TUMIA MUDA VIZURI.

TUMIA MUDA VIZURI.

Kitu pekee ambacho tumepewa na MUNGU kinachofanana kwa viumbe vyote ni “muda”..  Tunaweza tofautiana rangi, kimo, ukubwa, umri, utajiri, heshima, umaarufu, cheo, mamlaka n.k lakini hatuwezi kutofautiana muda.

Hata “Mchana” una muda sawa na “usiku” mgawanyo wa masaa 12, Bwana MUNGU hajaupendelea mchana kwa kuupa masaa mengi kuliko usiku, bali utaona usiku na mchana muda ni ule ule.

Mchana unaweza kuwa umependelewa kwa mambo mengi kuliko usiku.. lakini kwenye suala la muda, haujapendelewa, maana yake mambo yanayopaswa kufanyika mchana kwenye nuru na utukufu, yasipofanyika kwa masaa 12, basi giza litaingia na kutawala kwa masaa yale yale 12, ndio maana Bwana YESU alisema maneno hivi..

Yohana 11: 9 “Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.

10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake”.

Na yeye mwenyewe Bwana YESU alitumia muda vizuri sana na pia alitufundisha kuutumia muda vizuri..

Yohana 9:4 “Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka, maadamu ni mchana; usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi.”

Umeona?.. muda ni kitu cha kuzingatia sana kwetu sote….hata ibilisi anazingatia sana muda, hafanyi mchezo na muda kabisa… kwani anajua, ukiisha huo hawezi tena kuuongeza..

Ufunuo 12:12 “ Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, AKIJUA YA KUWA ANA WAKATI MCHACHE TU”.

Hivyo na sisi ni lazima tujifunze kutumia muda vizuri..

SASA TUNAUTUMIAJE MUDA VIZURI?.. tusome maandiko yafuatayo..

Waefeso 5:15 “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16 MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu

17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, BALI MFAHAMU NI NINI YALIYO MAPENZI YA BWANA.”

Kulingana na maandiko hayo ni dhahiri kuwa tunaukomboa muda “KWA KUYAFAHAMU NA KUYATENDA MAPENZI YA MUNGU”.

Mtu asiyeyafanya mapenzi ya MUNGU ni mtu anayetumia muda vibaya, na mapenzi ya MUNGU ni yale yaliyotajwa katika..

1Wathesalonike 4:2 “Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.

3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;

4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;

5 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu”.

Kwa urefu juu ya somo la “namna ya kuyajua mapenzi ya MUNGU na kuyafanya” basi wasiliana nasi kwa namba zilizopo mwisho wa ujumbe huu.

Je umeokoka?.. kama bado fahamu kuwa muda inakimbia kuliko kawaida, unavyozidi kukawia ndivyo mlango unavyozidi kuwa mwembamba zaidi, fanya uamuzi wa busara leo kumpokea BWANA YESU na atakusaidia kushinda dhambi.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JIWEKE TAYARI KUYAFANYA MAPENZI YA MUNGU.

YAFAHAMU NA YATENDE MAPENZI YA MUNGU.

JE UNAYAFANYA MAPENZI YA MUNGU?

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

ATAWAFANYIA WAMCHAO MATAKWA YAO.

About the author

Nuru ya Upendo administrator

Leave a Reply