Swali: Biblia inasema “Tukiongozwa na Roho hatupo chini ya sheria”(Wagalatia 5:18) maana yake nini andiko hili?
Jibu: Tuanzie ule mstari wa 16 ili tuelewe vizuri..
Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria”.
Wagalatia 5:16 “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.
18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria”.
Awali ya yote ni vizuri kujua roho inayozungumziwa hapo ni roho gani?.. si roho ya mtu, bali roho ya MUNGU (Yaani Roho mtakatifu) ndio maana imeanza kwa herufu kubwa… maana yake “Tukiongozwa na Roho Mtakatifu hatupo chini ya sheria”
Sasa anaposema “tukiongozwa na Roho hatupo chini ya sheria” haimaanishi kuwa tunapookoka basi tuna ruhusa ya kufanya kila kitu, au kutenda jambo lolote, au kuvaa vyovyote au kuishi vyovyote, na kwamba tupo juu ya sheria.
La! Hiyo sio tafsiri yake.. ili tuelewe vizuri maana au tafsiri halisi ya andiko hilo, hebu takafakari mfano huu.
Mwalimu wa Hisabati anawaambia wanafunzi wake kuwa “Mkitumia kikokoteo (yaani calculator) hamtateseka na kanuni/sheria za mahesabu”.. maana yake ni kwamba mtafanya mahesabu yale yale lakini katika urahisi, lakini si kukwepa mahesabu… ikiwa na maana kuwa ile calculator inarahisisha kufanya mahesabu bila mwanafunzi kutumia kanuni.
Ni ivyo hivyo katika hilo andiko anaposema “Mkiongozwa na Roho hampo chini ya sheria”… maana yake sheria za kumcha MUNGU ambazo kwa udhaifu wa mwili ni ngumu, kama vile zile sheria za hisabati, kwa kupitia Roho Mtakatifu zinakuwa nyepesi.
Maana yake kama Biblia imesema “Usizini” au “Usiseme uongo”… kutimiza sheria hiyo ya kukaa bila kudanganya au bila kufanya zinaa ya nje au moyoni ni ngumu.. lakini kwa msaada wa Roho Mtakatifu inawezekana kutimiza sheria hiyo kirahisi,
Ndio maana hapo kwenye mstari wa 16 anasema “Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili”.
Na hapa ndipo tunapoona umuhimu mkubwa wa kujazwa Roho Mtakatifu kama Biblia inavyotufundisha..
Waefeso 5:18 “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho”.
Watu waliojaa Roho Mtakatifu kweli kweli hawaoni shida kuishi maisha matakatifu yasiyo na dhambi, wengine wote wanaweza kuwashangaa wanawezaje kuishi bila wizi, matusi, rushwa, zinaa, ulevi na bado wanayafurahia hayo maisha, pasipo kujua siri kuwa ni Roho Mtakatifu aliye ndani yao, anawasaidia udhaifu wao.
Na ili tujae Roho Mtakatifu ni lazima tufahamu kanuni ya kumpata Roho Mtakatifu, kama tu ili tupate kikokoteo wepesi (calculator) itakachotusaidia kutatua mahesabu magumu kwa haraka na wepesi ni lazima tujue jinsi ya kuipata au mahali pa kuipata na gharama zake.
Sasa tunampataje Roho Mtakatifu ili tuwezi kuishi pasipo sheria??
Tunampata kwa kanuni ifuatayo..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Kwa njia ya kutubu dhambi kwa kumaanisha kuiacha!, na kubatizwa kwa Maji mengi kwa jina la Bwana YESU, yule Roho ataingia ndani ya kuwezesha uwezo huo mkubwa wa kuishi kwa utakatifu bila mapambano makubwa moyoni.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho Mengine
ZIDI KUTAFUTA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.
Ahadi Ya Roho Mtakatifu.
KUWA NA MAFUTA YOTE YA ROHO MTAKATIFU NDANI YAKO.
ZIFAHAMU KARAMA 9 ZA ROHO MTAKATIFU NA UTENDAJI KAZI WAKE.
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ