Ulishawahi kutafakari kwanini yule mwanamke aliyemzaa yule mtoto wa kiume, kupewa uwezo wa kukimbilia nyikani, kama njia ya kuepushwa na joka lile?
Kwanini asichuliwe mashambani, au mjini, au milimani, kinyume chake iwe nyikani.
Ufunuo 12:13-14
[13]Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. [14]Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
[13]Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
[14]Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Nyikani ni mahali ambapo hapana uzuri wowote, hapana mahitaji yoyote ya msingi, mahali pasipovutia, kwasasa tunaweza kusema ni nyakati za ukame, ambazo huoni, jambo lolote, huoni hatua yoyote dhahiri,ijapokuwa unajitahidi sana..huoni mafanikio yoyote, huoni mazingira rafiki..
Wakati mwingine ni kipindi cha kupungukiwa kwa muda mrefu, upo pale pale.
Tunapofikia hatua hii, mara nyingi tunamlilia Mungu atuondoe huko, tunahuzunika, tunanyong’onyea, tunasinyaa kiroho, tunamlilia Mungu kwa juhudi nyingi atuvushe..
Ni kweli kabisa jangwa si zuri, lakini wakati mwingine Bwana hulitumia kutuepusha na yule mwovu. Njia pekee iliyompasa huyu mwanamke kuepushwa na joka lile, ilikuwa ni kukimbilia jangwani, na si vinginevyo.
Hivyo ujikutapo katika nyakati mbalimbali ngumu, maadamu upo ndani ya Kristo na unaendelea vema katika imani, fahamu pia huko ulipo Mungu anakuandaa na unatimiza kusudi la Mungu.
Tuwapo katika mazingira yoyote, suluhisho si kulalamika bali ni kuomba, kushukuru na kuitafuta hekima.
Bwana akubariki.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ