Huu ni mfululizo wa masomo yawahusuyo watumishi wa Mungu.
Kuna makosa mengi yapo miongoni mwa mitazamo yetu sisi (watumishi wa Mungu), tunadhani mafanikio ni pale hasaa huduma yetu inaposhawishi mioyo ya wengi …pale tunapoona umati unaipokea, na kuishangilia.
Lakini tukifuatilia huduma za manabii wengi wa Mungu, kwenye biblia kama vile Isaya na Ezekieli, Yeremia hawakuwa na mafanikio makubwa ya mahubiri yao, kama tunavyodhani hivi leo, kinyume chake waliishia kukataliwa, kuteswa na kuuliwa, kwa ufupi huduma zao ziliwavunja sana moyo, lakini kwasababu aliyewatuma ni Bwana, injili yao imesimama vizazi na vizazi mpaka leo..
Walijua wanakwenda kuhubiri kwa watu ambao wana mioyo migumu sana…na Mungu aliwaeleza kabisa, lakini walifanya hivyo kwa uaminifu wote, kana kwamba wanauokoa umati wa watu.
Yeremia 7:27
[27]Nawe utawaambia maneno hayo yote; lakini hawatakusikiliza, nawe utawaita; lakini hawatakuitikia.
Ezekieli 2:3-7
[3]Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo. [4]Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. [5]Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao. [6]Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma i pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi. [7]Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.
[3]Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wamekosa juu yangu, naam, hata hivi leo.
[4]Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi.
[5]Nao, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao.
[6]Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma i pamoja nawe, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
[7]Nawe utawaambia maneno yangu, kwamba watasikia, au kwamba hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.
Hakuna jambo linaloumiza kwa mtumishi wa Mungu pale unapoona unahubiria jamii kubwa ya watu lakini matokeo yoyote huoni kwao,…Ni vema ufahamu kuwa Mungu hakutumi ukawe mshawishi, anakutuma ukawe mwaminifu kwa kazi yake.
Kushindwa kwako katika huduma sio, kukosa watu wa kukusikiliza au watu kupungua kwenye huduma yako, kushindwa kwako ni kukosa uaminifu..hilo tu.
Leo hii ungewekwa kwenye nafasi ya Nuhu ambaye aliuhubiria ulimwengu kwa miaka mia moja na ishirini, na kuambulia tu familia yake, ungeshamkimbia Mungu siku nyingi na kusema sijatumwa, ungewekwa kwenye nafasi ya Yeremia, Mika, sefania ungesema huyu si Mungu, ni akili zangu zimenituma, ungesema ninachofanya ni uwendawazimu…hii sio huduma lazima kuna shida mahali, haiwezekani watu hawataki kugeuka, na kutubu, ungewekwa nafasi ya Musa ungesema hawa nilionao sio watu wa Mungu ni kizazi cha nyoka, pamoja na ishara zote na miujiza…lakini bado wanatengeneza ndama wa shaba, wanaasi, wananung’unika…najitaabisha bure tu.
Kama mtumishi wa Mungu jitahidi sana kuwa mwaminifu, hata kama huoni ukuaji wowote, au mafanikio yoyote ya machoni, ya kuokoka kwa watu wengi…wewe ifanye kazi yake, mtumikie yeye, timiza ratiba zako. mtumikie Mungu kwa mtazamo huo wa uaminifu na sio wa matokeo, utadumu na hutapindishwa na chochote.
Kwani thawabu yako ni kubwa mbinguni.
Mungu akubariki sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
MHESHIMU MCHUNGAJI WAKO.
SIKU ZA WATUMISHI WA MUNGU.
KARAMA TUZIPATAZO KWA MSAADA WA WATU WENGI.
Print this post
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ