Ukisoma Injili ya Luka utaona Bwana Yesu anafundisha vitu vitatu tofauti vinavyopotea.
1) Kondoo: Luka 15:3-7
2) Shilingi: Luka 15:8-10
3) Mwana: Luka 15:11-32
> Kondoo anapotea kutoka kwenye kundi, na kuishi maporini, anaanza kutafutwa na mchungaji.
> Shlingi inapotea ndani ya nyumba, inaanza kutafutwa na mwanamke.
> Lakini mwana anamwacha makusudi baba yake anachagua kwenda nchi ya mbali. Anangojewa na baba yake.
Haya ni makundi matatu ya watu ndani ya nyumba ya Mungu.
Kundi la kwanza ni aina ya watu ambao hutoweka katikati ya jamii ya waaminio, ukichunguza sababu sio kwamba wamedhamiria wao kuwa hivyo, lakini udanganyifu wa dhambi, anasa za kidunia, na mafundisho ya uongo, huwapoteza,na kutokomea huko. wakati wa mwanzoni hawajijui kama wanapotea…lakini baadaye wanapojikuta katika ukame wa kiroho, katika kuharibika, kuvurugwa, ndio wanagundua kuwa njia waliyoiendea sio sahihi.
Wanaanza kutaabika huku na huko, kutafuta msaada lakini hawaupati, mpaka watakaporudi kwenye zizi lao. Sasa Hapa ni wajibu wa kanisa kuwafuatilia, watu na namna hii.
Ndio hapo Bwana Yesu anasema ……
Luka 15:4-6
[4]Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? [5]Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi. [6]Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
[4]Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
[5]Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
[6]Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
Lakini kundi la pili hufananishwa na ile shilingi iliyopotea. Kumbuka ilipotelea ndani, sio nje.
Hili ni kundi la watu ambalo haliondoki ndani ya kanisa, lakini linapotelea likuwa huko huko. Hawa ndio wapo.kwenye hatari kubwa zaidi kwasababu wanaweza wakawa wanaendelea kuwa viongozi, wazee wa kanisa, waimba kwaya lakini maisha yao yapo mbali na Kristo, ni wazinzi, walevi, washirikina.
Kama wewe ni mmojawapo, tubu haraka kwasababu kuwa katikati ya kundi haimaanishi umekubaliwa na Mungu, Yuda aliishi na Bwana Yesu miaka yote, na akafanya miujuza lakini bado alikuwa upotevuni.
Halikadhali kanisa linapowagundua watu kama hawa, ni wajibu wao kuwarejesha iadha kwa mafundisho, au maonyo, au makaripio ili wapone.
Ndio hapo Bwana Yesu akasema..
Luka 15:8-10
[8]Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? [9]Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea. [10]Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
[8]Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
[9]Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
[10]Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Lakini kundi la tatu, ni wale ambao kwa makusudi kabisa wanaamua kumwacha Mungu na kurejea ulimwenguni. Ndio mfano wa yule mwana mpotevu.
Hawa ni wale wanaosema kuanzia leo mimi sipo nanyi, habari za wokovu sitaki. Wanaamua kujiachanisha moja kwa moja na kanisa au habari za kiroho.
Hawa ni kuwaombea, Bwana awape moyo wa kuzingatia wenyewe mioyoni mwao warejee, lakini kanisa linapaswa lifahamu wanaporejea hawapaswi kuwatenga au kuwaona hawafai…kanisa halipaswi kuwa kama yule mwana mkubwa, bali linapaswa liwapokee na kuwajenga upya, kwasababu Mungu anawapokea.
Luka 15:28-32
[28]Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi. [29]Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu; [30]lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona. [31]Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako. [32]Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
[28]Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
[29]Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
[30]lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
[31]Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako.
[32]Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.
Je mahali ulipo umemwona aliyemmoja wa kundi hili?
Mfuatilie, mwonye, mwombee.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ