Shalom, jina la Mwokozi YESU libarikiwe, karibu tujifunze pamoja Biblia, Neno la Mungu wetu.
Maandiko yanatabiri kuwa siku za mwisho kutatokea aina ya watu wasiotaka “suluhu” katika nyanja mbalimbali za kifamilia hata kikanisa.
2 Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3 wasiowapenda wa kwao, WASIOTAKA KUFANYA SULUHU, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema”.
2 Timotheo 3:1 “Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
3 wasiowapenda wa kwao, WASIOTAKA KUFANYA SULUHU, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema”.
Tabia ya kutotaka kufanya Suluhu imwsababisha ndoa nyingi kuvunjika, familia nyingi kutengana, makanisa kuanguka , undugu kuisha, na hata urafiki mwema kuisha..
Jambo ambalo si jema machoni pa MUNGU wetu.
Lakini pamoja na hayo yote, yawezekana zimetumika njia nyingi kuleta suluhu na mapatano imeshindikana..
Yawezekana mazungumzo na vikao vimefanyika vya kutosha lakini hakuna suluhu, yawezekana umejaribu au mmejaribu kuweka mambo sawa kwa kila njia lakini bado hakuna mapatano wala makubaliano.
Kama njia zote hizo hazijaleta matokeo basi ipo kanuni moja ya kibiblia nzuri sana ambayo mtu akisimama na hiyo vizuri basi hata wale maadui zake atapatana nao.
Na njia hiyo si nyingine zaidi ya ile tunayoisoma katika Mithali 16:7.
Mithali 16:7 “Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye”.
Ikiwa na maana kwamba Mtu akizitengeneza njia zake zikawa thabiti kwa MUNGU, na hata MUNGU akapendezwa naye, basi hatawale waliokuwa wanampiga vita, Mungu ataweka amani, hata wale waliokuwa wanamchukia Mungu ataweka upendo.
Lakini ni lazima njia za Mtu kwanza zimpendeze MUNGU,
Labda tujifunze mfano mmoja wa kwenye Biblia tuweze kuelewa zaidi, tumrejee Yakobo ndugu yake Esau,
Tunaona baada ya Yakobo kuchukua mbaraka wa ndugu yake, mara moja Esau aliapa kumuua, jambo lililomfanya Yakobo akimbie.
Lakini pamoja na kukimbia kwake Yakobo alijua fika kuwa hataweza kumkimbia ndugu yake milele, na hivyo alitamani mapatano naye.
Sasa Yakobk alichokifanya sio kuandika barua nyingi za kuomba msamaha kwa Esau, bali katika mazingira ya kujitenga alitengeneza njia zake kwa MUNGU, katika ukamilifu na usafi, na wala hakuketi kumsema kaka yake, na MUNGU akapendezwa naye na kumpatanisba na ndugu yake Esau ambaye aliapa kumuua hapo kwanza.
Mwanzo 33:1 “Yakobo akainua macho yake, akaona, na tazama, Esau anakuja na watu mia nne pamoja naye. Akawagawanyia Lea, na Raheli, na wale vijakazi wawili, wana wao…… 3 Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake. 4 Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia. 5 Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake. 6 Ndipo wale vijakazi, na wana wao, wakakaribia wakainama. 7Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama. 8 Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu. 9 Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, uliyo nayo na yawe yako. 10 Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami. 11 Pokea, tafadhali, mbaraka wangu, ulioletewa, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote Akamshurutisha, naye akapokea. 12 Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia”.
Mwanzo 33:1 “Yakobo akainua macho yake, akaona, na tazama, Esau anakuja na watu mia nne pamoja naye. Akawagawanyia Lea, na Raheli, na wale vijakazi wawili, wana wao……
3 Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake.
4 Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia.
5 Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake.
6 Ndipo wale vijakazi, na wana wao, wakakaribia wakainama.
7Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama.
8 Akasema, Kundi hili lote nililolikuta, maana yake ni nini? Akasema, Kunipatia kibali machoni pa bwana wangu.
9 Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, uliyo nayo na yawe yako.
10 Yakobo akasema, Sivyo; kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, iwapo nimeona uso wako kama kuona uso wa Mungu, ukapendezwa nami.
11 Pokea, tafadhali, mbaraka wangu, ulioletewa, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote Akamshurutisha, naye akapokea.
12 Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia”.
Unaona hiyo kanuni?.. Kama njia za Yakobo zingekuwa mbovu nyumbani kwa Labani, hakika wakati huu wa kukuata na Esau ageuawa.
Yawezekana nawe ndoa yako haijakaa sawa na mke wako au mume wako. Usikimbilie manung’uniko na malalamiko na kusema umbea huku na kule, wala usitafute kujitetea sa a au kujionesha kuwa wewe ni mwenye haki.
Unaweza kujitenga kwa muda (si vibaya kujitenga kwa amani).. lakini ukiwa katika kujitenga ombi lako kuu liwe ni Kupata suluhu jema na patano zuri, huku ukizitengeneza njia zako lwa MUNGU.
Nakuhakikishia kukingana na Biblia kama njia zako zitampendeza Bwana, basi tegemea matokeo ya ajabu katika eneo hilo la mapatano au suluhu, utaona yule mume ambaye alikuwa anakusumbua sasa anatulia, yule mke rafiki, yule ndugu anakupenda na kuifuata imani yako.
Sasa Swali unatengenezaje njia yako kwa Bwana?. Si kwa njia nyingine bali kutii Neno la MUNGU.
Zaburi 119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”
Neno la MUNGU kwanza linasema tutubu, na kuimini injili (Marko 1:15). Na pia kubatizwa kwa maji na kwa Roho mtakatifu (Marko 16:16), na kuishi maisha ya utakatifu baada ya hapo (Waebrania 12:14).
Kwa kulitii hilo Neno basi mlango wa mapatano kwatu umefunguka?.
Je umempa Bwana YESU maisha yako?
Kama bado unasubiri nini?. Tubu leo na kuiamini injili.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengine:
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ