Eliya alipoagizwa na Mungu kuzifunga mbingu kwa miaka mitatu na miezi sita, aliagizwa aelekee, karibu na kijito cha kedroni, na huko Mungu atamuhudumia kupitia kunguru kumleta mkate na nyama, asubuhi na jioni.
1 Wafalme 17:2-6
[2]Neno la BWANA likamjia, kusema, [3]Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. [4]Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. [5]Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. [6]Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
[2]Neno la BWANA likamjia, kusema,
[3]Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani.
[4]Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko.
[5]Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.
[6]Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
Unaweza ukajiuliza kwanini hakumwagizia malaika wake kama alivyomfanyia wakati ule anaelekea mlima Herobu (1Wafalme 19:4-8), au kwanini asimwagizie mtumishi wake, au mnyama safi kama huwa (njiwa), kinyume chake anamuagizia kunguru mnyama mchafu na najisi.
Kwa wakati ule ndege hawa waliwekwa miongoni mwa ndege wachafu wa hali ya juu sana. Hivyo chochote kilichoguswa na wanyama hawa hakikuliwa..lakini Mungu alimwagiza Kunguru huyo huyo amletee Eliya chakula.
Mara nyingi njia na kanuni za Mungu hazichunguziki, Si kila wakati Mungu atatumia watu wema sana, kama tunavyodhani kutuhudumia kimahitaji.
Kunguru hajui kusoma, hakujui kuandika, lakini alisikia agizo la Mungu.
Watu hawa rohoni si lazima wajue theolojia, wajue kanisa, wajue njia za haki, lakini Mungu akiwaamuru, watafanya tu.
Kwanini Mungu anafanya hivi wakati mwingine, ni kutushusha kiburi chetu, na kumwachia hukumu yote yeye mwenyewe.
Mungu anaweza kumwagiza mtu wa dini nyingine, kuisapoti huduma yako. Lakini hilo lisimaanishe kwamba Mungu amemkubali..
Anaweza kutumia maskini, kukutoa mahali fulani na kukupeleka kwingine, anaweza tumia mtu nje ya duara lako, kutenda kitu kwako wewe mwana wa Mungu.
Huyo unayemdhania kwenye akili yako, anaweza asifanye, yule usiyekuingia akilini ndio akatumiwa kufanya.
Eliya angeweza kusema Aah! Bwana…umeshindwa kuniletea Gabrieli, mbona nisingenajisika, lakini Bwana anasema kunguru ndiye nimemwagiza kwako.
Swali, vipi kama kunguru ndiye anayekufadhili kwasasa…Je utamlaumu Bwana?
Kumbuka uumbaji wote bado unamtii Mungu, haijalishi umetengwa naye, kwa umbali mrefu kiasi gani. Bado ni milki ya Bwana.
Mjue sana Mungu ili uwe na amani!
SALA.
Bwana Yesu! Asante kwa kunifumbua macho yangu na kunijuza kuwa ulimwengu wote unakutii wewe, naomba niwe mwepesi kupokea neema zako mbalimbali kwa namna ambayo zinatimiza mapenzi yako, bila mimi kunajisika. Asante kwa hilo, nimeamini, nimepokea. Amen.
Shalom.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ