NJAA KUU IKAINGIA KATIKA ILE NCHI.

NJAA KUU IKAINGIA KATIKA ILE NCHI.

Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu tujifunze Biblia.
Je unaikumbuka ile habari ya mwana mpotevu?..
Luka 15:13 “Hata baada ya siku si nyingi, yule mdogo akakusanya vyote, akasafiri kwenda nchi ya mbali; akatapanya mali zake huko kwa maisha ya uasherati.
14 Alipokuwa amekwisha tumia vyote, NJAA KUU ILIINGIA NCHI ILE, YEYE NAYE AKAANZA KUHITAJI.
15 Akaenda akashikamana na mwenyeji mmoja wa nchi ile; naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe”.
16 Akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe, WALA HAPANA MTU ALIYEMPA KITU”.
Kilichomfanya huyu kijana “ateseke sana” wala si kwasababu ya “kutumia vyote alivyokuwa navyo”..kwasababu hata baada ya kiutumia vyote alikuwa na matumaini kwamba mambo yangeweza kuwa vizuri hata kwa kufanya kazi ya kuajiriwa na kupata chochote kitu.
Lakini kilichomtesa sana hata kufikia hatua ya kuzingatia kurudi kwa baba ni “njaa kuu iliyoingia katika ile nchi”.
Maana yake ni kwamba ile nchi labda mvua ilikata, kukawa hakuna chakula cha kutosha au labda mji ulizungukwa pande zote kama kipindi kile cha njaa ya Samaria.
2 Wafalme 6:25 “Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama, wakauhusuru, hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya fedha, na kibaba cha mavi ya njiwa kwa vipande vitano vya fedha”.
Hii njaa ya Samaria ilisababisha Mavi (kinyesi) cha njiwa kuuzwa kwa fedha nyingi sana..
Nashawishika kuamini kuwa kijana yule aliyetamani kula maganda ya nguruwe, alikuwa kwenye nchi yenye njaa inayoikaribia hiyo nchi ya Samaria.
Sasa kikawaida njaa ikashaingia kwenye nchi hata fedha inakuwa haina thamani tena, ni tabu kuu.
Ndivyo ilivyo kwa watu wenye kukimbia mbali na hifadhi ya MUNGU, wenye kuukimbilia ulimwengu na kumwacha Baba wa mbinguni wakiamini kuwa ulimwenguni kuna raha.
Pasipo kujua kuwa matatizo yatakuwa katika mahali wanapokaa, au katika vitu wanavyovitegemea.
Utajitumainia leo na kazi yako, lakini utafika wakati njaa kuu itaingia katika hilo shirika, katika hiyo taasisi, katika hilo kampuni utafanya nini?.
Unawategemea wanadamu na moyoni umemwacha Bwana, utafika wakati njaa kuu itaingia katikati ya hao watu unaowategemea.
Utafika wakati shida kuu zitaingia hapo shuleni unapopatumainia, hapo chuoni au taasisini ulipo, njaa itakayofanya fedha isiwe na thamani hata kama unayo tele.
Utafika wakati njaa kuu itaingia katika nchi ambapo hata fedha yako haitakuwa na thamani.
Leo hii jifunze kwa mwana huyu aliyepotea ambaye mwishoni alizingatia kurudi kwa baba yake.
Luka 15:17 “Alipozingatia moyoni mwake, alisema, Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanaokula chakula na kusaza, na mimi hapa ninakufa kwa njaa.
18 Nitaondoka, nitakwenda kwa baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako;
19 sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.
20 Akaondoka, akaenda kwa babaye. Alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona, akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana”.
Zingatia leo hii kurudi kwa Baba yako wa mbinguni, kabla ya njaa kuu kuingia mahali ulipo au katika kile unachokitegemea.
Na unarudi kwa baba kwa njia ya kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU KRISTO.
Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

YAFAHAMU NA YATENDE MAPENZI YA MUNGU.

NAMNA GANI NITAPOKEA NGUVU ZA BWANA YESU?.

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

HEKIMA YA KIMUNGU, INAINGIAJE MIOYONI MWETU?

NINI TUNAJIFUNZA KWA MWANA MPOTEVU NA NDUGUYE?

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply