ITAFAKARI SANA MAUTI YA BWANA.

ITAFAKARI SANA MAUTI YA BWANA.

 
Je unajua Mauti inaweza kuza uzima?.
Unajiuliza “mauti inawezaje kuzaa uzima, na ili hali yenyewe haina uzima”.
 
Jibu ni ndio inawezekana kabisa kwani Mauti ya Bwana YESU ilizaa uzima.
 
Tofauti na inavyotafsiriwa na baadhi kuwa kifo cha Bwana YESU kilikuwa ni “msiba” , lakini ukweli ni kwamba kufa kwa Bwana YESU hakikuwa msiba wala simanzi kwetu na wala Bwana YESU, hajawahi kuitwa marehemu wala hayati.
 
Bali kifo chake kilikuwa ni shamgwe na mpango kamili wa MUNGU, katika hatua za kumkomboa mwanadamu aliye dhambini.
 
Kivipi?
 
Unakumbuka kifo cha Elisha kilivyoleta uzima kwa yule mmoabi aliyekufa?…
 
Tusome…
 
2 Wafalme 13:20 “Elisha akafa, nao wakamzika. Basi vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi mwanzo wa mwaka.
 
21 Ikawa, walipokuwa wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi; wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka, akasimama kwa miguu”
 
Umewahi kujiuliza inawezekanikaje maiti kuifufua maiti yenzake?.Lakini jambo hilo liliwezekana kwa mifupa ya Elisha. (Mauti ilizaa uzima).
 
Sasa kama kupitia Mauti ya nabii Elisha Mungu alishawahi kutenda muujiza mkubwa kiasi kile wa kufufua maiti vipi Mauti ya Bwana YESU?.
 
Ni wazi kuwa Mauti ya Bwana ina muujiza mkubwa kuliko huo wa Elisha, kwani Elisha alimfufua mmoja tu, bali Bwana YESU atawafufua maelfu watakaomwamini.
 
Je unataka kufufuliwa baada ya kifo?
Kama unatamani kutokea na kuishi tena baada ya maisha haya kupita, chagua leo njia njia ya uzima ya kumwamini Bwana YESU na kutuvu dhambi kwa kumaanisha kuacha kabisa makosa.
 
Kumbukumbu la Torati 30:15 “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya”.
 
Hakuna “shortcut” ya kwenda kumwona MUNGU, njia ni moja tu iliyonyooka na ni nyembamba, nayo ni YESU KRISTO.
 
Mathayo 16:24 “Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
 
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
 
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake? 
 
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake” .
 
Kama bado haujampokea YESU(haujaokoka), wasiliana nasi kupitia namba tajwa hapo chini, tutakupa mwongozo utakaokufaa, lakini kama tayari umeshampa YESU maisha yako, basi nakuombea uendelee mbele kwa bidii na Roho Mtakatifu akuongezee Neema.
 
Shalom.
 
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply