NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 1 (MAPENZI YA  MUNGU)

NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 1 (MAPENZI YA  MUNGU)

 

Jina la Bwana YESU libarikiwe, karibu katika kujifunza Neno na Maombi. Kusoma Neno bila Maombi, au kuomba bila Neno ni sawa na kitamba cha bendera kisicho na mlingoti, kupitia mfululizo huu wa tafakari tutapata mwongozo sahihi wa kuomba kupitia maandiko ya kwenye Biblia.

MAPENZI YA MUNGU.

Bwana YESU alisema si kila aniambiaye Bwana Bwana atakayeingia katika ufalme, bali yule afanyaye mapenzi ya Baba wa mbinguni.

Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?

23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.

Sasa basi kama kigezo cha kuingia mbinguni ni “KUFANYA MAPENZI YA MUNGU”, hivyo tukimwomba MUNGU atusaidie kuyajua na kuyafanya mapenzi yake tutakuwa tunaomba jambo sahihi kabisa.

  1. OMBA KUYAJUA MAPENZI YA MUNGU KWAKO (Tumia dakika 30)

 

  1. Katika Eneo la kiroho.
  • Hapa utaomba Bwana akufunulie uyajue mapenzi yake katika kazi yake ya huduma, na wapi unapaswa utumike na utumikeje, pia kama bado haujaifahamu karama yako, mwombe Bwana akufunulie.
  1. Katika Eneo la kimaisha.

– Hapa utamwomba Bwana akufunulie kuyajua mapenzi yake katika kazi unazozifanya au elimu, ni kipi sahihi unapaswa ukifanye ukiwa hapo kazini, ni watu gani sahihi unapaswa ushirikiane nao ili usifanye kinyume jambo nje na mapenzi ya MUNGU pia kama unatafuta kazi, basi omba MUNGU akakufunulie kazi sahihi na kukuongoza hapo.

               iii.        Katika eneo la kifamilia.

                           – Hapa omba Bwana akakuoneshe mapenzi yake kuishi na mke, mume, na watoto, au wazazi pia ombea wanafamilia yako wote wakayajue mapenzi ya MUNGU na kuyafanya.

 

  1. OMBA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU. (Tumia dakika 30)

Utauliza katika kuyatenda mapenzi ya MUNGU kuna haja ya kuomba?. Jibu ni Ndio! Kwasababu pasipo yeye kutusaidia sisi hatuwezi kufanya lolote. (Soma Yohana 15:5).

  1. Katika Eneo la kifikra
  • Hapa utaomba Bwana akakusaidie fikra zako, Bwana akakupe uwezo wa kufikiri yanayompendeza yeye kila wakati akilini mwako (Waefeso 5:10).

 

  1. Katika eneo la Viungo
  • Hapa mwombe Bwana akusaidie viungo vyako kama mikono, miguu, macho, masikio viwe vyepesi katika kufanya mapenzi ya MUNGU, baada ya kuyajua mapenzi ya MUNGU, ikiwa na maana kwamba miguu yako iwe tayari kukimbilia kuyafanya mapenzi ya MUNGU, mikono yako iwe tayari na mwepesi kufanya mapenzi ya MUNGU, macho yako yawe tayari kufanya mapenzi ya MUNGU.

 

  1. KEMEA KILA ROHO INAYOKUZUIA WEWE KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU.

Zipo roho za adui zinazozua kuyafanya mapenzi ya MUNGU, roho hizi zinazuia fikra zako za ndani zisifikiri, wala kupenda kuyafanya mapenzi ya MUNGU, ndio hapo utatamani kwenda kushuhudia habari za wokovu, ndani ya fikra zako woga unaingia au aibu au kukosa ujasiri, tumia muda kuzikemea.

 

Pia zinazuia viungo vyako visiwe tayari kufanya mapenzi ya MUNGU, ndio hapo utatamani kwenda kuhubiri au kwenda kufanya kazi yoyote iliyo halali na ghafla udhaifu wa mwili utaingia kama uchovu, uvivu, au ugonjwa. Hivyo chukua muda kukemea roho hizo na Bwana atakufungua.

 

1Petro 4:2 “Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.

3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana”.

 

Bwana akubariki usikose sehemu ya Pili ya Mwongozo huu wa Neno na Maombi, kwa msaada zaidi wasiliana nasi kwa namba tajwa hapa chini.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply