2 Samweli 6:22
[22]Kisha nitakuwa hafifu zaidi, nami nitakuwa mnyonge machoni pangu mimi mwenyewe; lakini kwa wale vijakazi uliowanena, kwao nitaheshimiwa.
Pale kiongozi anapokubali kuwa dhaifu machoni pake mwenyewe ndio mwanzo wa yeye kuwa na heshima machoni pa watu wake.
Kinyume chake ni kweli pale kiongozi anapotaka kujiwekea heshima yake mwenyewe ndivyo anavyokuwa dhaifu machoni pa watu anaowaongoza.
Mke wa Daudi alidhani Daudi atadharauliwa kwa kucheza cheza na kuruka-ruka mpaka nguo kumtoka mbele za Bwana na watumishi wake. Lakini kinyume chake, kumbe ndivyo walivyompenda na kumthibitisha zaidi.
Daudi alikuwa ni kiongozi wa kiroho wa watu, sio mfalme tu wa watu, haikuwa rahisi kumtofautisha na mtu mwingine yeyote, katika bidii yake ya kumtafuta Mungu, hakukitanguliza cheo alichokuwa nacho, palipostahili kufunga sana na kuomba alifunga, palipostahili kulia alilia na kuvaa nguo za magunia, palipostahili kuimba aliimba kwa nguvu zake zote hadi nguo kumdondoka.
Alitenga mambo ya ufalme na ibada, alionyesha bidii kuwathibitishia watu kuwa yeye ni mnyonge, na mdhaifu, mbele ya macho yake mwenyewe, ndio maana mke wake akamdharau. Akasema mimi siwezi kuitwa mke wa mfalme wa namna hii, asiyejitofautisha na vijakazi wake, ambaye haeleweki kama ni mfalme au mchungaji.
Unyenyekevu aliokuwa nao, alipokuwa mchungaji wa kondoo, ndio huo huo aliendelea nao alipokuwa mchungaji wa watu. Katika namna ya kimwili alionekana dhaifu, tofauti na wafalme wengine, waliokuwa wanajivunia majeshi, Daudi alijivunua Jina la Bwana.
Halikadhalika wewe kama kiongozi wa kiroho, Je!, unaweza kuwa si kitu, kwa mambo unayoyatenda kwa Mungu wako, yanayopelekea mpaka wengine kukudharau, kwa kusema unajishusha daraja?
Bwana atusaidie.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ