Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao.

by Admin | 17 February 2020 08:46 pm02

SWALI: Biblia inamaana gani kusema   “Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa;nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza”.(1Timotheo 5:11-12).

Ni kwanini wahukumiwe kwa kuolewa kwao tena, wakati biblia inaruhusu wajane kuolewa?


JIBU: Kama ukisoma kuanzia mistari ya juu utaona zamani za mitume kulikuwa na utaratibu wa kuwakumbuka wajane katika posho la kanisa..Na kulikuwa na masharti yake ili uweze kuandikwa,

1Timotheo 5:1 “Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja”;

1Timotheo 5.10  “naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema”.

5.4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.

5.5  Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku.

Hivyo mjane yeyote ambaye alikuwa amekidhi hivyo vigezo basi alikuwa anaruhusiwa kuandikwa katika kanisa, na kanisa lilikuwa linawatambua watu kama hao, na walikuwa wanatengewa fungu lao maalumu.

Lakini sasa kama tayari alishajitoa kikamilifu kwa Bwana namna hiyo, ameshaingia katika nadhiri kama hizo kwamba tumaini lao lote sasa ni kwa Bwana tu, mpaka anafikia hatua ya kuchukua uamuzi wa kwenda kuandikwa katika kitabu cha kanisa kwamba ni yeye ni mjane kweli kweli aliyemwekea Mungu tumaini lake lote, halafu inatokea ghafla tu anageuka na kutaka  kuja kuolewa tena….Sasa katika mazingira kama hayo watu wa namna hiyo maandiko haya ndio yanayowahusu.

5.12 wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza..

Na ndio maana mtume Paulo akatoa angalizo kabisa, wajane wazee ni heri wasiandikwe waolewe, kwa namna nyingine ni kwamba  kama wanajijua siku moja  watakuja kuolewa basi wasijiingize katikati  ya wajane kweli kweli waliodhamiria kumuishia Mungu maisha yao yote vinginevyo watakuwa wanajitafutia hukumu ya bure..wakizidiwa na tamaa.

Ubarikiwe.

Mada Nyinginezo:

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Je! Ni sahihi kwa mkristo kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine?

NDOA NA TALAKA:

KUSUDI LA MIMI KUWEPO DUNIANI NI LIPI?

JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

Kwanini kila nikitaka kusali naingiwa na uvivu?

USILALE USINGIZI WAKATI WA KUMNGOJEA BWANA.

CHUKIZO LA UHARIBIFU

Rudi Nyumbani:

DOWNLOAD PDF
WhatsApp

Source URL: https://wingulamashahidi.org/2020/02/17/bali-wajane-walio-vijana-ukatae-kuwaandika-hao/