Je! Ule mwiba uliokuwa katika mwili wa Paulo ulikuwa ni nini?

by Admin | 15 May 2020 08:46 pm05

JIBU: Tusome

2Wakorintho 12:7 “Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.

8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.

9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.”

Kumekuwa na mtazamo mingi juu ya mwiba uliokuwa katika mwili wa Paulo, wengine wanabaki kudhani ni mwiba halisi kabisa uliwekwa ubavuni mwake, kwamba kila anapojaribu kujivuna basi unamtoboa..wengine wanasema ni kumbukumbu ya yale mambo mabaya aliyoyafanya kule nyuma hivyo Mungu alikuwa anamletea yale mawazo yanamsononesha na hivyo yanageuka kuwa kama mwiba kwake na anaacha kujivuna.

Lakini, katika hayo yote, tukiutazama tena kwa ukaribu ule mstari wa 7, unasema Mungu alimwekea mwiba katika mwili wake “Mjumbe wa shetani”..Hilo Neno mjumbe, ni Neno linalomaanisha mtu na sio mawazo fulani au kitu fulani. Hata katika akili ya kawaida mwiba wa kijiti una uhusiano gani na kujisifu?..Hivyo hapo Paulo hakuzungumzia kijiti cha mwiba au ugonjwa fulani katika mwili wake bali alikuwa anamzungumzia mtu fulani, ambaye ndiy aliyekuwa kama mwiba kwake…

Sasa swali lingine utauliza mbona kasema ni katika mwili na sio katika roho?..Jibu ni kwamba Neno mwili linaweza kumaanisha maisha ya mtu au watu…Hebu soma mistari ifuatayo Bwana aliyokuwa anawaambia wana wa Israeli tutazidi kuelewa..

Hesabu 33: 55 “Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.

56 Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi”.

Waamuzi 2: 3 “Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu”.

Umeona hapo?..maisha ya mtu yanaweza kufananishwa na mwili, na mtu anayekusumbua na kukutesa katika maisha yako anaweza kufananishwa na mwiba mwilini mwako…

Lakini tukirudi kwa Mtume Paulo, huyu mtu ambaye alikuwa ni mwiba kwake alikuwa ni nani?

Tukisoma.. 2Timotheo 4:14 inasema..

“Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake.

15 Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.”.

Biblia haijatoa habari zake ndefu juu ya huyu Iskanda, mfua shaba. Lakini inatueleza alikuwa kikwazo kikubwa sana wa Paulo, katika maisha yake na katika huduma yake.. Hajiatumia neno “Ubaya ” tu bali imetumia neno “Ubaya mwingi”.Kuashiria ni matendo mengi mabaya huyu Iskanda alimwonyesha Paulo.

Pengine, alikuwa anamzungia Paulo kwa ubaya tu wakati wote, alikuwa anazungumzia mapungufu yake tu, jinsi alivyokuwa muuaji huko nyuma (akiwaua na kuwatesa wakristo), akimshuhudia na maneno mengine ya uongo mbele za watu waliokuwa wanamwamini Paulo..Na hiyo ikawa inamfanya Yule Paulo ambaye anasifika kwa mafunuo mengi, na miujiza mingi, na huduma kubwa, kuonekana kuwa sio kitu katikati ya baadhi ya watu waliokuwa wanamwamini.

Hilo si ajabu kuliona hata leo unaweza kuliona kwa viongozi wengi wa nchi, Mungu anawanyanyulia wapinzani kama mwiba kwao, ili wazungumze mabaya yao tu, au mapungufu yao, haijalishi kiongozi huyo atakuwa amefanya mambo mangapi mazuri ya kimaendeleo kiasi gani. Mungu anaruhusu hayo ili kiongozi huyo asijivune kupita kiasi.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Paulo kwa huyu Iskanda mfua shaba alikuwa mwiba mkubwa kwake, mpaka akamwomba Mungu amwondolee (amwue),

Soma:

1Timotheo 1:20 “Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu”.

lakini Mungu alimwambia Neema yake yamtosha..Hivyo aliendelea kubakia nao, mpaka wakati wake ulipokwisha.

Vivyo hivyo na sisi, tukiwa watu wa kujivuna, kujiona sisi ni kitu Fulani, kisa tumepiga hatua kuliko wengine, au tuna kitu kikubwa kuliko wengine. Tukumbuke kuwa Bwana anaweza kutunyanyulia miiba, kututweza..

Shalom.

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=BWMmC9aLXnY[/embedyt]

Mada Nyinginezo:

MIILI YA UTUKUFU ITAKUWAJE?

IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.

FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.

JE! TUNAPASWA KUUAMINI UNABII WA SYLVIA BROWNE?

Je kuweka mapambo kama mikufu, vikuku na kutoboa pua ni dhambi?

Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?

JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?

Je! kuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kwenye mateso ya kuzimu?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/05/15/je-ule-mwiba-uliokuwa-katika-mwili-wa-paulo-ulikuwa-ni-nini/