Dhambi pekee inayotajwa kwenye Biblia yenye laana ya umaskini na inayofilisi ni “Uasherati”.
Luka 15:13 “Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; AKATAPANYA MALI ZAKE HUKO KWA MAISHA YA UASHERATI”.
Ukitaka kufilisika kuwa mwasherati… kila utakachokipata kitapukutika na hutajua kimeishaje.
Labda unawaza kwamba mali zitaisha tu kwa “kuonga” (kwa kuwapa makahaba). Ndio hiyo namna ya kwanza ya kufilisika, Lakini nataka nikuambie hata usipoonga pesa yoyote, ukawa unafanya uasherati bila kugharimika….nataka nikuambie kuwa bado tu utaanguka kiuchumi, utaombea na kila aina ya watumishi na kutoa kila aina ya sadaka na hautafunguliwa.
Kwasababu uasherati “unaondoa akili”
Mithali 6:32 “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake”.
Uasherati unaondoa akili ya “maendeleo”…kwahiyo hata pasipo kuonga mwanamke bado tu utafilisika, ndio maana hata wanawake wanaofanya uasherati maisha yao yanafanana tu na wanaume waasherati, wote wanasumbuka, kwasababu hata pesa wanazopewa na wanaume hazijawahi kuwasiadia chochote kwasababu tayari kile kitendo kimewatolea akili.
Haujawahi kusikia popote kahaba kapata pesa za kutosha sasa ameacha kazi hiyo na kupitia mtaji wa ukahaba wake sasa anajishughulisha na jambo jingine, wote utaona hata wapate fedha nyingi bado watarudi katika hiyo kazi.
Dhambi ya uasherati inatajwa kama ubaya mkubwa..
Mwanzo 39:9 “Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?”.
Ndugu ukitaka kufunguliwa kimaisha acha uasherati kabisa, jitenge na huyo binti unayemwita “girl friend”..kama unataka kuishi naye funga naye ndoa takatifu na halali inayojulikana na sio ufanye uasherati.
Binti, achana na huyo kijana unayemwita “boyfriend”..ukitaka kuishi naye funga naye ndoa halali ya kibiblia, lakini maisha ya uasherati unayoendelea nayo yanakuondolea akili za asili na zile zile za neema.
Matokeo ya mwisho ya uasherati ni hukumu ya MUNGU.
1 Wakorintho 6:9 “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; WAASHERATI HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti”.
Hii ndio hasara kubwa inayotokana na uasherati, (kuukosa uzima wa milele).
Ni heri ukose mali zote za duniani kuliko uukose uzima wa milele, kwani dunia inaita na mambo yake yote.
Lakini pamoja na hayo, kwanini uteseke duniani na bado uteseke baada ya kifo?.
Amua leo kumpa YESU KRISTO maisha yako, akusafishe dhambi zako na kukutakasa.
Huo uasherati ambao unaona ni mgumu kuuacha, ni kwasababu haujaokoka sawasawa, wewe fanya maamuzi thabiti ya kutubu dhambi kwa kumaanisha kuziacha, na ondoa vichocheo vyote vya uasherati katika maisha yako kama mavazi ya kizinzi ( ya kubana maungo, na mitindo yote ya kidunia).
Pia jitenge na makundi ya watu wenye mizaha, na acha mahusiano hayo yasiyo rasmi, futa namba zote za watu unaozungumza nao mambo ya kihuni, na kiri mbele yao kwamba umeokoka, uone kama Roho Mtakatifu hatakutengeneza, na uasherati wote utakufa ndani yako itabaki historia tu.
Lakini ukitubu na kuendelea kuishi maisha yale yale ya siku zote, nakuambia hitaona matokeo yoyote zaidi sana ndio utazama zaidi katika dhambi.
Ikiwa utahitaji kuokoka utaweza kuwasiliana nasi kwa namba zilizopo hapa chini na utasaidika kwa Neema ya MUNGU.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ