MAKEDONIA.

by Admin | 10 July 2020 08:46 pm07

Makedonia ni mojawapo ya mataifa tunayoyasoma sana katika biblia, hususani katika ziara za mtume Paulo za kuhubiri injili katika mataifa. Makedonia ni taifa ambao mpaka sasa lipo, na linajulikana kwa jina hilo hilo makedonia (kwa kiingereza Macedonia),  taifa hili lipo kusini mashariki mwa bara la Ulaya.

Tunaweza kusoma habari zake, katika biblia na kuona kuwa taifa hili lilikuwa ni miji mikuu mitatu, nayo ni Filipi, Beroya na Thesalonike, ambayo Mtume Paulo aliiendea kuhubiri injili. Kabla ya kupita na kwenda katika taifa lingine lijulinalo kama Akaya mji wa Athene.

Sifa mojawapo ya mji huu ni kwamba watu wake walikuwa na kiu sana ya kujua habari za Mungu tofauti na watu wa miji mingine, licha ya kwamba walikuwa ni maskini kuliko makanisa mengine,(soma 2Wakoritho 8:1-3) jambo ambalo lilipelekea  mpaka Paulo kuzuiliwa kwanza na Roho Mtakatifu kuhubiri katika miji mingine iliyokuwa Asia ndogo wakati ule, kama vile Galatia na Frigia, Utasoma hilo katika..

Matendo 16:6 “Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia.

7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,

8 wakapita Misia wakatelemkia Troa.

9 PAULO AKATOKEWA NA MAONO USIKU; ALIMWONA MTU WA MAKEDONIA AMESIMAMA, AKIMSIHI, NA KUMWAMBIA, VUKA, UJE MAKEDONIA UTUSAIDIE.

10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema”.

Hivyo nasi pia tunalo la kujifunza juu ya watu hawa wa makedonia,. Kwamba tuwe na bidii katika kumtafututa Mungu, na pia tuwe watu wa kupenda kuyachunguza maandiko kwanza kabla ya kubisha pale tunapohubiriwa mfano wa watu wa Beroya walivyofanya (Maendo 17:10). Ndivyo Mungu atakavyotuona na sisi tunastahili kupokea neema ya wokovu.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

VUKA UJE MAKEDONIA UTUSAIDIE.

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

JE KUNA UISLAMU KATIKA BIBLIA?

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

KUMBUKA, VIVUKO VYA YORDANI VINAKUNGOJA MBELENI.

UFALME WAKO UJE.

IKIMBIE DHAMBI KWA GHARAMA ZOZOTE ZILE!

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/10/makedonia/