Kisiwa cha Patmo kipo nchi ya Ugiriki kwa sasa…Kisiwa hicho kipo mashariki mwa Taifa la Ugiriki na magharibi mwa nchi ya Uturuki, kama vile Zanzibar ilivyo mshahariki mwa nchi ya Tanzania ndivyo kilivyo hichi kisiwa cha Patmo kwa Ugiriki.
Kisiwa hicho ndicho Mtume Yohana, ambaye alikuwa mwanafunzi wa Bwana Yesu, alifungwa.
Warumi walimkamata Yohana na kumtupa katika kisiwa hicho, kwa lengo la kumtesa kwa kosa la kumhubiri Yesu. (Kwa maelezo kwa njia ya sauti, fungua hapa chini)
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=EhBLp-8-vPw[/embedyt]
Lengo la kumtupa Yohana katika kisiwa hicho cha Patmo, sio tu afe, bali afe kwa mateso. Kwani kisiwa hicho hakikukaliwa na mtu yeyote wakati huo, kwasababu kilikuwa ni kisiwa ambacho hakistawi nafaka, wala miti na zaidi sana, kilisifika kuwa na nyoka wengi.
Kwahiyo yoyote aliyetupwa katika kisiwa hicho, ilikuwa ni lazima afe kama hatakuja kuokolewa huko.
Lakini tunasoma, Yohana alipelekwa kule, kwaajili ya ushuhuda wa Neno la Mungu, wakati Jeshi la Warumi linaona limempeleka kwaajili ya mateso, yeye Yohana alijiona amepelekwa kwaajili ya ushuhuda…Kwamba akashuhudie mambo atakayokwenda kufunuliwa au kuambiwa na Mungu huko.
Ufunuo 1:9 “Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu”
Hii ikifunua kuwa sio kila jaribu baya, lengo lake ni baya!. Yohana asingepelekwa Patmo, tusingekuwa na kitabu cha ufunuo, hali kadhalika Bwana Yesu asingepelekwa msalabani, tusingepata wokovu.
Kisiwa cha Patmo, sasahivi kinakaliwa na watu, kutokana na kuongeza kwa idada kubwa ya watu ulimwengu na yenye kuhitaji makazi..vile vile, kuongezeka kwa teknolojia ya mawasiliano, na usafiriwa wa haraka, umekifanya kisiwa hicho kiweze kukalika na watu leo.
Kisiwa cha Patmo, jina lake mpaka leo halijabadilika, kinaitwa hivyo hivyo Patmo, kama vile Yerusalemu jina lake lisivyobadilika siku zote.
Wakazi wa kisiwa cha Patmo kwasasa hawazidi 4,000 kulingana na sensa za Ugiriki.
Na kisiwa hicho, hakina miujiza yoyote ya kiroho, kwamba yeyote afikaye kule basi atapata ufunuo kama aliopata Yohana.
Bwana akubariki.
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kutakabari ni nini katika biblia?.
Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?
Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?
KWANINI KRISTO AFE?
Rudi nyumbani
Print this post
Shalom,kazi yenu njema.
Asante kwa somo hili.
Je ni mwanamke gani alikuwa mitume katika biblia
Hakuna mwanamke yeyote aliyekuwa mtume katika biblia
Amina asante sana. Na Mungu akubariki.
Amen Amen🙏🙏🙏
Mbarikiwe
Amen 🙏
Amen
Swali; Yohana alitokaje tokaje katika kisiwa hicho, kwa maana warumi walimtupa Kule na kumtelekeza, ndipo baadae Bwana Yesu anampa ule ujumbe wa Makanisa saba… Je alitokaje Kule patmo.??
UBARIKIWE.
Amina
Amen, Mtumishi wa Mungu ubarikiwe
Mungu ni mwema sana
Swali; Yohana alitokaje tokaje katika kisiwa hicho, kwa maana warumi walimtupa Kule na kumtelekeza, ndipo baadae Bwana Yesu anampa ule ujumbe wa Makanisa saba… Je alitoka Kyle patmo.??
Biblia haijaeleza alitokaje tokaje huko..labda hao hao warumi walikuja kumtoa, au kuna watu walipita na mashua pembezoni mwa kisiwa hicho na kumwona na kumtoa..
Lakini kwa njia yotote ile alitoka kule, na kupeleka hizo jumbe kwenye hayo makanisa…
Amen.
Amina somo nzuri sana
Amen shea na wengine…
Amen amen