SWALI: Kwanini Anasi na Kayafa walihudumu pamoja? Je Mungu aliruhusu makuhani wakuu wawili kuhudumu kwa wakati mmoja?
Luka 3:2
[2]wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, neno la Mungu lilimfikia Yohana, mwana wa Zakaria, jangwani.
JIBU: Ni kweli kipindi cha Bwana Yesu tunaonyeshwa makuhani wawili walihudumu katika nafasi ya ukuhani mkuu. Jambo ambalo ni kinyume na agizo la Bwana kuhusu nafasi hiyo..Kwani kuhani mkuu alipaswa awe mmoja tu, mpaka atakapokufa ndio asimamishwe mwingine..Lakini kwanini ilikuwa vile.
Uhalisia ni kuwa Ukuhani ulikuwa kwanza kwa Anasi, lakini kwasababu za kisiasa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na dola ya Warumi wakati ule.. walimteua ndugu yake ( yaaani mkwe wake) ambaye ni Kayafa asimame kwa awamu nyingine…
Ni kwanini iwe vile..
Kwa warumi nafasi za kikuhani zilikuwa ni moja ya nafasi nyeti, zenye nguvu kubwa ambazo zisipodhibitiwa walihisi uasi unaweza kutokea, na kuhatarisha ufalme, hivyo kupungumza nguvu zao hawakuwa wanawaacha makuhani wamalize muhula wao wote, mpaka kifo.kwasababu sheria ya kikuhani ilikuwa kifo ndio mwisho wa ukuhani, hivyo wenyewe waliwastaafisha makuhani…
Ndicho kilichotokea kwa Anasi, alikatizwa ukuhani wake na warumi akapewa mkwewe Kayafa. Jambo ambalo ni kosa kwa agizo la Mungu.
Yohana 18:13
[13]Wakamchukua kwa Anasi kwanza; maana alikuwa mkwewe Kayafa, yule aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule.
Japo kwa wayahudi waliendelea kumheshimu Anasi zaidi ya Kayafa kama ni kuhani sahihi kwa Bwana…lakini Kayafa pia walimpokea maana ndiye aliyekuwa anaendesha shughuli zote za kikuhani.
Ndio maana hata wakati Bwana Yesu anakamatwa, wayahudi walimpeleka kwanza kwa Anasi kabla ya Kayafa. Hiyo kuonyesha walimtambua Anasa hata baada ya kuondolewa ukuhani
Hivyo wote waliheshimika ndio maana wanatajwa kama makuhani.
Ni nini tunafunzwa katika habari zao?
Mkanganyiko.
Si ajabu kwanini nyakati zile mifumo ya kidini haikuweza kumtambua Kristo ijapokuwa alijidhihirisha kwao kwa namna zote..
Wayahudi walivunjika vunjia kwanza kiiamani licha ya kuwepo makuhani wawili…walikuwepo pia mafarisayo na waandishi.. na madhehebu mengine kadha wa kadha.
Mfano tu wasasa uwepo wa madhehebu mengi..ikidhaniwa kuwa Mungu yupo huko.
Leo hii kila mtu ana lake..Lakini je Kristo ni hayo?
Embu tuwazie kwa wakati ule…
Kuhani mkuu halisi (Yesu Kristo), alikuwa akizunguka huku na huko akiwahubiria maskini wa roho habari njema, akiwafanya huru waliosetwa na shetani, akiwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao (Luka 4), sio kuunda dini, au dhehebu au taasisi, fulani, Sio mashindano, n.k.
Sio kwamba taasisi Haziifai, zinafaa sana lakini je, Kazi za msingi za Kristo zinapewa kipaumbele?
Makuhani wakuu wa tatu waliokuwepo.. Kati ya hao Kristo ndiye aliyekubaliwa, hivyo mfuate yeye.
Amen
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ