IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

by Admin | 21 August 2020 08:46 am08

Ikabodi maana yake ni “Utukufu umeondoka”

Hili ni jina ambalo alipewa mtoto wa Finehasi na mke wake siku alipokuwa anajifungua, na hiyo ni baada ya kusikia  Mume wake amekufa katika vita, pamoja sanduku la agano kuchukuliwa na wafilisti na  yeye vilevile anakaribia kufa ndipo akaona jina sahihi linalompasa huyo mtoto ni IKABODI, akiwa na maana kuwa utukufu wa Mungu umeondoka katika Israeli.

1Samweli 4:19 “Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.

20 Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama.

21 Akamwita mtoto, IKABODI, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.

22 Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa”.

Lakini hiyo yote ni kwasababu ya Makosa ya Eli kuhani mkuu kutowazuia watoto wake (Hofni na Finehasi) kuinajisi madhabahu ya Mungu, kwa kulala na wale wanawake waliokuwa wanahudumu mbele ya hema ya Bwana. Japokuwa walionywa sana lakini hawakusikia, ndipo Mungu akamwambia Eli kwa kinywa cha Samweli kuwa atafanya jambo ambalo wakisikia, masikio yao wote yatawasha..Na jambo lenyewe ndio hilo la Sanduku la Mungu kuibwa na maadui jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia ya taifa la Israeli.

Hata sasa, utukufu wa Mungu unaweza kuondoka katika kanisa Fulani(Ikabodi), ikiwa wahudumu au watumishi wa madhabahuni hiyo ya Mungu watainajisi nyumba ya Mungu kwa kufanya dhambi za makusudi, mfano wa hawa watoto wa Eli.

Vilevile utukufu wa Mungu unaweza kuondoka(Ikabodi), kwa mtu binafsi, ikiwa ataonywa mara nyingi asisikie. Ikiwa na wewe unaonywa mara nyingi auche dhambi, uache uzinzi, uache anasa, utubu umgeukie Kristo lakini husikii, upo wakati huo utukufu wa Mungu utaondoka ndani yako moja kwa moja, na siku ukiondoka basi habari yako imeishia hapo hapo kamwe hutakaa uiamini injili tena.

Hivyo ikiwa upo bado nje ya Kristo tubu dhambi zako ukabatizwe. Na Bwana atakuponya.

Kama upo tayari kufanya hivyo, fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo ya biblia kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye  namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?

USISUBIRI MPAKA MUNGU AKUAMBIE, NDIO UFANYE!

 

CHA KUTUMAINI SINA lyrics

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

EPUKA MUHURI WA SHETANI

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/08/21/ikabodi-maana-yake-ni-nini/