NGUVU YA SADAKA.

by Admin | 21 July 2020 08:46 pm07

Ijue nguvu ya sadaka.


Kuna nguvu ya kipekee  iliyo ndani ya sadaka ambayo watu wengi hawaifahamu.

Mungu anaweza kweli akawa ni Rafiki yako mkubwa sana, anaweza kweli akawa anazungumza na wewe, na ukaisikia sauti yake, ikikwambia nimekusikia mwanangu na nitakupa kitu Fulani..Lakini ukashangaa kitu hicho hujakipata japokuwa alikuahidia kabisa atakuwa na wewe..

Hiyo ni kutokana na kuwa ulichomwomba Mungu, hukukiambatanisha na sadaka..Leo hii nitakuonyesha mfano wa watu wa namna hiyo katika biblia ambao walimwomba Mungu sana Na Mungu akawasikia na kuwaahidia kuwa anatakuwa nao, lakini majibu yalikuja tofauti na walivyokitarajia mpaka walipogundua kuwa tatizo ni nini?….

Bwana atusaidie tuifahamu Nguvu ya Sadaka.

Hiyo ni Habari ya wana wa Israeli siku ile walipotaka kwenda kupigana na ndugu zao Benyamini kutokana na wao kuwa na tabia ya kuutamia uovu wa wazinifu, bila kuwashaadhibu. Hivyo vita vikapangwa dhiki yao na waisraeli wengine wote waliosalia, Sasa Israeli wote walimwomba Mungu aende nao ili wakawapige Benyamini, mara ya kwanza, Mungu akawajibu akawaambia nitakuwa Pamoja nanyi, nanyi mtashinda, Lakini walipokwenda walipigwa mapigo makubwa sana..

Wakamrudia Mungu wakamuuliza tena, Je utakwenda Pamoja nasi mara hii nyingine?, Mungu akawaambia ndio nitakuwa Pamoja nanyi, lakini walipoenda kapigwa, tena wakafa watu wengi kweli.

Wakamrudia tena Mungu kwa mara ya tatu, lakini safari hii hawakumrudia mikono mitupu, walimrudia kwa kufunga, na kwa sadaka nyingi sana, jambo ambalo hapo Mwanzo hawakulifanya..Kisha wakamuuliza Mungu tena Je! Utakwenda Pamoja na sisi, ndipo Mungu akawaambia, Hakika nitakwenda Pamoja na nyie..

Na kweli walipokwenda waliwapiga Wabenyamini wengi sana, wakatoka na ushindi mnono (Waamuzi 20:22-29)..Hapo ndipo walipojua nguvu ya sadaka ipo wapi!

Kwa marefu ya Habari hiyo na fundisho lake fungua  hapa usome. >>> UMUHIMU WA SADAKA.

Hata wewe, inawezekana unamtii Mungu sana, unajibidiisha sana katika kumwomba kwa bidii, lakini kwenye suala la kumtolea Mungu, hulizingatii sana, unaona kama halina umuhimu kwa mkristo, ni pengine kwasababu hukujua nguvu ya sadaka…

Ndugu Ijue nguvu ya sadaka..

Umekuwa ukimwomba Mungu akupe kitu Fulani, na muda mrefu umepita..Leo hii fahamu kanuni za kupokea kutoka kwa Mungu. Kumbuka Mungu hana shida na fedha zako..Kwasababu vyote ni mali yake, alishasema hivyo (Hagai 2:8) , lakini anataka kuona mtu anayemwomba anao moyo wa kujali..Hicho tu..

Pale unapomtolea kinono, ndipo unapougusa moyo wake Zaidi na kuona sababu ya kwanini wewe akujibu haraka kuliko yule mwingine asiyemjali?. Fedha unazomtolea Mungu, zinakwenda katika kuwabariki wengine pia rohoni,

Hivyo unapomwomba Mungu akupe, au akutendee jambo lolote, hakikisha kwa uwezo ulio nao, ambatanisha sadaka yako tena iliyo  NONO ya hicho unachomwombea… Usiombe tu Mungu nipe, gari, nipe nyumba, nipe hiki, nipe kile halafu huna mpango wa wewe pia kumtolea Mungu, nataka nikuambie, ukiwa na tabia hiyo  majibu yako yatakuwa ni ya kuchelewa sana.

Hivyo anza leo, kujifunza kuambatanisha sadaka ya kila unachomwomba Mungu, kwa jinsi Mungu alivyokujalia…

Ijue nguvu ya sadaka..

Na kumbuka pia sadaka hiyo haipaswi kupelekwa sehemu nyingine yoyote Zaidi ya madhabahuni pa Mungu.. Haipaswi kupelekwa kwa watoto yatima, au watu wasiojiweza, au kwa mtu mwingine yoyote hapana..Inapaswa ifikishwe madhabahuni pa Mung utu! yaani Kanisani kwako.

Hivyo zingatia vigezo hivyo, Na hakika utaona matokeo chanya, katika maombi yako.

Hiyo ndiyo nguvu ya sadaka.

Bwana akubariki.

Soma masomo mengine chini…

Mada Nyinginezo:

TUMTOLEE MUNGU VILE VINAVYOTUGHARIMU ZAIDI.

HALI ZETU JINSI ZINAVYOWEZA KUATHIRI UTOAJI WETU.

HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.

FUKUZA TAI WOTE JUU YA SADAKA YAKO.

KUFUKIZA UVUMBA NDIO KUFANYAJE?

NGUVU YA MSAMAHA

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/21/nguvu-ya-sadaka/