Hauhitaji nafasi kubwa kuzijua siri za Mungu.
Naamani alikuwa ni mtu mkuu, jemedari wa vita, lakini alikaa na ukoma uliomtesa kwa muda mrefu, bila ufumbuzi wowote wala tumaini lolote la kupona.
Katika ushujaa wake, na cheo chake hakuwahi kujua siri za uponyaji zipo wapi, isipokuwa kijakazi wake ambaye hajatajwa hata jina lake, aliuona uzima wa Bwana wake, mahali ulipo, mbali sana na taifa lake, kwa mtu wa Mungu aliyeitwa Elisha.
Kijakazi huyu ndiye aliyefungua njia ya Naamani kupokea uponyaji wake mkamilifu
2 Wafalme 5:1-4
[1]Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. [2]Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. [3]Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. [4]Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
[1]Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
[2]Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani.
[3]Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.
[4]Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi.
Huhitaji kuwa mtu fulani, wala huhitaji kuwa hodari duniani, kuwa msomi sana, jasiri sana, kuzidhihirisha nguvu za Mungu, au kuwahudumia watu wake, au kuwaponya na kuwafundisha, unahitaji tu, unyenyekevu ambao unadhihirishwa kwa kumcha Bwana. Kisha yeye mwenyewe Mungu kwa hekima yake ataitengeneza njia yake anayoijua mwenyewe kuwasaidia wengine kupitia wewe.
Ndio maana Neno la Mungu linasema;
1 Wakorintho 1:26-29
[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; [27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; [28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; [29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
[26]Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa;
[27]bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
[28]tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
[29]mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
Wekeza zaidi kwenye kumcha Mungu, zaidi ya juhudi za kibinadamu kwasababu hekima yake ni mbali sana na mavumbuzi ya wanadamu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ