by Admin | 17 February 2020 08:46 pm02
Kifo ni nini?, Je ni kweli kila nafsi itaonja mauti?.
Kifo sio mtu, wala si kitu bali ni “hali”…Kitu kinapopitia hali ya kukosa “UHAI”. Tayari kitu hicho kinakuwa kimekufa.
Kwamfano tuchukue kifaa kinachoitwa SIMU. Simu ikikosa chaji simu ile inazima hivyo tunaweza kusema “imekufa chaji”..Sasa kitendo cha umeme kukosekana kwenye ile simu…Ni sawa na simu ile imekufa..kwasababu haiwezi kuwaka, spika zake haziwezi kufanya kazi, kadhalika haiwezi kutoa mlio wowote wala kufanya chochote mpaka ichajiwe tena.
Vivyo hivyo Uhai wa Mungu ni kama “UMEME” ndani mwetu…Huo unapokosekana au unapotoka ndani ya mwili wa mtu…Mtu yule anakuwa amekufa. Hawezi kunyanyuka, hawezi kuona kupitia macho..hawezi kuhisi, hawezi kujibu, hawezi kufanya chochote kile..Mwili wake unakuwa umekufa.(Hivyo kifo ni nini?..Ni hali ya uhai wa Mungu kutoka ndani ya kiumbe hai)
Lakini kitu cha kipekee na cha muhimu kufahamu ni kwamba..Mtu kaumbwa na sehemu mbili kuu, nazo ni UTU WA NDANI, na UTU WA NJE. Utu wa nje ndio mwili ambao ndio huu wenye vidole, macho ni mikono…Huu uhai wa kiMungu unapoondoka unazima!.
Kadhalika kuna utu wa ndani..Huu wa nje unapozima wa ndani bado upo..unakuwa bado una uhai wa Mungu. Hivyo unaendelea kuishi..Unaendelea kuona, kusikia, kufahamu ingawa hautumii macho ya damu na nyama wala viungo vya damu na nyama…Unatumia viungo vya rohoni kuona, kusikia, kuelewa n.k
Kama mtu alikufa akiwa ndani ya Imani ya Mwana wa Mungu Yesu Kristo, analo tumaini la kufufuliwa na kuvalishwa mwili mpya wa utukufu na kwenda mbinguni kwa Bwana…ambao huo haufi wala hauzeeki. Lakini kama mtu alikufa katika ndambi anakuwa hana tumaini hilo zaidi ya kungojea kwenda kutupwa katika Ziwa la Moto.
Je ni kweli kila nafsi itaonja mauti?
Jibu ni hapana! sio kila nafsi itaonja mauti…kwani mpaka sasa kuna ambao hawajaonja mauti na wameshavuka kutoka mautini kuingia uzimani…Mfano wa watu hao ni HENOKO na ELIYA. Hawa walinyakuliwa juu bila kuonja mauti..Hivyo ni uongo kusema kwamba kila nafsi itaonja mauti.
Vivyo hivyo biblia inasema siku ya Unyakuo wa kanisa itakapofika, wapo watakatifu ambao siku hiyo itawakuta wakiwa hai. Hao Biblia imesema watanyakuliwa wakiwa hai ambapo kufumba na kufumbua miili yao itabadilishwa na kuwa kama ya Malaika, na wataungana na watakatifu waliofufuliwa na kwa pamoja watakwenda kumlaki Bwana mawinguni.
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
Na pia jambo hilo biblia imeliweka vizuri katika mstari ufuatao..
1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele”.
Hivyo wapo ambao hawataonja mauti kabisa…Na dalili zote zinaonyesha kwamba unyakuo unaweza kutokea katika kizazi chetu hichi kwasababu kila dalili zimeshaonekana na hata zimezidi na kuonekana vitu vingine ambavyo ni zaidi ya zile dalili…maana yake ni kwamba kuna uwezekano wa kulishuhudia tukio la unyakuo kwa macho yetu..
Je umejiandaa?..Utakuwa miongoni mwa watakaonyakuliwa?..kumbuka biblia inasema waasherati, wazinzi, waabudu sanamu, walevi, na wanaoupenda ulimwengu kuliko kumpenda Mungu hawataurithi uzima wa milele.
Bwana atusaidie sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/17/kifo-ni-nini/
Copyright ©2024 unless otherwise noted.