Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?

by Admin | 25 May 2020 08:46 pm05

SWALI: Je ni sahihi kualikwa kwenye karamu za watu wasio wakristo (mfano waislamu kwenye sikukuu zao za eid au futari) na kula nao ni dhambi?


JIBU: Swali hili jibu lake lipo katika kitabu cha 1Wakorintho 8, Mtume Paulo kwa uweza wa Roho alifafanua jambo hili, akasema chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu (Maana yake hakitusogezi mbele za Mungu)..tukila hatuonekani watakatifu mbele za Mungu na wala tusipokula hatujipunguzii kitu kutoka kwa Mungu…(1Wakorintho 8:8).

Tunajua Mungu ni mmoja na ndiye aliyeumba vitu vyote, Naye ni Yehova, sababu hiyo basi hakuna mchele wowote ulioumbwa na shetani, wala muhogo ulioumbwa na mungu fulani mwenye jina fulani aliyeko Asia, wala hakuna pilipili iliyoumbwa na mungu fulani aliyopo mashariki ya kati tofauti na Yehova, n.k. vyote hivyo vinatoka kwake.

Hiyo ikiwa na maana kwamba chakula chochote kilichopikwa kwa mimea au viungo vyovyote vinavyopatikana katika dunia tunayoiishi vimetengenezwa na Mungu mmoja na ni halali kuliwa. Ukipita njiani na kukuta mpera na una njaa usiogope kula! Hakuna chochote kitakachokupata, ukitumiwa zawadi ya chakula fulani na baada ya kumshukuru Mungu kile kwa Imani, utakuwa hujafanya kosa lolote mbele za Mungu.

Ukifika mahali umekaribishwa chakula usianze kuuliza uliza kimetoka wapi, au kimepitia wapi au kimetengenezwa na nini…wewe baada ya kumshukuru Mungu kula!, lakini wenyewe wakikwambia chakula hichi ni wakfu kwaajili ya miungu yetu hapo usile kwasababu ukila utawafanya na wao waamini kwamba miungu yao ipo sawa…na kama kuna mkristo aliyemchanga kiroho karibu yako akikuona umekula chakula hicho atashawishika kuamini kwamba ni sahihi kuabudu hiyo miungu na hivyo utamsababisha aanguke kitu ambacho hakimpendezi Mungu mtu yoyote apotee..Kwahiyo kwaajili ya dhamira za hao watu ili wasitie muhuri ibada hizo, hapo tu ndio biblia imetukataza tusile…

Na kuna tofauti ya “chakula cha sherehe” na “chakula cha sadaka”…Chakula kinachopikwa kwenye sherehe ya mtu asiyeamini sio chakula kinachotolewa sadaka, hata Bwana alialikwa mara nyingi na watu wenye dhambi na wasioamini na alikula …chakula kinachotolewa sadaka ni kwa mfano unakuta labda kuna msiba umetokea, na wahusika wananjinja kuku fulani maalumu wa kimatambiko na damu yake imemwagwa sehemu fulani na nyama ya yule kuku inapaswa iliwe na watu fulani maalumu..sasa nyama ya yule kuku aliyefanyiwa matambiko ndio mfano wa chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, hicho ndio tunapaswa kuwa nacho makini…Lakini pilau iliyopikwa au chakula kingine chochote kilichopikwa kwenye huo msiba kisichohusisha matambiko sio chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu….Na sherehe ni hivyo hivyo.

1Wakorintho 10:25 “Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; 26 maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.

27 Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.

28 Lakini mtu akiwaambia, Kitu hiki kimetolewa kiwe sadaka, msile, kwa ajili yake yeye aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.

29 Nasema, dhamiri, lakini si yako, bali ya yule mwingine. Maana kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?

30 Ikiwa mimi natumia sehemu yangu kwa shukrani, kwa nini nitukanwe, kwa ajili ya kitu nikishukuriacho?

31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

32 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu,

33 vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.”

Kwahiyo ikiwa ni ndugu yako au jirani yako (labda ni muislamu au mhindu ), na amekualika kwake au kwenye sherehe yao na amekuandalia chakula kwajinsi anavyojua yeye…kula bila kuhojihoji hufanyi dhambi kwa Mungu….isipokuwa tu amekupa chakula kilichotolewa sadaka na amekueleza

Mada Nyinginezo:

Chapa zake Yesu ni zipi hizo?

 

SAKRAMENTI NI NINI, NA JE! IPO KATIKA MAANDIKO?

Kwanini Bwana aliongea na Abramu baada ya kutengeana na Lutu?

MUUNGANIKO WA MADHEHEBU NI MPANGO WA MPINGA-KRISTO.

https://wingulamashahidi.org/2018/06/27/maswali-na-majibu/

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Zile mbao mbili za mawe Musa alizoambiwa achonge zilikuwaje?

Biblia inamaanisha nini inaposema “Tusitweze unabii”?

RABI, UNAKAA WAPI?

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/05/25/je-kualikwa-kwenye-sherehe-za-watu-ambao-si-wakristo-ni-dhambi/