Shekemu alikuwa ni kijana wa mkuu wa nchi ya Wahivi. Biblia inamtaja kama kijana aliyekuwa na heshima kuliko vijana ndugu zake wote.
Lakini pamoja na heshima aliyokuwa nayo kwa wazazi, ndugu na jamii iliyomzunguka, alifanya kosa moja lililosababisha mauti, si kwake tu bali na kwa familia yake yote na Taifa kwa ujumla.
Na kosa lenyewe lilikuwa ni kufanya “Uasherati” na binti wa nyumba ya “kikuhani” ya Yakobo aliyeitwa Dina.
Na baada ya kufanya uasherati mara moja tu alijua ataendelea kuwa salama kwani binti aliyelala naye hakuwa kahaba, bali alimkuta bikra, na kwasababu ni bikira alijua kuwa huyo ndie mke wa kuoa, lakini ndoto zake hizo hazikutimia.
Mwanzo 34:1 “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi. 2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. 3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri. 4 Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu. 5 Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja. 6 Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye. 7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka. 8 Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe. 9 Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu. 10 Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo. 11 Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa. 12 Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu”…
Mwanzo 34:1 “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi.
2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.
3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri.
4 Shekemu akamwambia Hamori, babaye, akasema, Unipatie msichana huyu awe mke wangu.
5 Basi Yakobo akasikia ya kwamba amembikiri Dina, binti yake. Na wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja.
6 Akatoka Hamori, babaye Shekemu, kumwendea Yakobo, aseme naye.
7 Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka nyikani; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, neno lisilojuzu kutendeka.
8 Hamori akasema nao, akinena, Roho ya Shekemu, mwanangu, inamtamani binti yenu, tafadhalini, mpeni amwoe.
9 Mkaoane na sisi, mtupe sisi binti zenu, nanyi mkatwae binti zetu.
10 Nanyi mtakaa nasi, na nchi hii itakuwa mbele yenu; kaeni, na kufanya biashara humo, mkapate mali humo.
11 Shekemu akamwambia babaye yule msichana na nduguze, Na nikubalike machoni penu, na mtakavyoniambia nitatoa.
12 Mjapoongeza sana mahari na zawadi, nitatoa kadiri ya mtakavyoniambia, lakini mnipe huyu msichana, awe mke wangu”…
Baada ya kijana Shekemu kuomba sana kupewa binti Dina, kwa mahari nyingi na kwa kusihi sana, majibu yake yalikuna tofauti, kwani wana wa Yakobo walimwua Shekemu na baba yake pamoja na watu wote wa nchi ile na mali zao zote wakazichukua.
Mwanzo 34:26 “Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka. 27 Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao. 28 Wakachukua kondoo zao, na ng’ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni. 29 Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka”
Mwanzo 34:26 “Wakawaua Hamori, na Shekemu mwanawe, kwa makali ya upanga, wakamtwaa Dina katika nyumba ya Shekemu, wakatoka.
27 Wana wa Yakobo wakawajilia hao waliouawa, wakauteka nyara mji kwa sababu wamemharibu umbu lao.
28 Wakachukua kondoo zao, na ng’ombe zao, na punda zao, na vitu vilivyokuwamo mjini, navyo vilivyokuwako kondeni.
29 Wakatwaa na mali zao zote, na watoto wao wote, na wake zao, na vyote vilivyokuwamo nyumbani mwao wakavichukua mateka”
Huo ndio ulikuwa mwisho wa Shekemu ambaye anatajwa kuwa kijana mwenye heshima kuliko watoto wote wa mzee Hamori (Mwanzo 34:19).
Shekemu alitanguliza zinaa kabla ya ndoa, na baadae alipoitafuta ndoa kwa gharama kubwa aliiokosa na kulipwa mauti.
Yawezekena nawe ni kijana ambaye una heshima, huwenda huna rekodi yoyote ya uzinzi, wala huna sifa mbaya mtaani wala kwa wazazi, fahamu kuwa wewe ni windo kubwa la ibilisi kuliko wale ambao maisha yao yote ni zinaa,
Labda na wewe upo katika hatua kama ya Shekemu, umemwona binti tena wa imani na mwenye heshima na asiye na rekodi yoyote chafu, na moyoni unasema “nilale naye kwanza halafu nitamwoa”..kabla haujafikiria kufanya hivo mkumbuke Shekemu.
Inawezekana wewe binti unafuatiliwa na kijana mwenye heshima zake na hadhi zake, na moyoni unasema ngoja nimkubalie kwani atakuoa, Ni kweli wote mnaweza kuwa na malengo ya kuoana, hata Shekemu na Dina baada ya zinaa bado waliendelea kupendana, pasipo kujua kuwa dhambi haijui viapo mlivyoahidiana, bali yenyewe inaleta mauti iliyoumbiwa.
Leo utalala na huyo kijana lakini ndio heshima yako imeisha hapo hatuoni mahali panatajwa Dina kuolewa, zaidi imebaki kumbukumbu ya sifa mbaya ambayo mpaka sasahivi tunaisoma na itaendelea kusomwa vizazi vyote.
Na wewe aibu yako itaendelea kwa vizazi vyako vyote,
Binti jitunze, kijana jitunze..kuchochea mapenzi kabla ya wakati wake ni sawa na kuchochea moto huku umeshika galoni la mafuta ya petroli.
Wimbo Ulio Bora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe”
Zipo hatua za kufuata ikiwa unahitaji kuingia katika ndoa, wasiliana na viongozi wako wa kiroho watakufundisha hatua kwa hatua, usikurupuke na kutanguliza zinaa kabla ya ndoa.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kijana ni nani kibiblia?
KAMA WEWE NI KIJANA, BASI FAHAMU YAFUATAYO NA UCHUKUE TAHADHARI!
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
PALE WATUMISHI WANAPOSHINDWA KUTOA PEPO.
NENO NA MAOMBI~ Sehemu ya 2 (AMRI YA UPENDO)
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ