Hivi karibu mwanamke huyu amepata umaarufu mkubwa duniani japo alishafariki mwaka 2013, lakini kitabu chake kilichoitwa “End of days”, ambacho ndani yake kimeandika baadhi ya nabii zitakazotokea siku za mwisho, ndicho kilichomfanya ajulikane kwa haraka, na moja ya nabii hizo ni kuhusiana na mlipuko wa gonjwa ambalo kwasasa linajulikana kama Covid-19, kama wengi wanavyojua alitabiri kwa ufasaha kuwa kipindi cha mwaka wa 2020 kutazuka gonjwa linaloshambulia mapafu, ambalo litaathiri karibu dunia nzima, na akaongezea kusema kuwa hata hivyo gonjwa hilo litatoweka lenyewe kama lilivyokuja, na litarejea tena baada ya miaka 10 ndipo litakapotoweka moja kwa moja.
Lakini unabii mwingine alioutoa ambao ndio kiina cha ujumbe wa leo, ni ule aliosema, mwaka alioutaja kama “3020” Kutazuka viumbe wa ajabu duniani, ambao wataitwa “VAMPIRES” ni watu ambao watafufuka, na watakuwa wanaishi kwa kutegemea kunywa damu za watu, watakuwa hawapatani na mwanga, lakini baadaye watauliwa na hali itarejea kama kawaida. Hivyo watu wengi waliposikia hivyo mitazamo yao ikabadilika kuhusu mambo yajayo..
Lakini ulishawahi kujiuliza juu ya nabii nyingine alizowahi kuzitoa huyu mama? Siko kumkosoa lakini lipo japo nataka ujifunze mwisho wa makala hii ..baadhi ya hizo alisema..
Mwaka 2010 kutatokea Aliens (Viumbe kutoka sayari nyingine) duniani..Jambo ambalo halikutokea, mpaka sasa halipo.
Mwaka 2004, alitabiri Osama ameshakufa,.Lakini Osama alikuja kupatikana mwaka 2011 na kuuawa.
Ndani ya kitabu chake kimoja aliandika, chanjo ya ugonjwa wa HIV, itapatikana mwaka 2005. Lakini chanjo hiyo mpaka leo hii haijapatikana.
Na nyingine nyingi, ambazo hatuwezi kuzichambua moja moja kwasababu sio lengo la ujumbe huu kuwakosoa watu, lakini tufumbuke macho, tusipelekwe na kila aina ya mafunuo yanayokuja duniani siku hizi…
Sasa tukirudi kwenye lile la mwaka 3020 alilolisema kuwa kutatokea viumbe wajulikanao kama Vampires..Na hili limewafanya watu wengi waamini kwa asilimia kubwa kwamba watatokea, kwasababu tu lile la ugonjwa ufananao na nimonia (Corona) lilitokea kisahihi.. na wengine wamekuwa na mtazamo mwingine wa kuishi wakidhani kuwa hii dunia itaendelea kuwepo mpaka huo mwaka wa 3000 yeye alioutaja…
Ni vizuri ukafahamu biblia inatukumbusha kwamba hata kama unabii utatolewa na mtu fulani na ukawa sahihi kabisa, bila kuwa na kasoro kasoro lakini kama unakinzana na maagizo ya Mungu, hatupaswi kupokelewa hata kidogo kwani ni wa uongo, (Soma kumbukumbu 13)
Hivyo usikimbilie kuupokea kila unabii ukasema unatoka kwa Mungu, kisa tu umetokea! bila wewe kukaa chini na kuutathimini katika maandiko..
Hizi ni nyakati za mwisho, kuhusu janga hili la Corona wapo wengine wengi sana wametabiri kiufasaha kuhusu juu ya gonjwa hili kama ulikuwa hujui lakini hawakuwa wakristo fuatilia hata habari ya Novel ya the eyes of the darkness, utaona, wapo wengine wengi sana, watafute internet utawaona,.. Lakini Pia Mungu anaweza kumtuma mtu wake kabisa , atoe unabii na ukaja kutimia, na akatoa maagizo yanayokinzana na Neno lake, Kumbe Ni Mungu ndiye aliyemtuma ili akupime moyo wako kama kweli unalishika Neno lake au la!!.. Na kama ukifuata tu, ndio umekwenda na maji.. Hebu tusome kidogo andiko linalozungumzia mambo hayo…
Kumbukumbu 13: 1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 IKATUKIA HIYO ISHARA AU HIYO AJABU ALIYOKUAMBIA akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote”.
Kumbukumbu 13: 1 “Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu,
2 IKATUKIA HIYO ISHARA AU HIYO AJABU ALIYOKUAMBIA akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo;
3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote”.
Sasa tukirudi kwenye maandiko hakuna mahali popote panapotabiri kuhusu ujio wa “Vampires”..Au kutokea kwa viumbe vingine kutoka sayari za mbali (Aliens).. unabii huo ni batili..Hizo ni ndoto za wanasayansi ambazo zinakinzana na Neno la Mungu..
kama hayo yatakuja kutokea basi ungeshayaona kwenye maandiko tangu zamani, kwasababu hakuna jipya chini ya jua..Kwamfano tabiri za kutokea magonjwa ya mlipuko mfano wa tauni, yalitabiriwa hivyo mtu akitabiri kuhusu hilo sio jambo la kushangaza kwasababu biblia ilishaeleza, vile vile matetemeko, au njaa, au vita,manabii wa uongo, wapinga Kristo n.k. yote hayo yapo kwenye maandiko na yalishatabiriwa.. Lakini sio watu wanaofufuka na kunyonya damu za watu, watakaofufuka ni watakatifu tu, na sio kitu kingine chochote..Yesu pekee ndio UFUFUO NA UZIMA(Yohana 11:25), Na yeye peke yake ndiye mwenye funguo za kuzimu na mauti, shetani hana tena hizo funguo, hawezi kumfufua mtu wala kumleta mtu juu kama alishanyang’anywa hayo mamlaka kitambo sana…sasa jiulize atakayewafufua hao mavempire(mazombie) Wanyonye watu damu ni Bwana Yesu?..tafakari..unaona kabisa haingii akilini, ni kinyume na maandiko?…Ufufuo uliotabiriwa ni ufufuo wa wenye haki kwa ajili ya uzima na ufufuo wa waovu kwa ajili ya kuhukumiwa kwa maovu waliyoyafanya, na si kwaajili ya kunywa damu za watu!.
Yohana 5:28 “ Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Yohana 5:28 “ Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu”.
Hivyo jihadhari na udanganyifu wa ndoto za wanasayansi..
Kwa hiyo ndugu kwa maneno mafupi..Ni kwamba tunaishi katika siku za mwisho, na siku yoyote Kristo anarudi kulinyakua kanisa lake.. anayekupa matumaini kuwa kutakuwa na miaka mingine elfu moja ya kuishi mbeleni (1000), anakupoteza, ni agenda za shetani kuwaminisha watu kuwa muda bado sana, Kwamba Kristo bado sana arudi. Ilihali Dalili zote tulizoelezwa na Kristo zimeshatimia..Hivyo ni wakati wa kujiandaa sasa, acha kufuata mafunuo yasiyo dhahiri ya siku hizi za mwisho..Yapo mengi na yataendelea kuwa mengi, kwajinsi siku zinavyozidi kusogea..Ukiyafuata utayumbishwa sana, na kupotezewa mwelekeo wa imani yako kama huna msingi mzuri wa kimaandiko..Hizi ni nyakati za mwisho kweli kweli mpinga-Kristo ameshajiweka tayari kuanza kazi na sio VAMPIRE au ALIENS.
Hivyo Tubu dhambi zako leo, mpokee Kristo, kama hujamwamini, jiweke tayari kwa kurudi kwa pili kwa Kristo duniani.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
KUTAKUWA NA MATETEMEKO YA NCHI, NJAA NA TAUNI.
Kuna ufufuo wa aina ngapi?
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
KUZIMU ni mahali pa namna gani, Je! huko wanaishi watu wakifa na kwenda kupata mateso au ni vinginevyo?
Rudi Nyumbani:
Print this post
Nimependa sana masomo na ntapenda zaid kama ntatumiwa WhatsApp -0683845180 au email- chrisbrain051@gmail.com
Amen ubarikiwe..tutakuwa tunakutumia ndugu