by Admin | 31 May 2020 08:46 pm05
Rafiki wa kweli ni mmoja tu naye ni YESU..Leo tutatazama ni kwanini!.
Ni rahisi kujitoa kwa ndugu yako wa damu, kujitoa kwa mali na hali….hata wakati mwingine kujitoa hata uhai kwaajili ya ndugu yako wa damu, hilo linawezekana pia…Ndio, wengi wapo radhi wafe ili watoto wao waishi, wapo radhi wao wapitie shida nyingi na dhiki lakini wadogo zao, au wazazi wao wasipitie hizo dhiki. hilo kundi la watu lipo, tena idadi yake ni kubwa sana…
Lakini kuwapata watu ambao wanaweza kuutoa uhai wao kwaajili ya “rafiki zao”, ni wachache sana, kama sio hawapo kabisa..
Kwanini ni ngumu?..kwasababu Ndugu ni bora mara nyingi kuliko rafiki, Baba ni bora kuliko rafiki, mtoto ni bora kuliko jirani rafiki, mama ni bora kuliko rafiki n.k..kwasababu rafiki haaminiki leo anaweza kuwa rafiki yako mzuri kesho akawa adui yako tena mbaya sana…Sifa hiyo ya rafiki ndiyo inayoficha thamani ya urafiki usiwe na nguvu kuliko cha ndugu wa damu.
Lakini endapo akitokea mtu ambaye atakuwa tayari kuutoa uhai kwake kwaajili ya rafiki zake…Yaani yeye yupo tayari kufa ili tu rafiki zake wasife!…bila shaka huyo mtu atakuwa ni wakipekee sana..Kwasababu japokuwa anaujua unafiki wa marafiki lakini yupo tayari kuutoa uhai wake hivyo hivyo, hata kama anajua hao marafiki wanaweza kuja kumsaliti au kumkana baadaye.. Hakika huyo atakuwa zaidi ya rafiki…Upendo wake utakuwa umepita upendo wa ndugu..
Na huyo si mwingine zaidi ya Yesu..ambaye alikubali kuutoa uhai wake kwa sisi rafiki zake, ambao ni vigeugeu..Ndio!..alijua Petro atakwenda kumkana masaa machache tu mbeleni lakini alikubali kuutoa uhai wake kwaajili yake hivyo hivyo…Alijua Yuda anakwenda kumsaliti masaa machache tu mbele lakini alimwita rafiki..(kasome Mathayo 26:48-50).
Yohana 15:13 “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.
14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu”.
Je bado tu hujamwona rafiki wa kweli?..Yeye mwenyewe anasema HAKUNA ALIYE NA UPENDO MWINGI KULIKO HUU, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake…(Kuutoa kwa Ndugu ni rahisi lakini si rafiki).
Mimi siwezi kuwa rafiki yako wa kweli, wala yule rafiki yako wa karibu sana hawezi kuwa rafiki yako kwa kiwango hicho cha kufikia kuutoa uhai wake kwaajili yako…Je! huyo rafiki yako ukijua kwamba kesho atakusaliti ufe, je utaendelea kumpenda leo?..bado utaendelea kumwita rafiki??…
Au je rafiki yako akijua kwamba kesho utamrusha ataendelea kukuita leo rafiki? Si atakuchukia na kukuita mnafiki..je! yupo tayari kufa kwa ajili yako?..kama haweza basi sio rafiki wa kweli..ni rafiki tu! Lakini si rafiki wa kweli.
Rafiki wa kweli yupo mmoja tu…ambaye hata sasa japokuwa upo mbali naye bado anakupenda, na alishakufa kwaajili yako..
Mithali 18:24 “…. Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu”.
Hivyo msogelee huyu rafiki aitwaye YESU, yeye si mnafiki, haweki kinyongo, wala hasitisiti..amekupenda amekupenda!!..hana kusitasita..Na anamaanisha kuhitaji kuyaokoa Maisha yako.
Usimdharau, Mpe maisha yako leo kama hujampa…na utapata mema, na siku ya mwisho atakufufua na atatufufua wote tuliomwamini na kumpokea…Maana alisema mahali atakapokuwepo ndipo na sisi tutakapokuwepo.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JIRANI YANGU NI NANI?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!
CHUKIZO LA UHARIBIFU
UZAO WA NYOKA.
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
BASI, JIANGALIENI MIOYO YENU ISIJE IKALEMEWA NA ULAFI, NA ULEVI.
MASHAHIDI 40 WALIOUAWA MJINI SEBASTE, NI UJUMBE KWETU.
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/05/31/rafiki-wa-kweli-ni-yupi/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.