ITAFAKARI SIKU YA HUKUMU.

ITAFAKARI SIKU YA HUKUMU.

Shalom, Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe…Sio vibaya tukajikumbusha mambo ambayo tulishawahi kujifunza huko nyuma au kufundishwa..Bwana katika agano la kale aliwazuia wana wa Israeli kula wanyama ambao hawacheui…kucheua kama ilivyotafsiriwa kwenye biblia maana yake sio kutoa hewa mdomoni inayotoka tumboni..au kutapika…Hapana..kucheua ni tabia Wanyama wanayokuwa nayo ambapo baada ya kula nyasi huwa wanahifadhi chakula kile katika matumbo yao na kisha baadaye wanauwezo wa kukirudisha chakula kile na kukitafuna tena na kisha kukimeza kikiwa kimesagika vyema zaidi…Sasa mnyama kama nguruwe alikuwa hacheui, hivyo ni najisi…Ikifunua tabia ya aina ya watu fulani..ambao Hawana tabia ya kukumbuka mambo waliyojifunza nyuma, wala hawana tabia ya kurudia kutafakari tena na tena..wakila wamekula, hawana muda wa kukirudia tena kukitafakari, kukitafuna tena kile chakula…Na hiyo inawafanya wanakuwa warahisi kusahau mema yote na mazuri yote ambayo Mungu alishawhi kuwafanyia huko nyuma.

Lakini tukijifunza kujikumbusha mambo tuliyojifunza huko nyuma, na kurudia kuyatafakari tena na tena tunajiweka katika nafasi nzuri ya kumshinda yule mwovu, na hivyo katika roho sisi tunaonekana ni viumbe ambavyo si najisi mbele za Mungu.

Hivyo tujikumbushe kidogo kuhusu hukumu. Tuitafakari kidogo hukumu ya Bwana Yesu itusaidie kujua hukumu yetu itakuwaje huko mbeleni baada ya Maisha haya.

Kama tunavyojua Bwana alishtakiwa na Wayahudi (yaani wa-Israeli) lakini alisulubiwa na warumi (Yaani watu wa Mataifa). Kwahiyo jamii zote mbili: Wayahudi na sisi watu wa Mataifa) tuna hatia juu ya Damu ya Yesu. Ndio maana ukombozi na msamaha unatuhusu sote. Kwasababu wote tumetenda dhambi..

Warumi 3:23 “ kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu”..

Na kama Bwana Yesu alisimamishwa mbele ya kiti cha hukumu alivyokuwa hapa duniani…Na akahukumiwa mbele ya watu wote (wayahudi na watu wa mataifa), na akatoa hesabu ya mambo yote.

Yohana 19:13 “Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha”.

Vivyo hivyo siku ile ya hukumu watu wa mataifa yote duniani nao pia watasimama mbele zake yeye katika kiti cheupe cha hukumu. Na kila mmoja atatoa hesabu ya mambo yake aliyoyafanya alipokuwa hapa duniani.

Kwahiyo ufanyalo leo kumbuka kwamba siku moja litaletwa hukumuni..

Mhubiri 12:13 “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya”.

Na zaidi tena Biblia  inasema..

Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.

12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.

13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.

14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.

15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”

Kama Bwana Yesu na ukamilifu wake wote alisimama mbele ya kiti cha Hukumu cha Herode…Sisi ni nani tuikwepe hukumu inayokuja?..Tujitahidi siku ile tusiwepo katika kundi la watu watakaohukumiwa mauti ya milele katika ziwa la moto..bali watakaohukumiwa kwa kupewa thawabu katika kuushinda ulimwengu.

Mathayo 25:19 “Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.

20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.

21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.

23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.

24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi”.

Tukikumbuka pia hakuna nafasi ya pili baada ya kifo..Mtu kaandikiwa kufa mara moja tu, na baada ya kifo ni hukumu kasome (Waebrania 9:27). Hakuna maombi yoyote yanayoweza kumwamisha mtu kutoka katika moto wa kuzimu na kumwingiza katika paradiso…Ukifa katika dhambi ndio tayari umepotea milele..Biblia inasema mti uangukiapo huko huko utalala (Mhubiri 11:3)…maana yake ukifa na kwenda kuzimu ndio huko huko utakuwepo milele.

Je umesimama katika Imani?..Unauhakika Kristo akija leo utakwenda naye. Bwana akusaidie, na Bwana atusaidie sote katika Jina la Yesu Kristo.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii 0789001312


Mada Nyinginezo:

PENGINE MUNGU ALISHASEMA NAWE KWA NJIA HII.

HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.

HISTORIA YA ISRAELI.

Kuna ufufuo wa aina ngapi?

HAKIKISHA UNALIELEWA NENO.

UWE MWAMINIFU HATA KUFA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments