Je! Imani ya mitume ipo katika maandiko?

Je! Imani ya mitume ipo katika maandiko?

Imani ya mitume (Apostle’s creed), inapatikana wapi kwenye biblia?


Imani ya mitume ambayo unaisikia mara kwa mara ikikiriwa katika baadhi ya madhehebu hususani Katoliki, Lutherani, na Anglikana, haipo mahali popote katika maandiko, na wala haikuwahi kukikiriwa na mitume wa Kristo sehemu yoyote.

Imani hii, ilikuja kuaandikwa miaka mingi mbeleni(zaidi ya miaka 300),baada ya mitume kuondoka, waliiandika wakizingatia kiini cha wazo kuu la mitume walichokuwa wanaamini  katika maandiko.

Na kimsingi imani hii ipo kimaandiko. Hivyo mtu kuikiri hakuna shida, kwasababu haimpotezi katika misingi ya imani ya biblia.

Inasema hivi.

Namwamini Mungu Baba mwenyezi, muumba wa mbingu na nchi, na Yesu Kristo, mwana wake wa pekee, Bwana wetu.

Aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Akazaliwa na bikira Mariamu. Akateswa zamani za Pontio Pilato. Akasulubiwa. Akafa. Akazikwa.

Akashuka mahali pa wafu. Siku ya tatu akafufuka. Akapaa mbinguni. Ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba mwenyezi. Kutoka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.

Namwamini Roho Mtakatifu, kanisa takatifu lililo moja, ushirika wa watakatifu, ondoleo la dhambi, ufufuo wa wafu na uzima wa milele.

Amina.

Jambo la kuzingatia ni kuwa, ukiikiri/usipoikiri sio tiketi ya wewe ni mkristo, au utakwenda mbinguni, huu ni utaratibu tu au mapokeo tu ya baadhi ya wakristo. kitachokufa wewe uwe mkristo, ni kuamini, kutubu na kuoshwa dhambi zako kwa damu ya YESU Kristo, kwa njia ya ubatizo( sawasawa na Matendo 2:38).

Na ubatizo sahihi wa kimaandiko ni ule wa kuzamwishwa katika maji mengi,(Yohana 3:23) na kwa jina la Yesu Kristo.

Hivyo kama utahitaji upate ubatizo huu sahihi.  Na Kama utapenda tuwe tunakutumia masomo  ya biblia  kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

 Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?

Je mtu akifa anakuwa hana dhambi tena?

KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.

FANYIKA SIPORA WA KRISTO, UNYAKUO UPO KARIBU.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Leave a Reply