JE WAKRISTO TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA VALENTINE’S DAY?

by Admin | 16 February 2020 08:46 pm02

Je wakristo tunaruhusiwa kusheherekea valentine’s day(siku ya valentine)? siku ya wapendanao?

Valentine kulingana na Historia alikuwa ni kuhani wa kikatoliki aliyekuwa anaishi Rumi katika karne ya 3..Aliishi Wakati wa Utawala wa Mfalme wa Rumi, aliyeitwa Claudius wa pili…Huyu Claudia alikuwa mpagani na akatengeneza sheria za kuwazuia wakristo kufanya baadhi ya mambo…Historia inasema huyu Claudia ilifika wakati akatamka kuwa Wanajeshi wote wa Rumi wanapaswa wawe wamejitoa kikamilifu kwa nchi yao..hivyo hawapaswi kuoa..Kwahiyo akapitisha sheria kwamba hakuna mwanajeshi yoyote anayepaswa kuoa. Akiamini kuwa jeshi bora linajengwa na watu ambao hawajaoa.

Lakini huyu Valentine (au valentino)..hakukubaliana na hilo shauri…Hivyo akawa anawafungisha ndoa kwa siri baadhi ya wanajeshi hao..Lakini alikuja kujulikana na taarifa zikamfikia mfalme..na akahukumiwa kifo.

Wakati akiwa huko gerezani historia inasema alimpenda binti wa mkuu wa gereza aliyekuwa kipofu, na alimhudumia mpaka akapata kuona tena…Na siku yake ya kuuawa ilipofika alimtumia mwanamke aliyempenda kadi yenye sahihi hii…“kutoka kwa Valentino wako”. Na akenda kuuawa..siku hiyo ya February 14, mwaka 270.

Miaka mingi ilipopita ndio baadhi ya watu wakaichagua iwe ni siku ya kupelekeana kadi zenye ujumbe wa mapenzi kama Valentino alivyofanya kwa yule mwanamke kabla ya kuawa kwake.

Sasa hadithi hiyo inahusiana nini na ukristo?..Valentino kumtumia kadi mwanamke huyo sisi inatuhusu nini?..Je! nini kiliendelea baada ya pale?…hakuna anayejua wala historia haijaeleza…Hivyo ni hadithi tu ambazo hazina faida yoyote kwetu sisi kuzienzi wala kuzishika…zaidi zinatutoa kwenye mstari wa imani yetu..

Ni hadithi tu ambazo maudhui yake ni kuongeza maasi na maovu duniani..na karamu za ulafi ambazo biblia imetuonya katika..1Petro 4:3…na kuchochea uzinzi..

Siku ya wapendanao ni ipi?..Bila shaka ni kila siku, hakuna siku moja maalumu ambayo upendo unazidi Zaidi au unaenziwa!…Upendo upo kila siku… kama ni upendo halisi!..lakini kama sio upendo halisi..labda unaweza kuwa na siku yake moja maalumu ya kuongezwa nguvu inayoitwa valentine’s day..Lakini kwa wakristo wa kweli upendo ni kila siku, unabubujika kila siku, kila saa..

Kwahiyo “Valentine’s day” ni sikukuu za kipagani, ambayo lengo lake ni kuwafanya watu wazame katika ulimwengu zaidi..na kuwafanya waupenda ulimwengu Zaidi ya kumpenda Kristo. Siku hii ndio siku disko zinajaa watu, siku hii ndio siku ambayo idadi kubwa ya watu wanafanya uasherati, siku hii ndio siku ambayo idadi kubwa ya watu ndio wanakwenda kulewa pombe…Wala hata sio siku ya watu kwenda kanisani, sio siku ya watu kwenda ibadani kumwabudu Mungu au kusali…Ni siku maalumu shetani aliyoiandaa ya watu kuzama ulimwenguni kusambazo upendo bandia ambao hata watu ambao hawajaona wanapelekea kadi hizo..Sasa itakuwaje sikukuu ya kiMungu hiyo?. Ni ushujaa gani kauonyesha kwa ajili ya kanisa la Kristo mpaka siku yake ihadhimishwe?

Upendo tunaopaswa tuusambaze ni upendo wa Kristo, Na sio upendo wa Valentino.

Bwana atusaidie kwa hilo.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

Je! mtu anapofunga kwa muda wa SAA 24,anapaswa kunywa maji au kitu chochote?

MAONO YA NABII AMOSI.

KIFO CHA REINHARD BONKEY KINAACHA UJUMBE GANI KWETU?

NI NINI TUNAJIFUNZA JUU YA MT. DENIS WA UFARANSA?

JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.

ITAFAKARI SIKU YA HUKUMU.

Mtakatifu ni Nani?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/16/je-wakristo-tunaruhusiwa-kusheherekea-valentines-day/