KAMA ZILIVYOKUWA SIKU ZA NUHU NA ZA LUTU.

by Admin | 12 February 2020 08:46 pm02

Luka 17:26 “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.

28 Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;

29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.

30 Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu”.

Kuna mambo makuu manne ya kuzingatia hapo ambayo yalikuwa yanaendelea vipindi vifupi kabla ya Mungu kumwaga ghadhabu yake juu ya wanadamu wa kipindi hicho……ambayo yatajirudia tena kipindi kifupi kabla ya kurudi kwa Bwana Yesu Kristo..

Mambo hayo ndio haya… 1) KULA na KUNYA…2) KUOA na KUOLEWA …3) KUNUNUA na KUUZA…3) KUPANDA na KUJENGA

Leo tutaangalia moja baada ya lingine na kisha tutathmini wenyewe je! Tupo siku za mwisho au la?

1.KULA na KUNYWA.

Kama tunavyojua kula sio kubaya…Lakini mlo unaozungumziwa hapa ni ule wa ulafi, haramu..kama unaondelea katika nyakati hizi..watu wanakula hata vitu visivyolika wanakula madawa ya kulevya, ni n.k..na kadhalika vinywaji vinavyozungumziwa hapo sio maji…kwasababu hakuna ubaya wowote katika kunywa maji…bali unywaji unaozungumziwa hapo ni unywaji wa pombe, Unywaji wa madawa ya kuongeza kiwango cha maasi kama vile madawa yakuongeza matiti, makalio, kuuongeza ukubwa wa sehemu za siri, madawa ya kuongeza homoni za jinsia tofauti, watu wanakunywa madawa ya kujichubua na madawa ya kuongeza hisia za kufanya uasherati n.k hayo ndiyo yaliyokuwa yanaendelea hasaa katika kipindi cha Nuhu…yaliyosababisha gharika. Na sasa teknolojia tuliyonayo imekwenda Zaidi ya hapo..

Hali ilivyokuwa kipindi cha Sodoma na Gomara ilitabiriwa kujirudia tena vile vile katika siku za mwisho, karibia sana na kuja kwa pili kwa Bwana Yesu.

2) KUOA na KUOLEWA…(walikuwa wakioa na kuolewa)

Sehemu ya pili ni kuoa na kuolewa…Kumbuka hakuna ubaya wowote wa kuwepo kwa ndoa ya mume mmoja na mke mmoja…hata hivyo watakatifu Bwana Yesu akirudi na kuwakuta wapo kanisani wanafunga ndoa iliyo halali..watanyakuliwa na kwenda na Bwana..Hivyo kuoa na kuolewa Bwana Yesu alikokuwa anakuzungumzia pale ambapo kulikuwa kunaendelea katika kipindi cha Nuhu ni ndoa za kishetani.

Na ndio hizo ni kama zifuatazo…Ndoa za jinsia moja..yaani mwanamume anamwoa mwanamume mwenzake na mwanamke anamwoa mwanamke mwenzako..hizo ndizo zilikuwa zinaendelea kipindi cha Nuhu na Sodoma na Gomora…ndio maana utaona hata wakati wa sodoma na gomora wale watu wa mji walitaka kulala na wale malaika hawakujali kuwa ni wanaume..vivyo hivyo ndoa nyingine ya kishetani ambayo Bwana Yesu alikuwa anaimaanisha pale kwamba ilikuwa inaendela kipindi cha Nuhu na Sodoma si nyingine Zaidi ya Ndoa za mitara…Yaani mwanamume mmoja anaoa wake wengi mambo hayo yalifanywa na uzao wa Kaini soma (Mwanzo 4:19)…au mwanamke mmoja anaolewa na wanaume wengi jambo ambalo sasahivi limeongezeka kwa kasi kubwa sana…huwezi kosa ukoo mmoja ukakosa mtu aliyeoa mke Zaidi ya mmoja…

Halikadhalika ndoa nyingine ya kishetani Bwana Yesu aliyoimaanisha ni ndoa ya mwanadamu na mnyama..Duniani sasa katika historia tayari kuna mataifa yameshahalalisha ndoa kati ya wanadamu na wanyama…jambo ambalo ni laajabu sana…Na Zaidi ya yote ndoa hiyo inahudhuriwa na watu wengi na kuheshimiwa… Kutimiza unabii unaosema ”watakuwa wakioa na kuolewa”…

Na ndoa nyingine ya kishetani iliyokuwa inaendelea kipindi cha Nuhu na kujirudia tena katika kipindi chetu ni ndoa ya Mwaminio kuoana na mtu asiyeamini..pamoja na mabinti wadogo kufunga ndoa na watu wa makamo makubwa kutokana na tamaa za mali, na vijana kuoa wanawake wenye umri mkubwa kwa tamaa ya mali… Yote hayo ndiyo yaliyokuwa yanaendelea kipindi cha Nuhu…na yamejirudia kwa kasi tena kipindi hichi cha siku za mwisho.

3) KUNUNUA na KUUZA…(walikuwa wakiuza na kununua)

Kununua na kuuza pia sio kubaya..Hata hivyo Bwana akija na kumkuta mtu wake anauza mkate ulio halali dukani mwake atanyakuliwa hata katika hali hiyo…Hivyo kuuza na kununu Bwana alikokuwa anakuzungumzia hapo ni kwingine..

Na huko si kwingine Zaidi ya kununua na kuuza vitu visivyompendeza Mungu, kwamfano kununua mavazi yasiyompendeza Mungu..kama nguo fupi, vimini, kununua suruali kwa wanawake…kadhalika kuuza vipodozi, kuuza lipsticks, wanja, rasta, kuuza hereni, kuuza sigara, pombe, na vitu vyote visivyofaa…Leo hii jaribu kwenda sokoni uone ni vitu vingapi vya kukosesha vinavyouzwa…utahuzunika sana…katiza kona mbili kama hutaona pombe au sigara zinauzwa, Tunaishi katika siku za mwisho..wengi hawalijui hilo kwasababu wanadhani kununua na kuuza kunakozungumziwa pale ni peremende na siagi tu..

Tumefikia hatua ambayo ukihitaji chochote kile katika hii dunia unaweza kukinunua kwa fedha. Hata watu siku hizi wanajiuza wenyewe ili kupata fedha, kama hujui fanya tathimini ya madanguro yanayokuzunguka hutaamini mambo yanayoendelea kwa siri….na wako pia wanaouza viungo vyao ili kupata fedha…wako wanaouza mpaka figo..na wengine wanauza mpaka uchawi..na wapo wanaoununua.n.k.. Na msingi huo wa kuuza na kununua ndio utakaokwenda mpaka kipindi cha dhiki kuu ambapo mpinga-kristo ataona idadi ya mauzo na manunuzi inaongezeka kwa kasi hivyo itahitajika chapa kiasi kwamba hakuna mtu atakayeweza kununua wala kuuza bila kuwa nayo.

3) KUPANDA na KUJENGA….(walikuwa wakipanda na kujenga)

Kupanda na kujenga sio vibaya…hata hivyo mkristo aliyesimama katika Imani kamilifu ya utakatifu..akiwa shambani kwake anapanda mbegu zake za mahindi atanyakuliwa tu..hata hivyo Bwana alisema siku ile wawili watakuwa shambani mmoja atatwaliwa mwingine ataachwa (Mathayo 24:40)…hivyo kupanda Kristo alikokuzungumzia kulikokuwa kunaendelea kipindi cha Nuhu ni pamoja na kupanda vitu visivyofaa (kama ilivyokuwa siku za Nuhu ndivyo itakavyokuwa siku za mwisho)…mashamba ya bangi katika mataifa mengine ni kama mboga, na hata katika mataifa kama haya yetu vilimo hivyo vinaendelea..kadhalika kujenga kunakozungumziwa sio kujenga nyumba…Ndio kupoteza muda mwingi kujenga na kumsahau Mungu kuna madhara makubwa sana lakini pia kupoteza muda kujenga Bar, kujenga kumbi za disko, kujenga casino, kujenga jengo la massage, kujenga danguro, kujenga nyumba za wazinzi na kuziita nyumba za kulala wageni, kujenga kiwanda cha pombe, na sigara n.k Ujenzi huo ndio uliokuwa unaendelea wakati wa kipindi cha Nuhu na Lutu.

Vivyo hivyo kujenga nyumba ya kuishi na kuizindika.., kujenga nyumba na kutoifanya kuwa nyumba ya sala bali kama pango la wasioamini huo pia ndio ujenzi uliokuwa unaendelea wakati wa Nuhu na Sodoma na Gomora uliosababisha ghadhabu ya Mungu kumwagwa..

Ndugu yangu yakumbuke tena maneno haya Bwana Yesu aliyoyasema… “Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu”. Upewe uthibitisho gani tena kwamba tunaishi katika siku za Mwisho ndipo uamini?..

Uthibitisho ni kuwa hayo mambo miaka ya hapo kati yalikuwa hayafanyiki sana..lakini katika nyakati hizi tunaozishi, ni jambo la kawaida sana..

Bwana atusaidie sana.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mafundisho mengine:


Mada Nyinginezo:

MTINI, WENYE MAJANI.

MAONO YA NABII AMOSI.

Je! Ni sahihi kuoa/kuolewa na mtu uliyemzidi umri?

MIHURI SABA

Naomba kujua watakaoenda mbinguni je! ni wengi au wachache?

HATUTAACHA KUJIFUNZA NENO KILA INAPOITWA LEO.

USIMPE NGUVU SHETANI.

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/12/kama-zilivyokuwa-siku-za-nuhu-na-za-lutu/