MADHARA YA KUTOA MIMBA.

by Admin | 5 June 2020 08:46 pm06

Madhara ya kutoa mimba rohoni.


Licha ya kwamba yapo madhara mengi ya mwilini mtu atakayoyapata kwa kutoa mimba, hata wakati mwingine kukumbwa na mauti au kuharibika kwa kizazi kabisa, lakini yapo madhara mengine ya rohoni ambayo ni makubwa zaidi ya hayo mtu atayapata ikiwa atajaribu kikifanya kitendo hicho ..Haijalishi atafanikiwa kutoa mimba mara nyingi kiasi gani bila kupata tatizo lolote la kiafya, bado lakini yapo madhara makubwa sana ya rohoni atakumbana nayo katika maisha yake yote atakayoishi duniani..

Mungu alimwambia Nabii Yeremia maneno haya;

Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”.

Natamani sana hili Neno lingezama katika moyo wa kila mwanamke ambaye anafikiria kwenda kutoa mimba.  Kwamba Kulingana na maneno hayo Mungu huwa unamwandaa mtu kabla hata hajatungishwa mimba na ndio maana anasema ‘Nalikujua’, na pale anapotungishwa, anakuwa tayari ni mtu kamili, na wakati huo huo Mungu ‘Anamtakasa’, kwa ajili ya kutimiza kusudi Fulani maalumu duniani.

Na wengine utaona wanajazwa na Roho Mtakatifu hata wakiwa bado angali wapo katika matumbo ya mama zao. Mfano mmojawapo ni Yohana Mbatizaji..

Luka 1:15 “Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye”.

Hivyo kazi ya Mungu kwa mwanadamu huwa inakamilika tangu akiwa tumboni mwa mwanamke. Sasa pale mtu anapojaribu kulikatisha kusudi hilo la Mungu juu ya kiumbe hicho cha Mungu kwa kutoa mimba, Basi moja kwa moja anakuwa ametiza dhambi kubwa sana ya UUAJI.

Anakuwa hana tofauti na wachunaji ngozi za wanadamu, hana tofuati na watoaji kafara mbele za Mungu, hana tofauti na wauaji watu, hana tofauti na mtu aliyemwekea mwenzake sumu kwenye chakula afe,.. dhambi aliyoifanya ni ile ile isipokuwa tu imechukua umbile tofauti.

Sasa kwa kuwa mtu huyo anakuwa amemwaga damu isiyokuwa na hatia.. Biblia inasema damu yake itakuwa inalia hapo ardhini daima..

Utauliza imeandikwa wapi hiyo? Kasome habari za Kaini pale alipomuua ndugu yake, Mungu alimwambia hivi..

Mwanzo 4:10 “Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi. 11 Basi sasa, UMELAANIWA WEWE KATIKA ARDHI, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; 12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani”.

Angalia hilo Neno.. “Umelaaniwa wewe katika ardhi”..Ndugu, Laana ya Mungu ni zaidi kutofanikiwa kimaisha..Ni laana ambayo itakufanya hata ujitahidije, hutakaa uione njia ya wokovu, na mwisho wa siku utaishia katika dhambi na kwenda motoni..

Lakini kuna mwingine atauliza, Mimi sikuwa na mpango wa kuzaa kwa sasa, Wazazi/Ndugu hawatanielewa Au Mimba hii nimeipata nje ya ndoa nifanyeje?.

Unapaswa ufahamu ni heri ukapitia dhiki za wanadamu kuliko kutengwa na Mungu daima..

Wapo watu katika biblia walizaliwa kwa njia isiyohalali, wakafikia hatua hata ya kutengwa na ndugu zao wa mama halali, lakini baadaye walikuja kuwa Mashujaa wa Mungu.. Nenda kamsome mwamuzi mmoja anayeitwa YEFTHA katika biblia utalithibitisha hilo (Waamuzi 11).

Hapo ndipo utakapojua kuwa kila kiumbe kina kusudu chini ya jua. Hicho kiumbe ni nani ajuaye ndio Mungu alikikusudia kije kuwa raisi wa nchi, au Mhubiri wa kimataifa.?

Ikiwa wewe ni mmojawapo uliyepata mimba, unapousoma ujumbe huu, usifikirie kabisa kwenda kuitoa kwa namna yoyote ile. Hata kama utashurutishwa na watu kiasi gani usifanye hivyo kamwe. Usijitafuta ziwa la moto.

Vile vile ikiwa wewe ni mtu ambaye umeshawahi kutoa mimba huko nyuma, au ulimshawishi mwenzako akatoe mimba basi ujue kuwa Damu ya hao uliowatoa inamlilia Mungu ardhini.. Lakini habari njema ni kuwa Nafasi ya kutengeneza upya bado unayo..

Na ndio hapo utaona umuhimu wa Damu ya Yesu Kristo iliyomwagika kwa ajili yetu, inayofuta deni la dhambi zote, ambayo inanena mema kuliko ile ya Habili..Ukimkaribisha Yesu katika maisha yako, kuanzia huo wakati ile damu yake inaanza kunena mema kwa ajili yako, mbele za Mungu, kuomba ufutiwe kosa hilo na yale mengine yote uliyoyafanya katika maisha yako.

Utakuwa mpya, kama vile hukuwahi kumkosea Mungu hapo kabla, na wala laani hizo zote hazitakuandama tena kuanzia huo wakati na kuendelea. Lakini kama hutataka kumpokea Yesu maishani mwako, basi ujue hatakulazimisha lakini fahamu kuwa laana ya Mungu itakufuata siku zote za maisha yako,. Na ikitokea umekufa ghafla leo au kesho, au baadaye, ni moja kwa moja katika lile ziwa la moto,milele.

Kwanini usimpokee leo? Haijalishi wewe ni mwislamu, au mpagani, Yesu ndiye pekee njia ya kutufikisha mbinguni..

Yohana 14:6 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.

Ukimkaribisha atakutengeneza upya na wewe utaona badiliko la ajabu atakalolileta ndani yako. Sasa Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU  MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu unayaacha na kujitenga nayo, Sasa Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana

Ikiwa utahitaji msaada zaidi wa kiroho basi utatutumia ujumbe au kutupigia kwa namba hizi hapo chini.

+255 789001312

Mada Nyinginezo:

UTAKUWA MTORO NA MTU ASIYE NA KIKAO DUNIANI.

WAKATI ULIOKUBALIKA NDIO SASA.

FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

RACA

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/06/05/madhara-ya-kutoa-mimba-rohoni/