya kustawi, yenye nafaka na uchumi kama mwanzo, ni hakika kuwa wana wa Israeli wangemsumbua sana MUSA katika safari ile na wengi wao wangerudi Misri baada ya kuona lile jangwa,

Lakini MUNGU alitangulia kuiharibu Misri kukawa hakuna chakula tena nyuma, wala maisha, hivyo ile hamu ya kuendelea kukaa Misri, haikuwepo tena kwa wana wa Israeli katika ile hatua ya kwanza, watakaaje kwenye nchi ambayo makao yake makuu hakuna mmea uliosalia?..

Kama tu katika hali hiyoya kuharibika bado wana wa Israeli walikuwa na vipindi vya kumtishia Musa kurudi Misri, vipi kama Misri ingekuwa bado ina ustawi ule ule, si ndio kabisa wasingevuka shamu?.

Kwahiyo tunachoweza kujifunza ni kuwa MUNGU anapoharibu mambo tuliyoyaacha nyuma wakati mwingine ni kwa faida yetu, kwamba tusitamani kurudia mambo ya nyuma..

Ukiona Mungu anakuharibia network zako za kazi haramu ulizokuwa unazifanya jua ni kwa faida yako, ukiona Mungu anakuondolea baadhi ya watu waliokuwa rafiki zako wakati upo Misri, fahamu kuwa ni kwa faida yako.

Ukiona watu uliokuwa unawategemea kipindi uko Misri, wanaanguka au wanashuka chini, ni kwa faida yako, ili kusudi wewe usirudi kuwatumainia baada ya kuanza safari yako ya kwenda mbinguni.

Ukiona shirika au  kampuni ulilokuwa unalitegemea limeanguka baada ya wewe kuanza safari ya wokovu, usiogope na kujiona kuwa una bahati mbaya, fahamu kuwa ni kwa faida yako, usirudi nyuma wala usiweke tegemeo kwa wanadamu.

Endelea mbele katika imani, wala usitazame uharibifu unaendelea huko nyuma ulikotoka..fahamu kuwa wingu la Bwana litakuwa nawe kukuongoza na kukufikisha kule alikokusudia ufike.

Kamwe usirudi Misri, na Bwana akusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Print this post

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply