Je! Naweza nikawa nimepokea Roho Mtakatifu na bado nikataabika na dhambi?

Je! Naweza nikawa nimepokea Roho Mtakatifu na bado nikataabika na dhambi?

Jibu ni ndio endapo hutatajua tabia za Roho Mtakatifu.

Katika biblia tunaona Petro alipokea Roho Mtakatifu, siku ile ya Pentekoste pamoja na watu wengine,  lakini baadaye mtume Paulo anamkemea kwa dhambi ya unafki, ya kula na mataifa, wakati akaapo nao lakini pale wayahudi wanapokuja kuketi naye anajitenga nao.(Wagalatia 2:11-14)

Hiyo ni kutuonyesha kuwa mtu anaweza akapokea kweli Roho Mtakatifu lakini bado akasumbuliwa na dhambi fulani.

Je! Hiyo husababishwa na nini, ilihali tunajua alipo Roho Mtakatifu dhambi haimtawali mtu?

Ni vema kujua kuwa ipo tofauti ya mtu kuwa na Roho Mtakatifu,  kujazwa Roho na kuenenda kwa Roho.

Pale mtu anapookoka moja kwa moja hupokea Roho Mtakatifu, lakini ili Roho huyo awe na nguvu ndani ya Mtu, kupokea tu haitoshi bali anapaswa ajazwe,(Waefeso 5:18) lakini sio tu kujazwa bali ajifunze kuenenda kwa Roho, akihakikisha kuwa hamzimishi ndani yake.

Kuenenda kwa Roho ni kutembea na Roho Mtakatifu wakati wote. Ni rahisi mtu kujazwa Roho awapo katika mazingira fulani tu maalumu labda kanisani, au kwenye mifungo au maombi. Lakini kuenenda kwa Roho ni kumruhusu atembee na yeye kila mahali awapo. Ambapo itathibitika kwa tabia ya mtu ya kujikana nafsi, kujichunguza,  kuomba, kujitahidi kuliishi Neno katika mwenendo wake wa kila siku. Mtu wa namna hii akisimama vema Roho wa Mungu humjawa na kumsaidia kushinda wingi wa dhambi.

Na hivyo kamwe hataweza kusumbuliwa na dhambi ya namna yoyote. Hivyo tukirudi kwa Petro. Ni wazi kuwa eneo mojawapo alilegea ndio maana akanaswa na dhambi ya unafki.

Wagalatia 5:16

[16]Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 

Hivyo tujue kuwa kwa jinsi tunavyompa Roho Mtakatifu nafasi mioyoni mwetu ndivyo ambavyo, tunapokea nguvu ya kuzishinda dhambi kirahisi, lakini pale tunapomzuia ndivyo tunavyoanza kulemewa na dhambi.

Pokea Roho, jazwa Roho, enenda kwa Roho, usimzimishe Roho, usimhuzunishe Roho. Utaushinda ulimwengu. 

Tukitembea na mambo yote hayo. Roho ni thabiti kwetu

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply