Jina la Bwana wetu YESU KRISTO libarikiwe, karibu katika kujifunza Biblia.
Upo usemi usemao “wanadamu tumeumbiwa maradhi”..Usemi huu ni wa hekima za ulimwengu, ambao Biblia inasema ni upuuzi mbele za Mungu (1Wakorintho 3:19).
Ni kweli maradhi yapo lakini hatupaswi kuyakiri na kuyakumbutia kama sehemu yetu, (ikiwa tumeshampokea YESU) ….hata kama yapo ndani yako si sahihi kusema “hayo ni ya kwako” au “umeumbiwa”, ni kauli ambayo ni hatari sana.
Kwanini Maradhi si sehemu yetu tuliomwamini YESU? Na kwanini hatupaswi kutawaliwa nayo?.
Hebu tujifunze kidogo historia ya Maradhi mabaya na hatari kibiblia.
Kipindi wana wa Israeli wanatoka MISRI, kuelekea nchi ya Ahadi, Kanaani, Mungu aliwaambia yale maradhi yaliyokuwa yanawapata MISRI hayatawafuata Kaanani..
Kumbukumbu 7:15 “Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako MARADHI YO YOTE MABAYA UYAJUAYO YA MISRI, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao”.
Maana yake ni kwamba wakiwa Misri pamoja na kwamba walikuwa katika utumwa wa mwilini lakini pia Misri ILITAWALIWA NA MAGONJWA YA KUTISHA (Soma Kutoka 15:26 na Kumbukumbu 28:60).
Misri haikuwa sehemu salama kiroho na hata kimwili, kulikuwa kuna mlipuko wa magonjwa ya ajabu na ya kutisha, ambayo hayo yalitokana na miungu wa Misri waliyokuwa wakiiabudu..Na Bwana aliwaonya wana wa Israeli kwamba wakirudi kuitumikia hiyo miungu basi yale maradhi ya MISRI yatavuka kuwafuata waendako.
Kumbukumbu 28:60 “Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. 61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.
Kumbukumbu 28:60 “Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa”.
Kwahiyo tunachoweza kuona ni kuwa “Magonjwa yote asili yake ni Misri”, na Mungu aliyaweka kwa waMisri kutokana na maisha yao ya kuabudu miungu (shetani)..
Sasa swali kwanini yatutawale sisi ambao hatuabudu miungu ya Misri, na wala hatupo Misri, vile vile kama yanavyowatawala waMisri (watu ambao hawamjui Mungu)?
Ni swali la kutafakari sana..
Ukiona kuna ugonjwa unakusumbua miaka mingi, na umejaribu kutumia matibabu ya hospitalini yaliyo halali lakini tatizo linabaki kuwa sugu, au linakwenda baada ya muda linarudi..hebu wakati wa leo simama na kusema “imetosha”.
Huenda hujajua tu haki yako ndio maana ibilisi anakutesa na kukusumbua…anakujengea saikolojia kwamba huo ugonjwa ni wa kwako na huwezi kupona.. Leo hii simama na kusema “Magonjwa ya Misri si sehemu yangu”.
Kama umeokoka kweli kweli, usikae ukiri kwa kinywa chako, au uamini moyoni mwako kuwa “magonjwa ni sehemu yako”.. anza kuanzia leo kufuta kalenda za kwenda hospitali hospitali kila mara.
Tatizo linalowakabili watu wengi waliookoka ni kuamini na kujiwekea matumaini katika madawa na mahospitali, sio vibaya kuamini hivyo, lakini kunadumaza imani yako kwa MUNGU na kuyapa nafasi magonjwa ya Misri juu yako.
Si kila dalili tu ya mafua unayoyasikia unakimbilia dawa!..si kila homa tu inayokupata unakimbilia hospitalini utaacha lini hiyo tabia?.. Hufanyi dhambi lakini unadumaza imani yako.
Jenga tabia ya kuamini kuwa ninaweza kuwa na afya na uzima bila ya madawa wala hospitali, kwasababu wewe sio Mmisri, kwahiyo Maradhi ya Misri hayakuhusu, wala taarifa za maradhi ya Misri si sehemu yako.
Afya yako ni ya muhimu sana, ukiwa na maradhi hata uwezo wako wa kiutendaji kiroho unakuwa hafifu, hivyo usikubali hata kidogo, maandiko yanatufundisha hivyo kwamba ni mapenzi ya Mungu tuwe na afya zetu..
3Yohana 1:2 “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”
Ikiwa una maradhi yanayokuonea leo kwa imani fuatisha maneno yafuatayo na yatakuacha haraka sana..
Sema “Bwana YESU ninasogea mbele zako, ninaomba unisamehe nilipofungua mlango wa maradhi katika maisha yangu, lakini pia naomba unisamehe nilipopungukiwa imani, siku leo ninakiri uzima na afya, ninayakataa maradhi yote ya Misri juu ya mwili wangu, kwakuwa mimi sio Mmisri, kuanzia leo mimi ni mzima na wala sitasumbuka tena, ninaomba na kuamini katika jina kuu lako Bwana YESU KRISTO. Amen”
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nini maana ya kuinuliwa juu ya nchi? (Yohana 12:32).
JINSI MATENDO YA IMANI YANAVYOWEZA KULETA UTAMBULISHO MPYA KWA MTU.
UTAIKUZAJE IMANI NDANI YAKO?
Je ni kweli imani ya mtu ndiyo itakayomuokoa, na si kitu kingine?
Je! Imani ya mitume ipo katika maandiko?
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ