Jibu: Kutakabari maana yake ni “kuwa na kiburi”…Na hicho kinaweza kuja kutokana na kujiamini sana, au kuwa na kitu fulani ambacho wengine hawana, na kujiona huhitaji kitu kingine chochote…Kutakabari huko kunazaa kujisifu au kujiona bora kuliko wengine, na kujiinua sana hata kudharau wengine au kumdharau Muumba.
Katika biblia tunaweza kuona mifano kadhaa ya watu waliotakabari..
Huyu alikuwa mtoto wa Mfalme Daudi, wakati Daudi alipokuwa mzee, alijiona yeye ni bora kuliko watoto wengine wote wa Daudi, hata pasipo kumshirikisha baba yake, akaenda kujitangaza kwa watu kuwa yeye ndiye mfalme, angali bado baba yake akiwa hai.
1Wafalme 1: 5 “Ndipo Adonia mwana wa Hagithi AKATAKABARI, akasema, Mimi nitakuwa mfalme. Akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, na watu hamsini wapige mbio mbele yake”.
Lakini tunaona badae hakupata hicho alichokuwa anakitafuta, na nafasi hiyo alipewa Sulemani.
Wana wa Israeli ilifika wakati walimwacha Mungu, na hata kufikia hatua ya kuwatukana na kuwadharau manabii wake, na kupelekea ghadhabu ya Mungu kumwagwa juu yao kwa kuuawa na baadhi yao kupelekwa Babeli utumwani.
2Nyakati 36:15 “Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake; 16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na KUYADHARAU MANENO YAKE, NA KUWACHEKA MANABİİ WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya. 17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake”
2Nyakati 36:15 “Naye Bwana, Mungu wa baba zao, akatuma kwao kwa mikono ya wajumbe wake, akiondoka mapema, na kutuma; kwa sababu aliwahurumia watu wake, na makao yake;
16 lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, na KUYADHARAU MANENO YAKE, NA KUWACHEKA MANABİİ WAKE, hata ilipozidi ghadhabu ya Bwana juu ya watu wake, hata kusiwe na kuponya.
17 Kwa hiyo akaleta juu yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao kwa upanga nyumbani mwa patakatifu pao, asiwahurumie kijana wala mwanamwali, mzee wala mkongwe; akawatia wote mkononi mwake”
Kutakabari huko kwa wana wa Israeli ndiko kukapelekea kuchukuliwa utumwani.
Nehemia 9: 29 “ukawashuhudia ili uwarudishe tena katika sheria yako; LAKINI WALITAKABARI, wasizisikilize amri zako, bali wakazihalifu hukumu zako, (ambazo mtu akizitenda ataishi katika hizo), nao wakayaondoa mabega yao, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wasitake kusikiliza”.
Yeremia 48: 29 “Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi ALIVYOTAKABARI moyoni mwake. 30 Najua ghadhabu yake, asema Bwana, ya kuwa si kitu; majisifu yake hayakutenda neno lo lote. 31 Kwa sababu hiyo nitampigia yowe Moabu, naam, nitapiga kelele kwa ajili ya Moabu yote; nitawaombolezea watu wa Kir-heresi”.
Yeremia 48: 29 “Tumesikia habari za kiburi cha Moabu; Ya kuwa ana kiburi kingi; Jeuri yake, na kiburi chake, na majivuno yake, Na jinsi ALIVYOTAKABARI moyoni mwake.
30 Najua ghadhabu yake, asema Bwana, ya kuwa si kitu; majisifu yake hayakutenda neno lo lote.
31 Kwa sababu hiyo nitampigia yowe Moabu, naam, nitapiga kelele kwa ajili ya Moabu yote; nitawaombolezea watu wa Kir-heresi”.
Na mfano wa wengine waliotakabari kupita kiasi ni Farao (soma Nehemia 9:10), Nebukadneza (Danieli 4:37) n.k
Madhara ya kutakabari.
Tukiwa watu wa kutakabari Tutaanguka kama walivyoanguka wana wa Israeli na wengine wote waliokuwa wakitakabari katika biblia..
Mithali 16: 18 “Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye KUTAKABARI hutangulia MAANGUKO”.
Bwana atusaidie tusiwe na roho ya kutakabari..bali tuwe wanyenyekevu kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa..
Kama hujaokoka na ungependa kufanya hivyo leo..basi utakuwa umefanya uamuzi bora ambao hutaujutia maisha yako yote.. Fungua hapa kwa msaada wa sala ya Toba >> SALA YA TOBA
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JIHADHARI NA DHAMBI YA WIVU/HUSUDA.
Kwanini Mungu alisema hakuna mtu awazaye kuuona uso wake akaishi?
Je! Kuna dhambi kubwa na ndogo, na kama hakuna je! Mtu aliyeua na aliyetukana je watapata adhabu sawa?
MIGUU ILIYO MYEPESI KUKIMBILIA MAOVU, NI CHUKIO KWA BWANA.
WANA JUHUDI KWA AJILI YA MUNGU, LAKINI SI KATIKA MAARIFA.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Kweli mungu I nimushinfi
Amen ubarikiwe..