Nini maana Ya ‘Nimrodi alikuwa Hodari kuwinda Wanyama mbele za Bwana’

Nini maana Ya ‘Nimrodi alikuwa Hodari kuwinda Wanyama mbele za Bwana’

Tukisoma katika maandiko tunaona anatajwa mtu mmoja aliyeitwa Nimrodi, huyu alisifika kwa kujenga mataifa makubwa, ikiwa Babeli na Ashuru. Lakini katika biblia anatajwa kama alikuwa Hodari wa kuwinda Wanyama mbele za Mungu, Je! Kauli hiyo inamaanisha nini?

Mwanzo 10: 8-12  

8 Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.

11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.

JIBU: Kumbuka, Habari nzima inayozunguka sifa maisha ya Nimrodi ni kuhusu ujenzi wa ufalme wake, kwa namna ya kipekee. Kwani yeye ndiye mtu wa kwanza anayeonekana akiunda FALME. Wengine wote waliunda mataifa, lakini Nimrodi aliunda Falme.

Tofauti ya Falme na mataifa,  ni kwamba Falme ni utawala mmoja unaomiliki mataifa mengi kwa kuteka. Nimrodi aliteka mataifa mengi, kuanzia Babeli, mpaka Ashuru, na ndio hayo yaliendelea kuwa falme kubwa ambazo baadaye zilikuja kuhusika, kuwapeleka waisraeli uhamishoni.

Sasa kitendo hicho cha Nimrodi, kusogea, na kuteka, kilifananishwa na mwindaji, ajuaye kuwinda mawindo na kuyapata kifasaha. Ndivyo ilivyo kuwa kwa Nimrodi alipokwenda kuteka taifa, alifanikiwa, kupata mawindo yake. Akawa mtu mkuu.

Hivyo kauli hiyo ilikuwa ni mithali tu, ikimaanisha Nimrodi alikuwa Hodari wa kuteka ngome.

Biblia inaweka wazi vizuri kwenye Ezekieli kuhusu mfalme Nebukadreza pia.

Ezekieli 29:19 “Basi, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitampa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, hiyo nchi ya Misri; naye atawachukua watu wake jamii yote pia, na kutwaa mateka yake, na kutwaa mawindo yake, nayo yatakuwa ndio mshahara wa jeshi lake.”

Umeona, Nebukadreza mfalme wa Babeli hapo anatajwa kama mwindaji, wa mataifa. Lakini sio mwindaji wa swali au pundamilia.

Utauliza tena, kwanini iseme, alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana, kwanini mbele za Bwana, je! Alikuwa anayafanya hayo kwa ajili ya Mungu?

Jibu ni Hapana, biblia inaposema, ‘mbele ya Bwana’ haimaanishi wakati wote, kufanya kwa Bwana. Bali kitendo chochote, mtu anachokifanya, kiwe ni chema kiwe ni kibaya, vyote hufanyika mbele za Mungu. Hivyo Nimrodi, hakuwa na Mungu, alijiundia mwenyewe falme zake za kipagani.

Ni nini Bwana anataka tufahamu juu ya kisa cha Nimrodi?

Kinyume chake ni kuwa nasi tunapaswa kuwa Hodari wa kuwinda wanyawa kwa Kristo Yesu, kwa kueneza injili mfano wa mitume. Inapofikia hatua tunaweza kutoka na kupanda kanisa lingine jipya, mahali Fulani, huo ni uhodari wa kumwindia Bwana mawindo. Kila mkristo hana budi kuwa na sifa hiyo njema.

Kwa namna nyingine awe Nimrodi wa Kristo.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply