MAMBO 5 AMBAYO KILA MKRISTO ANAPASWA KUFAHAMU.

by Admin | 23 January 2020 08:46 am01

Mambo 5 ambayo kila mkristo anapaswa kufahamu.


NJIA IMESONGA.

Kuvuka ng’ambo si kurahisi kama inavyodhaniwa na wengi.

Mathayo 7:13  “Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

14  Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache”..

Hivyo usivunjike moyo, unapojikuta upo peke yako katika safari ya wokovu, kikubwa tu ni kukazana na Bwana, na kuhakikisha hurudi nyuma, kwasababu Bwana ameahidi kuwa pamoja na wewe safarini hadi mwisho.

MAJARIBU NI LAZIMA YAJE:

Yohana 16:33 “Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu”.

Usirudi nyuma unapokutana na utelezi safarini, mambo kama magonjwa, misiba, kupungukiwa, kuuudhiwa kwa ajili ya wokovu, kutukanwa, kupoteza n.k…utakutana nayo.Lakini Jipe moyo kama Bwana alivyosema..Kwasababu pamoja na hayo ameahidi kutuwekea na mlango wa kutokea, hivyo hayatadumu milele.

MAISHA NI MAFUPI.

Yakobo 4:13  “Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;

14  walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka”.

Tukilijua hilo pia basi tutautumia muda wetu vizuri kwa Bwana, kwasababu hatujui ni muda gani tuliobakiwa nao hapa duniani. Hivyo hatutaishi kwa kujisahau mpaka kupitiwa na mambo mengine tukasahau kuwa tupo ukingoni mwa safari.

HUKUMU INAKUJA.

Warumi 14:12  “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Tukijua kuwa utafika wakati ambao kila mkristo atasimama mbele ya kiti cha enzi cha Kristo na kueleza ni jinsi gani alivyoitumia talanta yake…Hiyo inatuhimiza, kila siku tuishi maisha ya kujitathimini , na vilevile kuitenda kazi yake kwa uaminifu wote na kwa bidii, ili tusiwe miongoni mwa  lile kundi la watumwa walegevu”.

UMILELE UPO.

Danieli 12:2 “Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele”.

Kuna kuishi maisha yasiyo na mwisho huko mbeleni. Fikiria unakwenda kuwa nani?  Tukilijua hilo, basi itatufanya tuwekeze kwa bidii kule ili thawabu zetu ziwe nyingi, tuwe matajiri katika ufalme wa Mungu, kwasabaabu utajiri wa kule utakuwa ni wa kudumu milele, lakini tusipowekeza chochote, mambo yatakuwa ni kinyume chake, tutakwenda kuwa watu wa kawaida milele, au tusifike kabisa…

Mimi na wewe tupige mbio tuumalize mwendo salama…

Shalom.

Mada Nyinginezo:

KWA KUWA NGUVU ZA MBINGUNI ZITATIKISIKA.

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

JE! WATOTO WACHANGA WANAWEZA KUHUKUMIWA NA KUTUPWA MOTONI.

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

NGUVU YA MSAMAHA

WALE WAZEE ISHIRINI NA WANNE (24), WANA KAZI GANI?

DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/01/23/mambo-5-ambayo-kila-mkristo-anapaswa-kufahamu/