Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?

Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?

Marko 3:16 “Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina la Petro;

17 na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo”.

Wana wa Zebedayo (yaani Yakobo na Yohana), walipewa jina hilo la Boarnege kwasababu ya ukaribu wao kwa Bwana.

Ikumbukwe kuwa ni wanafunzi watatu tu! Peke,e ndio waliobadilishwa majina na Bwana, na hao ni Petro, Yohana na Yakobo, Ambao biblia inawataja kama NGUZO! (Soma Wagalatia 2:9). Wakati Bwana akienda mlimani kusali hawa nao walikuwa Pamoja naye! (Soma Mathayo 17:1)..hawa walimpenda Bwana sana kuliko wale wanafunzi wengine 9 waliosalia.

Yakobo na Yohana ulifika wakati walikwenda kumwomba Bwana awaketishe mkono wa kuume na wa kushoto katika ufalme wake siku ile.

Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.

21 Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.

23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu”.

Umeona?

Hivyo hawa wana wa Zebedayo Pamoja na Petro siku zote walikuwa wanatamani kumsogelea Bwana sana, na Bwana aliijua mioyo yao!.

Kutokana na mapenzi hayo kwa Bwana, walikuwa ni watu wasiopenda kuona Bwana anakataliwa mahali popote!.. Utaona Petro, alimkata mtumwa wa kuhani mkuu sikio, kipindi ambacho walikwenda kumkamata Bwana. Halikadhalika Yohana na Yakobo walitaka Bwana ashushe moto kuwaangamiza watu wa Samaria kipindi kile walichomkataa.

Luka 9:51 “Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;

52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.

53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.

54 wanafunzi wake YAKOBO NA YOHANA walipoona hayo, walisema, BWANA, WATAKA TUAGIZE MOTO USHUKE KUTOKA MBINGUNI, UWAANGAMIZE; [KAMA ELIYA NAYE ALIVYOFANYA]?

55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]

56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”.

Umeona hapo?.. Tabia hiyo ya “kutaka Moto ushuke kutoka mbinguni” ni tabia za KUNGURUMA.. Moto hauwezi kushuka kabla mbingu hazijanguruma, sauti ya Ngurumo ni sauti ya Hukumu iliyokaribu au ya adhabu!.

Hivyo Bwana aliiona tabia hiyo ndani yao, kwamba siku za mbeleni baada ya kuondoka kwake, watakuja kunguruma juu ya kazi zote za shetani, na kuziteketeza!.. kipindi hicho watakuwa hawafanyi vita juu ya damu ya nyama, kama walivyotaka kufanya juu ya hawa watu wa Samaria,(kutaka kuwaua kwa moto) bali wakati huo, watanguruma juu ya kazi zote za shetani katika ulimwengu wa roho na kuzichoma na kuwaacha watu wa Bwana huru!.

Maran atha!

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

NGURUMO SABA NI NINI?

KAMA VILE UMEME UTOKAVYO MASHARIKI UKAONEKANA HATA MAGHARIBI.

Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?

UFUNUO: Mlango wa 1

Maswali na Majibu

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Devis Julius administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments