MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?

by Admin | 13 January 2021 08:46 pm01

Nakusalimu katika jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujikumbushe mambo ya msingi ambayo bila shaka moja ya hizi siku tutayaona yakitokea ulimwenguni. 

Kwa kawaida ulimwengu umeundwa na makundi mengi ya watu, na kila kundi ni lazima utakuta kuna mtu Fulani linamtazamia, ambaye wanaamini ataulimwengu umeundwa na makundi mengi ya watu, na kila kundi ni lazima utakuta kuna mtu Fulani linamtazamia, ambaye wanaamini atakuwa aidha mkombozi wao wa kudumu au atakakuwa aidha mkombozi wao wa kudumu au atakayewaletea suluhisho la maisha yao kwa ujumla. Kwamfano Wanasayansi, kila siku wanatafiti, usiku na mchana, wakitumai siku moja watakutana na viumbe vinavyotoka sayari nyingine(Aliens), ambavyo wanaamini vitakuwa na uwezo mkubwa sana wa kiteknolojia, hivyo siku watakapokutana navyo, na kuisoma sayansi yao basi matatizo mengi sana ya kijamii yaliyoshindikana yatatatuliwa. Hata pengine ikiwemo kifo au kuzeeka.

Vivyo hivyo, wanajamii,au wanasiasi nao hawapo tu hivi hivi, nao pia wanatazamia, atatokea kiongozi mmoja atakayeleta suluhu ya shida za watu, atakayeweza kuleta maendeleo ambayo yataigueza dunia na kuifanya kuwa sehemu ya amani, yenye furaha, na isiyokuwa na shida. Na ndio maana kila wanapomchagua kiongozi Fulani mpya, katika nchi wanampa muda ili waone kama ataweza kufanya hivyo, akishindwa watamtoa na kuleta mwingine, hivyo hivyo wataendelea mpaka wampate wanayemtafuta, lakini mpaka sasa bado hawajampata na ndio maana wanaendelea kuchagua na kurithisha, Jambo hilo lilikuwepo tangu zamani sana, na bado litaendelea kufanyika mpaka siku za mwisho.

Hali kadhalika  na watu  wa dini zote ulimwenguni, ikiwemo sisi wakristo kila dini  inayo matarajio ya mtu fulani huko mbeleni atakayekuwa suluhisho la matatizo yao ya mwilini na rohoni, moja kwa moja. 

Hivyo kiu hii  ya kutafuta mtu fulani, au kitu fulani cha kuwatatulia matatizo yao, ni kiu ya asili ambayo Mungu aliiweka ndani ya mioyo wa mwanadamu Ili kusudi kwamba wamtafute yule ambaye anapaswa kutafutwa.

Ni pengo ambalo mwanadamu amejikuta analo tu ndani ya moyo wake maadamu anaishi duniani, na ndio maana kila siku anatafuta kwa bidii ni kwa namna gani ataweza kulijaza.

Hivyo kufanya habari kuwa fupi ni kuwa mtu sahihi ambaye alikuwa ameandaliwa kwa ajili yao hakuwa  mwingine zaidi ya YESU KRISTO, huyu ndio jibu na suluhu ya tatizo na shida yoyote ya kiroho au ya kimwili, na huyu ndio wangepaswa wamtazamie, arudi kuja kuwakomboa na mateso ya ulimwenguni.

Sasa hakuna asiyejua kuwa hizi ni nyakati za majeruhi, kwamba Yesu yupo mlangoni kurudi kuleta suluhisho la matatizo yote ya ulimwenguni, lakini biblia inatuonyesha kabla kiongozi wa kweli hajarudi atatangulia kwanza yule wa uongo, na kwasababu watu hawapendi kuungozwa na Mungu, na huku  ndani ya mioyo yao wana kiu ya kuongozwa, mtu huyu atakapokuja itakuwa ni rahisi sana dunia  nzima kutekwa na yeye kwasababu atajifanya yeye kuwa kama Yesu,..Ndio maana Bwana Yesu alituonya akasema wakati wa mwisho watakuja  wengi kwa jina lake wakisema wao ndio.. hivyo tusiwasikilize,

Ndivyo itakavyokuwa kwa kiongozi huyu atakuwa mashuhuri na amebobea katika Nyanja zote, atakuwa ni mwanasiasi, pia atakuwa ni mtu wa dini kweli kweli, ataushawishi ulimwengu kuwa ataleta Amani waliyokuwa wanaitafuta kwa muda mrefu, ataleta suluhu ya matatizo yao yote, na kwa jinsi atakavyokuwa na ushawishi mkubwa biblia inasema wale watu ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha mwanakondoo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu watamwamini.

Ufunuo 13; 8 “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”.

Hata iweje, ikiwa wewe wakati huo utakuwepo ulimwenguni, utamwamini tu, kama sio katika upande wa kisiasa, basi utamwamini tu katika upande wa kiimani/dini, kwasababu, mtu huyo atakuwa pia na uwezo mkubwa wa kufanya ishara kubwa na maajabu yasiyo ya kawaida., 

2Wathesalonike 2: 9 “yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo”;

Shetani anajua watu wanapenda ishara na hivyo atajaliwa kuzifanya tu, tena za wazi kwa wazi kwenye TV, watu wote wataziona, Kama vile alivyozifanya kipindi kile wazi wazi mbele ya farao pale Musa alipokwenda kuonyesha maajabu ya Mungu kwake, , watu watamwabudu kama Vile Mungu. Vilevile atakuwa  Ni mtu ambaye atakuwa anaingia maagano mengi ya amani na watu wengi (Danieli 9:27) ….

Mtu huyo ndiye Mpinga Kristo, au kwa jina lingine asi, au mwana wa uharibifu..  kwa ufupi ni kuwa dunia nzima itamwelekea, na matokeo yake ni kuwa atafanikiwa kugeuza mfumo mzima wa dunia unavyokwenda, na wakati huo huo ndipo atakapoianzisha ile chapa ya mnyama kiasi kwamba hakuna mtu atakayeweza kununua au kuuza bila kuwa  chapa hiyo, ikiwa na maana hata kuajiriwa.

Mpaka hapo Wanasayansi,watakapoliona hilo watakuwa wameshapata majibu yao, wananchi nao pia watakuwa  wameshapata  majibu yao, na viongozi wote vipofu wa dini watakuwa wameshampata masihi wao.

Wakati huo ukifika na kama wewe upo bado hapa duniani, ujue kuwa Dunia hii haitakuwa na zaidi ya miaka saba mpaka iishe. Kwasababu atapewa kutenda kazi yake ya kuua na kuchinja watu wote wasioipokea ile chapa yake kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Dhiki itakayokuwepo huko, biblia inasema haijawahi kutokea na wala haijatakaa itokee baada ya hapo. Kiasi kwamba mpaka mtu utoboe ,na  hajashiriki kupokea chapa yake kwa namna yoyote ile, uwezekano wake ni sawa na asilimia sifuri. Ni jambo lisilowezekana kabisa.

Lakini mwishoni kabisa watu watakuja kugundua mbona hajaleta badiliko katika dunia, lakini hiyo itakuwa wameshachelewa, kwasababu mtu pekee ambaye anayeweza kuigeuza hii dunia na kuwa Paradiso ya Mungu ni MFALME YESU KRISTO PEKE YAKE.

Wakati huo ndipo Mungu ataanza kuiadhibu dunia kwa mpigo makali  ya vitasa saba  Ufu 16, ndipo watakapojua kuwa Kristo wa kweli  anakuja. Hapo ndipo watakapojipanga wapigane na Kristo katika vita ile ya Har magedoni..lakini watauliwa wote ndani ya muda mfupi sana.

Mambo hayo hayana muda mrefu kuanza kutokea, kwasababu kama siri ya kuasi imeshaanza kutenda kazi unategemea vipi, tutakuwa na muda mrefu sana hapa duniani? Kila ishara ya siku za mwisho iliyozungumziwa kwenye biblia imeshatimia, tunachongojea hapa ni UNYAKUO tu, ambao hatujui ni lini, unaweza ukawa ni leo usiku, au kesho asubuhi, na ukishapita huo ndipo huyu mpinga Kristo ataanza kufanya kazi zake. Swali ni je! Upo ndani ya Kristo?. Je akirudi leo usiku unao uhakika wa kwenda kumlaki mawinguni? Kama huna uhakika fahamu kuwa dhiki kuu au ziwa la moto linakungoja, Na sijui utamjibu nini Yesu siku ile ya hukumu, kwa kusikia maneno yote hayo lakini  hukutaka kuokoka.

Tubu mrudie muumba wako, hizi sio nyakati za kubembelezana tena.. Huu ni ule wakati wa NURU YA JIONI.

Maran Atha

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UTAWALA WA MIAKA 1000.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.

Maherodi walikuwa ni akina nani, Na kazi yao ilikuwa ni ipi?

INJILI YA MANENO LAINI ITAKUGHARIMU.

Rudi nyumbani

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2021/01/13/matarajio-ya-kila-mwanadamu-duniani-ni-yapi/