POPOBAWA NI KWELI YUPO?

by Admin | 29 July 2020 08:46 pm07

Karibu tuongeze maarifa ya rohoni. Yapo maswali machache ya kujiuliza ambayo yanaendelea katika jamii yetu..maswali hayo ni je! popobawa ni nani? Na je popobawa ni kweli yupo?..

Popobawa kulingana na waathirika wanasema ni viumbe (majini)..yanayowatokea watu usiku na kuwaingilia watu kinyume na maumbile pasipo hiari yao. Viumbe hao wanaonekana wakati wa usiku tu!..na vinawaingilia watu wa jinsia zote, wakiume na wakike pamoja na watoto wadogo.

Sasa kabla ya kujua hawa viumbe (popobawa ni nani)?..Hebu kwanza tujifunze historia ya uumbaji kulingana na biblia.

Ufunuo 12:7 “Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.

9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye IBILISI NA SHETANI, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye”.

Biblia inasema hapo huyo joka aliyetupwa chini ni shetani/ ibilisi, na hakutupwa peke yake, bali alitupwa pamoja na Malaika zake… Sasa hapo kwenye hilo neno “pamoja na malaika zake” ndio kiini cha somo hili.

Kama tunavyojua katika vita Yule kiongozi wa juu..hana tabia zinazofanana na wanajeshi wake asilimia mia…Ni wazi kuwa kila mwanajeshi anatabia yake na kazi yake maalumu..wapo wanajeshi waangani, wapo wa nchi kavu, wapo wa majini..Na katikati ya hao wanajeshi wapo wakatili sana, na wapo wenye roho ya wastani, na pia wapo wenye tabia mbaya na wapo wenye tabia za wastani…Na wanapopigwa basi wote wanakuwa wameshindwa na wanaonekana waasi…kwasababu wanashirikiana kwa kila kitu.

Kadhalika na malaika wa shetani ni hivyo hivyo, hawa malaika wa shetani baada ya kuasi na kushindwa vita mbinguni waligeuka na kuwa mapepo…sasa sio wote wanatabia zinazofanana..wapo walio wabaya sana, na wapo walio wa wastani..lakini wote ni wabaya tu!..kwasababu wanafanya kazi katika upande wa giza!..lakini wanatofautiana viwango…Na pia wanatofautiana vitu wanavyovipenda..yapo mapepo yanayopenda mazingira ya ulevi, yapo yanayopendelea mazingira ya uuaji na ukatili, yapo yanayopendelea mazingira ya uzinzi na uasherati, yapo yanayopendelea mazingira ya wizi n.k…Kama vile jinsi watu walivyo na tabia tofauti tofauti na haya mapepo ni hivyo hivyo.

Sasa pepo linaloitwa na watu “POPOBAWA” lipo katika hilo kundi la mapepo yanayofanya kazi katika mazingira ya UZINZI na UASHERATI. Kwa ufupi ni mapepo ya “uzinzi”…Lipo kundi moja na hayo mengine wanayoyaita “majini mahaba”..Yote yanafanya kazi moja ambayo ni “kupalilia dhambi ya uasherati duniani”.

Na Mapepo hayo (popobawa na mengineyo) yanaweza kuwatokea watu kwenye ndoto! Au  kwa wazi kabisa..Lakini huwa ni nadra sana kutokea kwa wazi, mara nyingi yanawajia watu kwenye ndoto. Kwahiyo hiyo popobawa ni kweli yupo?; Jibu ni ndio yupo!…anaweza kujulikana kwa majina tofauti tofauti kulingana na mahani na mahali…na pia anaweza kuonekana kwa maumbo tofauti tofauti, sio lazima aonekane na mabawa ya popo kama, anavyoshuhudiwa na watu….Ni mapepo yaliyoasi pamoja na shetani mbinguni, hivyo yanaweza kuchukua umbo lolote lile.

Sasa ni kwanini haya maroho (popobawa) yanawatokea watu na kuwafanya hayo yanayofanya?

Jibu ni rahisi sana..ni kutokana na hali za kiroho za watu!.

Mtu yeyote aliye nje ya Kristo ambaye hajaokoka anakuwa ni mlango uliofunguliwa wa kuingiliwa na roho yoyote ya mapepo…Na mapepo hayo yanayomwingilia yanaweza kumfanya chochote yanachokitaka kwa jinsi tabia zao zilivyo…kama ni pepo la uzinzi basi likimwingia litamfanya kuwa mzinzi, na hata linaweza kumtokea na kumwingilia..kama ni pepo la uuaji ni hivyo hivyo.

Hakuna mtu yoyote ambaye ameokoka kikamilifu na akasumbuliwa na hizi roho, hakuna! Kwasababu biblia inasema..Mtu aliye ndani ya Kristo “uhai wake unakuwa umefichwa” (Wakolosai 3:3).

Sasa ni namna gani unaweza kujidhibiti na hizi roho za popobawa na nyinginezo?

Kuna uongo uliozagaa kwamba unaweza kuzidhibiti kwa kuchoma ubani au udi, au kutojiangalia kwenye kioo, au kulala huku umevaa nguo, au kukesha usiku, au kulala na mfupa wa nguruwe!. Ndugu usidanganyike hakuna njia hata mojawapo ya hizo inayowafukuza au kuzidhibiti hizo roho. Dawa ni moja tu!..Ingia ndani ya Yesu UHAI WAKO UFICHWE. (Mwisho wa somo hili nitakufundisha jinsi ya kuingia ndani ya Yesu)!. Ukitumia  njia nyingine ndio utayaita zaidi badala ya kuyafukuza.

Pili utafanyaje kama tayari umetembelewa na hizi roho(popobawa) na bado zinakusumbua katika mwili na hata katika ndoto?.

Usiende kutafuta msaada kwa waganga wa kienyeji, wala usiende kutangaza…upo usemi kuwa ukienda kutangaza ndio zitaacha..nataka nikuambie tu hazitaacha!..badala yake ndio zitazidi, pengine utaona unafuu kwa kipindi Fulani lakini bado zipo ndani yako na zitaendelea kukutesa. Suluhisho pekee ni YESU KRISTO.

Sasa utaingiaje ndani Yesu Kristo! Ili usalimike na hayo mapepo?(popobawa na mengine) pamoja na kuurithi uzima wa milele.

Hapo ulipo piga magoti peke yako!..Sali sala hii kwa imani…Sema..

 “Bwana Yesu nakuja mbele zako leo, mimi ni mwenye dhambi, naomba nisamehe dhambi zangu zote, nami nawasamehe wale wote walionikosea…naomba nioshe kwa damu yako iliyomwagika pale msalabani…kuanzia leo nakupokea wewe maishani  mwangu.. Nisaidie nisiishi tena katika dhambi,  naomba uniponye na roho zote za adui kuanzia leo, roho zote za uasherati, na nyingine zote zinazoninyemelea, zisinifuate tena… katika Jina lako tukufu, jina la Yesu. Amen”

Baada ya kusali sala hii kwa imani, amini kwamba tayari Bwana Yesu kashaingia ndani yako…kuanzia sasa utaanza kuona kuna amani Fulani inaingia ndani yako..Na yale maroho ambayo leo umeyakana kwa kinywa chako tayari hayana mamlaka tena juu yako, wewe ni mshindi…Hivyo usiishi tena katika dhambi, wala usijiuhusishe na mazingira yoyote ambayo maroho hayo yanayapenda…mazingira kama kwenye disko, mazingira ya kutazama picha za ngono mitandaoni..na mengineyo..Kuanzia sasa tafuta kanisa lolote la kiroho lililo karibu nawe..Nenda huko kuanzia leo..Bwana atazungumza na wewe huko huko kupitia watu utakaowakuta huko. Pia anza kusoma kitabu cha Mathayo ili roho yako ianze kujengeka na kukua.

Bwana akubariki sana.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/07/29/popobawa-ni-kweli-yupo/