Mwanzoni nilidhani kilchowafanya mitume washindwe kumtoa yule Pepo ambaye alimvaa yule kijana, na kumtupa majini, ni uwezo wa pepo yule. Kwamba alihitaji kiwango cha juu zaidi cha kiroho ili kumshinda ambacho hicho kinakuja katika mifungo na maombi mengi kama Bwana Yesu alivyosema.
Marko 9:28-29
[28]Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa? [29]Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.
[28]Hata alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?
[29]Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.
Lakini uhalisia ni kwamba sio kuwa pepo lile lilikuwa na nguvu nyingi za ukinzani. Bali lilikuwa ni sawa tu na mapepo mengine ambayo walishawahi kukutana nayo huko nyuma, na huwenda hata yale yalikuwa ni yenye nguvu zaidi ya hili, lakini waliyatoa yote, na hapa wameshindwa…walijiuliza sana, mpaka wakaenda kumuuliza Yesu.
Ndipo Yesu akawaambia namna hii haiwezi kutoka isipokuwa kwa kuomba.
Hapo anaposema isipokuwa kwa kuomba, hamaanishi kuwa kiwango chao cha maombi kipo chini, lakini hasaa analenga “Utegemezi” wao kwa Mungu umeshuka.
Ikumbukwe kuwa wakati mfupi nyuma, Yeye alikuwa mlimani siku tatu, uwepo mwa Mungu, usiku na mchana anamtafakari Mungu lakini ni wanafunzi tu watatu walioongozana naye, ambao ni Petro, Yohana na Yakobo. Wengine wote waliosalia hawakuwepo, wapo bize na huduma, muda wa utulivu na Mungu hawana, muda wa kudumu magotini kujinyenyekeza kwa Mungu umefinywa .
Hawakujua kuwa utegemezi wao wa jana sio sawa na wa leo, ndio hapo wakashindwa kutoa pepo.
Hivyo wakajifunza, kuwa pamoja na huduma lakini pia kuwepo uweponi mwa Bwana kimaombi ni muhimu vinginevyo tutashindwa kutatua matatizo mengi ya kihuduma.
Nasi tujue nguvu za jana, haziwezi kuwa za leo, ikiwa hatatuendeleza utegemezi wetu kwa Mungu.
Inawezekana kabisa ukaitatua hiyo changamoto leo kwa ushindi wote, lakini kesho ikakushinda, ukapona leo, lakini kesho ugonjwa ukakurudia..
Ukatoa pepo leo lakini kesho ukashindwa, angalia utegemezi wako umeyumba kiasi gani..
Kisha rudisha ile namna yako ya ukaribu na Mungu, pata muda wa utulivu mwingi, kutafakari Neno, kuomba, kufunga, kuimba na kuabudu, na kuisikia sauti ya Mungu, hiyo yote ndio inaitwa kuomba…fanya hivyo mara kwa mara..hatimaye kile kilichokuwa kionanekana kama ni changamoto kinatatulika tena.
Tatizo sio nguvu, tatizo ni kiwango cha utegemezi wako. Kwasababu nguvu tayari zipo hazijatengenezewa njia ya kutoka.
Shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ