JINSI LUGHA MPYA NA USEMI MPYA UNAVYOANGUSHA MINARA.

JINSI LUGHA MPYA NA USEMI MPYA UNAVYOANGUSHA MINARA.

Jina la Mwokozi wetu YESU KRISTO, libarikiwe, Karibu tujifunze Neno la MUNGU wetu lililo taa na Mwanga wa Njia zetu (Zab. 119:105)

Ipo Minara inayoinuliwa na ibilisi katika maisha ambayo inaweza kuangushwa/kuharibiwa kwa LUGHA na USEMI tu, maana yake pale lugha inapobadilika au usemi unapobadilika minara hiyo inakufa au kupotea.

Mfano wa minara hiyo ni ule wa Babeli..

Mwanzo 11:1 “Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.

2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.

3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.

4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.

5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.

6 BWANA AKASEMA, TAZAMA, WATU HAWA NI TAIFA MOJA, NA LUGHA YAO NI MOJA; NA HAYA NDIYO WANAYOANZA KUYAFANYA, WALA SASA HAWATAZUILIWA NENO WANALOKUSUDIA KULIFANYA.

7 HAYA, NA TUSHUKE HUKO, TUWACHAFULIE USEMI WAO ILI WASISIKILIZANE MANENO WAO KWA WAO.

8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.

9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote”.

Umeona lugha jinsi ilivyo na nguvu?.. Ni hivo hivyo katika ulimwengu wa roho ipo minara ya dhambi, magonjwa, na matatizo ya kila aina, ambayo ili iweze kuharibika inahitajika badiliko la Lugha.

Kauli zinazotoka kinywani mwako zinaweza kuangusha minara ya maadui, hivyo ukiweza kubadilisha lugha yako na kuwa ya staha, heshima, na hekima isiyo ya kejeli, dharau au matukano utaweza kumpiga ibilisi pakubwa sana, na kuangusha minara yako yote ya fitna, shida, adha na aibu.

Lakini pia tunapokuwa katika maombi, kunena kwa lugha kuna maana sana kwa mwamini, kwani tunaponena kwa lugha ibilisi hajui ni nini tunaomba kwani muda huo Roho Mtakatifu ndiye anayetuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, hivyo adui hajui ni wapi mashambulizi yatamjia, na minara yake yote inaanguka.

Ndio maana ile siku ya Pentekoste Roho Mtakatifu aliwashukia mitume, na kuanza kunena kwa lugha mpya, adui alichanganyikiwa na kushindwa kujua ni nini kinaendelea, na pale pale Mitume walipata nafasi ya kuhubiri kwa ujasiri na watu elfu tatu wakaongezeka kwa Bwana na kubatizwa.

Matendo 2:41 “Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.

43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume”.

Omba kubadilishwa lugha yako na usemi wako, omba kujazwa Ujazo wa Roho Mtakatifu unene kwa lugha (1Wakorintho 14:5), na minara yote ya adui itatoa moshi.

Yoeli 2:28 “Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

30 Nami nitaonyesha mambo ya ajabu katika mbingu na katika dunia, damu, na moto, NA MINARA YA MOSHI”.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

ZIDI KUTAFUTA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.

FUNGUA KINYWA CHA ROHO MTAKATIFU KIHUDUMU.

ONGEZA NGUVU ZAKO ZA ROHONI.

MUNGU HAJARIBIWI NA MAOVU BALI MEMA.

Je ni kweli Bwana YESU hajui siku ya kuja kwake? (Mathayo 24:36)

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply