MTAZAME BWANA

MTAZAME BWANA

Jina la Bwana na Mwokozi wetu YESU KRISTO, libarikiwe daima.

Ipo faida kubwa sana ya kumwangalia Bwana, na Bwana kukuangalia wewe.. Wengi tunapenda Bwana atuangalie ila sisi tusimwangalie, hebu tutazame faida moja ya Bwana kutuangalia sisi na sisi kumwangalia Bwana, kwa kutafakari mfano ufuatao.

Mtu aliyemama mbele yako ukimtazama naye akikutazama, ni wazi kuwa mbele yake ni nyuma yako wewe na nyuma yake ni mbele yako wewe, kwasababu mnatazamana, tofauti na kwamba mngetazama wote upande mmoja, endapo mngetazama wote upande mmoja mbele yako ingekuwa ni mbele yake pia, na nyuma yako ni nyuma yake pia.

Sasa Bwana anapotutazama sisi yale mambo yetu yaliyopita kwake ni kama yajayo, na yale yajayo ni kama yaliyopita… Kwahiyo wakati tunawaza nini kitatokea kesho, tayari Bwana alishakipanga na kukimaliza, wakati tunawaza ni mambo gani na gani yatatupata miaka 10 au 20 ijayo tayari Bwana alishashughulika nayo zamani, kwani mbele yetu sisi ni nyuma ya Bwana muda mrefu sana.

Vile vile mambo yetu yaliyopita ambayo yanaonekana kama hayawezi kutengenezekeka tena, hayawezi kurekebishika tena, kwa MUNGU wetu yanakuwa ni mambo yanayotengenezeka na ni mambo yanayopangika, kinachotakiwa ni kitu kimoja tu!… nacho ni kumwangalia Bwana.

Yeremia 31:28  “Tena itakuwa, kwa kadiri NILIVYOWAANGALIA, ili kung’oa, na kubomoa, na kuangusha, na kuangamiza, na kutesa; kwa kadiri iyo hiyo nitawaangalia, ili kujenga, na kupanda, asema Bwana”.

Tunamwangaliaje Bwana?.. Kwanza kwa kuungama makosa, na kutembea katika Neno lake, hapo Bwana pia atatuangalia kwasababu siku zote pia analitazama Neno lake apate kilitimiza (Yeremia 1:12).

Usiangalie matatizo yanayokuzunguka, bali mwangalie Bwana, usiangalie mambo ya kutisha yanayojiandaa kutokea wewe mtazame Bwana, usiangalie mambo yaliyopita yaliyoharibika wewe mwangalie, kwani unayoyaona kama hayawezi tena kurekebika BWANA anaweza kuyafanya upya tena, na unayoona kama hayataweza kutimia kwa Bwana mambo yako yajayo kwake ni kama yaliyopita, endapo ukimtazama.

Mtazame  Bwana!, Mtazame Bwana!.

Maran atha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255693036618 au +255789001312

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je YESU KRISTO alikuwa na wadogo zake?

Tafsiri ya Wakolosai 2:18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu,

ZIDI KUTAFUTA UJAZO WA ROHO MTAKATIFU.

UJIO WA BWANA YESU.

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply